Lissu bhana ni mwana sharia mzuri sana, sema ni mlopokaji na temper yake pia ni kubwa, sikubaliani na shambulio la kutoa uhai wowote wa raia iwe mwana siasa au raia wa kawaida, lakini kabla ya shambulio tundu lissu alishaonyesha dalili kibao na negative nyingi katika serikali ya awamu ya tano, hata ukiwa mpinzani lazima ujue pia kuna serikali ,fanya mambo ya kipinzani lakini kumbuka serikali ipo na fuata sharia ,ni tundu huyu huyu ndio kaja na neon dictactor uchwara mbele ya vyombo vya habari, tyrant , tutamnyoosha magufuli ,kumbukeni tundu lissu mdomoni ni mzima balaa, halafu bila break na kujitengenezea maadui yeye mwenyewe bila kujua, mimi baada ya shambulio nilitoa tu ushauri kuwa tundu lissu atulie aachane na mambo ya kupigana na serikali, hata shinda, ni ngumu kushindana na serikali, hata ukilala USA na ukawa na meeting kila siku na trump sijui nani bado huwezi shinda, ni bora atulie alee watoto wake, mimi nina mfano wa Dai laima, alikuwa kila siku yupo hapo USA, ilifika muda hata Obama ana mkacha.
Mtandao wa serikali ni mkubwa kama wana nia ovu na lissu kama wengi tunavyoamini, inaweza kumdhuru mahali popote alipo, mungu aniepushe mbali kwa kauli hii, hivyo yeye atulie au afanye siasa za kwa njia tofauti, ana familia na watoto wana mtegemea , ni bora tuseme ukweli tumuepishe na majanga mengine.
Miguna miguna yuko wapi, aligoma eti yeye hatoki chini Kenya ,waka dunga sindano akajikuta yuko kwenye pipa anakwenda Canada by force, halafu akasindikizwa na somebody mwandishi wa habari Kenya ambaye yuko karibu na utawala wa sasa , akawa anamwangalia tu, hizi case zote zipo, sio kwamba zina halalisha maovu no zinatufundisha nini kama wanasiasa wajao pengine, tufanye mabadiliko lakini kwa makini.