Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anatumia muda mwingi kutafsiri Katiba na Sheria badala ya kutangaza sera?


Naona inakuuma sana kuona watanzania wanafunguliwa kutoka utumwani. Kutokujua sheria watanzania wengi ndo mtaji wa CCM kunyanyasa watu
 
Katiba ya nchi ndio dira kuu ya kuendesha nchi iwe kisiasa na mambo mengine yoote, ni vigumu kuikwepa katiba ya nchi hasa hasa kama una ndoto za kuongoza nchi pia maswali mengi anayokutana nayo kuulizwa ni ya kikatiba ivi kwani huoni watu wamemuelewa haraka kila siku makundi ya watu yanaongezeka
 
Anaelezea jinsi sheria zilivyokua zinavunjwa hapo nyuma na pia yapaswa mtu ajue kosa lake na utaratibu wa kuitwa kuhojiwa sio kienyeji kama walivyofanya hiyo tume so ni muhimu watu wawekwe wazi anapokosea na hatua anayochukua kwa uwazi! Tatizo wengine hamtaki watu wafahamu haki zao!
 
Yaani Leo katoa Pasi ya ovyo kabisa katika harakati zake za kujijenga kimaslahi. Sijui kama mnaona ninachokiona kwa Lissu. Au ndiyo mmeamua kuvaa miwani ya 'mabao'? Ebu vueni miwani hiyo!
Na Yule anayewadhalilisha wanawake ndo mwenye pasi kali?!!
 
Awe anatangaza Sera, au asitangaze nitamchagua hivyo hivyo. Nimeumizwa sana na utawala wa huyu mzee, Mimi namtumia mama yangu ela ya matumizi yeye analipia kitambusho.
 
Belezee baba
 
Jitahidi Sana kuwa mkweli ! MUNGU anampenda mtu mkweli . Tusipende kuupotosha Umma !!!
 
Jitahidi Sana kuwa mkweli ! MUNGU anampenda mtu mkweli . Tusipende kuupotosha Umma !!!
Umetazama ITV leo usiku? Uongo kwangu mwiko.

Nakuwekea ushahidi. Tazama channel ya ITV kupitia youtube kwenye link hapa chini. Kuanzia dakika ya 8:33 mpaka 11:44.



Karibu usione aibu.
 
Haki, Uhuru na Maendeleo ya Watu...somo la Uraia ni muhimu maana Magufuli na Tume wamekuwa wakikanyaga Katiba na Sheria waziwazi
 
Ni mbinu nzuri sana ya kuwaelimisha wananchi kabla ya kumwaga sera na wengi tumefunguliwa macho tupo tayari kumpa kura zetu sasa.
 
Sheria na katiba ndio msingi wa uongozi ktk nchi.


Kwann John anatumia muda mwingi kutembea na wasanii ?
 
anatueleza mambo ya sheria ili tujue haki zetu na kuzipigania hata ikibidi kuingia barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…