Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anaweza kuwa kiongozi mzuri wa Taifa?

Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anaweza kuwa kiongozi mzuri wa Taifa?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
1. Anaijua sheria ataongoza taifa kwa misingi ya haki

2. Hana tamaa ya mali, hatokimbilia kujenga mahekalu kwa na kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwao Mahambe, hawezi, hawezi hubadili msitu wa Mahambe kua hifadhi ya wanyama.

3. Ni muelewa mzuri wa masuala ya kimataifa, atasaidia kuimarisha diplomasia ya kimataifa

4. Hatorusu kuingia mikataba ya kinyonyaji kwa sababu ni mjuzi wa sheria

5. Hana rekodi ya ufisadi wala tuhuma zozote rushwa. Ni mwadilifu

6. Haturuhusu DPP kuchelewesha kesi mahakamani kusababisha mrundikano wa wafungwa

7. Hatoruhusu ubambikiaji wa kesi na uonevu unaofanywa na baadhi ya polisi
 
Tanzania hatupo tayari kuongozwa na mtu anaeji brand kuwa yeye Ni mkenya kwasabab ana damu nyingi ya Kenya. Mwisho wa siku akiingia ikulu ashirikiane na wakenya wenzake kuiuza Tanzania kwa Mabosi wake wa Ubelgiji.
 
8. Atatokomeza wasiojulikana tutaishi kwa amani ya moyo.
wewe unajikuta heti huishi kwa Amani.
Kwa maisha gani uliyonayo yani wewe hata ukienda kulala polini ukiondoa kudhuliwa na wanyama wakali utabaki salama kabisa.

Mtu hujawahi hata kusikia mlio wa bunduki tangu uwepo hapa Tanzania ndo unakuwa wa kwanza kuleta unafiki wako hapa.

Siasa Ni Mbaya Sana .
 
na wewe unajikuta heti huishi kwa Amani.
Kwa maisha gani uliyonayo yani wewe hata ukienda kulala polini ukiondoa kudhuliwa na wanyama wakali utabaki salama kabisa.

Mtu hujawahi hata kusikia mlio wa bunduki tangu uwepo hapa Tanzania ndo unakuwa wa kwanza kuleta unafiki wako hapa.

Siasa Ni Mbaya Sana .
Soma vizuri nilichondika , amani ya moyo. Lissu akiwa rais tutaishi bila hofu ya kutekwa.
Mlio wa bunduki niliushuhudia kinondoni alipouawa Akwilina (RIP).
Pinga kwa hoja kama anavyofanya Lissu sio kwa povu.
 
Kusema kweli tunajisumbua tu.. Tundu Lissu hawezi kuwa Rais sio kwasababu kura hazitatoshaa bali ni kwasababu ya corwadice ya Watanzania..

Atachaguliwa tena kwa kura nyingi kuliko watu wanavofikiria kama kuna mwaka ambao CCM itasambaratika ni baada ya matokeao ya uchaguzi kutangazwa Mungu anataka kuliinua hili taifa ambalo limebarikiwa kuwa na utajiri mwingi, lakini watu wake ni masikini wa kutupwa.
 
Tanzania hatupo tayari kuongozwa na mtu anaeji brand kuwa yeye Ni mkenya kwasabab ana damu nyingi ya Kenya.
Mwisho wa siku akiingia ikulu ashirikiane na wakenya wenzake kuiuza Tanzania kwa Mabosi wake wa Ubelgiji.

Hajajibrand kuwa ni Mkenya amesema ana damu ya wakenya sababu aliwekewa damu nyingi akiwa anatibiwa sasa kusema hivo ndo imekuwa shida, maneno mengine yaani hata hofu ya Mungu hatuna.
 
Mr Tyang una maana kuwa Tz hatujawahi kuongozwa na mtu asiye Mtanzania? Hiyo ya kuwekewa damu ya mtu haibadili wewe kuwa mtu yule.Acha kubabaisha wajinga!
 
Sasa hizi ni sifa za Rais au za Jaji Mkuu? Hivi nyinyi watu mbona hamjielewi? Ni tatizo la Elimu au Umbumbumbu?
 
1. Anaijua sheria ataongoza taifa kwa misingi ya haki

Kwanini.. ana kesi.. mingi mahakamani!!
Kwanini.. hatumii wa nchini.. kumuwakilisha.. anatumia wazungu wa ofisi za nje ta nchi.!!!.. kwanini mgomvi sana.. na mvunja sheria makusudi!!!.. na kuhimiza fujo nchini!!!
 
Msingi mkuu wa maendeleo ya watu na vitu ni Haki, utawala wa Sheria, Diplomasia ya Uchumi na Uwekezaji mpana wa kitaifa na kimataifa (Wageni na Wazawa)

Sina mashaka na Lissu na Chadema kwenye uwezo wao wa kufanikisha haya yote!!
 
Kwanini.. ana kesi.. mingi mahakamani!!
Kwanini.. hatumii wa nchini.. kumuwakilisha.. anatumia wazungu wa ofisi za nje ta nchi.!!!.. kwanini mgomvi sana.. na mvunja sheria makusudi!!!.. na kuhimiza fujo nchini!!!
Atumie mawakili wa ndani muwafutie uwakili kama Fatma Karume??? Mpige mabomu ofisi zao kama mlivyofanya kwa kampuni ya Imma advocates???!

Lissu kawashika pabaya sana Mataga na Lumumba!!! Poleni sana, jiandaeni tu kumkabidhi nchi hapo October kwa amani, maana hakuna namna!!
 
Serikali ya awamu ya awamu ya 6 licha ya kuzidi kujikita ktk kuyaendeleza mambo mazuri yaliyokwisha kuanza kutekelezwa kupitia kodi za wananchi, kwa namna ya pekee itunge sera rafiki zenye uwezo wa kuwakwamua kiuchumi wakulima maskini na hasa wengi wao waishio vijijini.

Awamu hii isije kutuletea tena miradi mingine mikubwa yenye kugharimu fedha nyingi kwa gharama ya kuwanyima haki makundi mengine ya watu mathalani wafanyakazi. Serikali iwe tayari kutoa majibu ya uhakika hata kama yatabeba ukweli mchungu, kuliko kutafuta visingizio vingi na porojo tupo zenye kubeba ahadi za uongo.
tapatalk_1594260968709.jpeg
 
Back
Top Bottom