Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anaweza kuwa kiongozi mzuri wa Taifa?

Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anaweza kuwa kiongozi mzuri wa Taifa?

Mtatatizo makubwa mara ngapi mbona tuna mtatizo makubwa tayari? Ccm must go!

Wewe jidanganye na mawenge yako. Lissu huyu huyu aliye na jeuri na kufuru ya kumdharau hata Mungu? JPM aliweka wazi kuhusu corona pamoja na hatua zote nyingine tulizo chukua lakini alituhimiza kama taifa la watu wenye hofu ya Mungu, tumuombe na kumtegenea Mungu. Tukaona muujiza corona ilovyofifia hapa Tanzaniia.

Lissu alipokuja kutoka ughaibuni akanza kuiaminisha dunia corona Tanzania iko kwa wingi ba watu wanakufa sana ila hakuna uhuru wa vyombo vya habari hivyo ukweli unafichwa.

Kwa maana nyingine alikuwa anasema hakuna Mungu huyo watanzania walio waaminisha dunia kuwa kawapigania katika corona. Hii ni kufuru inayo weza kufanywa na shetani na huyu wakala wake. Akasema mambo ya kura katika uchaguzi hatamuachia Mungu ataitisha mandamano ya wanadamu. Mkristo ambaye hajui kuwa amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu.

Lakini angalia Mungu alivyomuumbua na kumfanya ajikwae katika kuchanganyikiwa, akiwa anautangazia ulimwengu upotoshaji wake kuhusu suala la corona Tanzania akawa hachukui tahadhari ya barakoa na hata wale anawahutubia mabarabarani wamekusanyika bila ya hofu ya corona na wala kuvaa barakoa.
 
1. Anaijua sheria ataongoza taifa kwa misingi ya haki

2. Hana tamaa ya mali, hatokimbilia kujenga mahekalu kwa na kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwao Mahambe, hawezi, hawezi hubadili msitu wa Mahambe kua hifadhi ya wanyama.

3. Ni muelewa mzuri wa masuala ya kimataifa, atasaidia kuimarisha diplomasia ya kimataifa

4. Hatorusu kuingia mikataba ya kinyonyaji kwa sababu ni mjuzi wa sheria

5. Hana rekodi ya ufisadi wala tuhuma zozote rushwa. Ni mwadilifu

6. Haturuhusu DPP kuchelewesha kesi mahakamani kusababisha mrundikano wa wafungwa

7. Hatoruhusu ubambikiaji wa kesi na uonevu unaofanywa na baadhi ya polisi
Yeye mwenyewe angekuwa anasimama mbele ya watu anatoa madini Kama hayo, angekubalika zaidi ya anavyojihisi shida yeye anapata wakati mgumu kuongea hivi.
 
Atumie mawakili wa ndani muwafutie uwakili kama Fatma Karume??? Mpige mabomu ofisi zao kama mlivyofanya kwa kampuni ya Imma advocates???!

Lissu kawashika pabaya sana Mataga na Lumumba!!! Poleni sana, jiandaeni tu kumkabidhi nchi hapo October kwa amani, maana hakuna namna!!

Andika lolote kujipoza..ukweli munaujua nyie wapiga tarumbeta mitandaoni.. huku roho zikiwauma.. munajua upinzani bado badoooooo..
Lissu hawezi kuchaguliwa na wananchi kuongoza hii nchi..kwa sasa mufurahie tu utalii wake.. na anavyopeta kwa kuona Hapa kazi tu ya Magufuli..
Ni ndotoni Lissu atakuwa Rais wenu..

Magufuli 2020💯
 
Hajajibrand kuwa ni Mkenya amesema ana damu ya wakenya sababu aliwekewa damu nyingi akiwa anatibiwa sasa kusema hivo ndo imekuwa shida, maneno mengine yaani hata hofu ya Mungu hatuna.

Watanzania walizuiwa kuchangisha damu pia walizuiwa kufanya maombi kwa ajili ya TAL.

Huyo anayesema TAL anajibrand kuwa ni Mkenya na ALAANIWE.
 
Hawezi kuwa Rais, mpaka aamue kubadili kinywa chake na maneno anayotamka.

Aanze kusema nini kwa mfano kwa kutumia huo "mdomo" wake?

kwamba, ni Magufuli aliyejenga reli ya kati Dar - Mwanza na Tabora Kigoma - Mpanda mwaka 1902 na siyo Mjerumani?

KWAMBA, Magufuli kachimba msingi tu wa ujenzi wa nyumba kule Chato na hajajenga INTERNATIONAL AIRPORT?

KWAMBA, Magufuli hakuzuia pesa ya matibabu ya Tundu Lissu kiongozi mwenzake kabisa wa kuchaguliwa?

KWAMBA, Tundu Lissu aanze kusema uongo na kumsifu yesu wa Kangi Lugola??
 
Mali ilikuwa hivi hivi
Mkuu unafananisha mataifa ya West na letu?? Kwanza hata usiseme Mali hapo Malawi tu walifanya hivyo. Ila unafikiri mifumo yao ni sawa na yetu??

Kuweza kuondoa utawala dhalimu kuna njia mbili tu. Kwanza, Jeshi linalojitambua (liasi na kumtoa Rais) na pili Mahakama huru ambayo itasimamia haki na uchaguzi ulio huru. Box la kura pekee halitaiondoa CCM madarakani hasilani..

Sasa jiulize, una Jeshi wala Mahakama ya kufanya hivyo?? Kama huna utaandamana siku moja tu utabondwa na hakuna atakayekutetea sio Jeshi wala Mahakama..
 
Aanze kusema nini kwa mfano kwa kutumia huo "mdomo" wake?

kwamba, ni Magufuli aliyejenga reli ya kati Dar - Mwanza na Tabora Kigoma - Mpanda mwaka 1902 na siyo Mjerumani?

KWAMBA, Magufuli kachimba msingi tu wa ujenzi wa nyumba kule Chato na hajajenga INTERNATIONAL AIRPORT?

KWAMBA, Magufuli hakuzuia pesa ya matibabu ya Tundu Lissu kiongozi mwenzake kabisa wa kuchaguliwa?

KWAMBA, Tundu Lissu aanze kusema uongo na kumsifu yesu wa Kangi Lugola??
Lissu awezi kupata uraisi, atausoma kwenye fom tu, kwanza ni mla rushwa mkubwa, alikula ela za Lowassa na kuanza Kalamba matapishi yake kirahisi, ana msimamo anayeyumbayumba afai kuwa kiongozi.
 
Lissu awezi kupata uraisi, atausoma kwenye fom tu, kwanza ni mla rushwa mkubwa, alikula ela za Lowassa na kuanza Kalamba matapishi yake kirahisi, ana msimamo anayeyumbayumba afai kuwa kiongozi.

Pole sana...

Naona una argue kimihemuko hemuko ya kiaunafunzi wa shule...
 
Kama hadi Lowassa tu alionekana ana sifa za kuwa kiongozi mzuri na watu wakampigia kura,hivyo sioni ajabu hata Lissu nae kuonekana kuwa na sifa za kuwa kiongozi mzuri. Nakumbuka watu walikuwa wanasema wakiambiwa wachague kati ya jiwe na ccm wao wakawa wanasema watachagua jiwe.
 
Lissu awezi kupata uraisi, atausoma kwenye fom tu, kwanza ni mla rushwa mkubwa, alikula ela za Lowassa na kuanza Kalamba matapishi yake kirahisi, ana msimamo anayeyumbayumba afai kuwa kiongozi.
Wewee, hiyo namba acha kabisa. Lissu hajawahi kula cha mtu ni msafi na hapendi ujinga. Lete ushahidi wa Lissu kushtakiwa popote kwa sababu ya Rushwa.

Lissu Rais 2020, hutaki kaa kimya ujionee.
Hahahaaaa #Niyeue2020
 
Hii notion ya mtu mmoja aje kutukomboa tuangeanza kutoa kwenye mawazo yetu.

Tanzania haiwezi kuendelezwa na mawazo ya mtu mmoja, Tanzania itaendelea kwa kuwa na Taasisi imara zitakazowatumia Wananchi.

Hii nikiingia nitajenga barabara, nitanunua madawati sijui nitanunua nini ni rubish.

Kwa nini Kiongozi asisiseme akiingia atatengeneza mfumo wa Serikali za Mitaa ambao utatengeneza pesa za kuweza kuhudumia shule zake, Hospitali n.k?

Haya mambo ya Suprime Leader yanatufelisha.
 
Wewee, hiyo namba acha kabisa. Lissu hajawahi kula cha mtu ni msafi na hapendi ujinga. Lete ushahidi wa Lissu kushtakiwa popote kwa sababu ya Rushwa.

Lissu Rais 2020, hutaki kaa kimya ujionee.
Hahahaaaa #Niyeue2020
2015 Lissu aliongea maneno kama yako kumsea Lowassa kuhusu tuhuma za ufisadi za Lowassa.
 
Atumie mawakili wa ndani muwafutie uwakili kama Fatma Karume??? Mpige mabomu ofisi zao kama mlivyofanya kwa kampuni ya Imma advocates???!

Lissu kawashika pabaya sana Mataga na Lumumba!!! Poleni sana, jiandaeni tu kumkabidhi nchi hapo October kwa amani, maana hakuna namna!!
uchumi wa kati
 
Back
Top Bottom