Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Mkuu usiwe na moyo mgumu kuamini. Ni kweli CCM ni wezi sana, lakini Mara zote huwa inategemea huyo aliye mbele yukoje? Kama ni muoga basi wote nyuma yake wanakuwa waoga mfano mdebwedo kama Lowassa unategemea ingekuwaje?Kusema kweli tunajisumbua tu.. Tundu Lissu hawezi kuwa Rais sio kwasababu kura hazitatoshaa bali ni kwasababu ya corwadice ya Watanzania.
Leo yupo Lissu, ambaye tunamuona hata akiwa jukwaani sio muoga na ujasiri wake hakuna mfanowe Tanzania nzima tokea 2015 awamu hii katili iingie madarakani.
Pia Lissu kesha sema habari ya kumuachia Mungu hilo wasahau maana wakiiba kitawaka. Na kwa dunia ya sasa watu wakiandamana hata kama ni wahuni kudai haki ya kura zao na mkaua hata mmoja hao "mabeberu" wanapata sababu ya kunyea debe wahusika, jee wanataka hilo?