Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,663
Binafsi Nakipongeza Chama Changu kwa kumteua huyu Nguli wa Sheria Tundu Lissu kukiwakilisha Chama katika Ngazi ya Rais kwa sababu ni mtu Sahihi na anaijua Sheria Vizuri.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WaTz ni pamoja na weweTatizo watanzania ni waoga sana, mtachezewa sana na watawala, ondoeni woga mtaheshiwa na watawala wenu maana hamjawahi kuwa na viongozi
Atumie mawakili wa ndani muwafutie uwakili kama Fatma Karume??? Mpige mabomu ofisi zao kama mlivyofanya kwa kampuni ya Imma advocates???!
Lissu kawashika pabaya sana Mataga na Lumumba!!! Poleni sana, jiandaeni tu kumkabidhi nchi hapo October kwa amani, maana hakuna namna!!
Amini nakwambia. Yule ni Raisi wako 2020-2025Kabisa una hakika ana shinda? Au unajipa moyo?
Dhambi hizi mkuu
Kama unaweza danganya nafsi yako, ...wewe katili
1. Anaijua sheria ataongoza taifa kwa misingi ya haki
2. Hana tamaa ya mali, hatokimbilia kujenga mahekalu kwa na kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwao Mahambe, hawezi, hawezi hubadili msitu wa Mahambe kua hifadhi ya wanyama.
3. Ni muelewa mzuri wa masuala ya kimataifa, atasaidia kuimarisha diplomasia ya kimataifa
4. Hatorusu kuingia mikataba ya kinyonyaji kwa sababu ni mjuzi wa sheria
5. Hana rekodi ya ufisadi wala tuhuma zozote rushwa. Ni mwadilifu
6. Haturuhusu DPP kuchelewesha kesi mahakamani kusababisha mrundikano wa wafungwa
7. Hatoruhusu ubambikiaji wa kesi na uonevu unaofanywa na baadhi ya polisi
Kapongo, uzalendo upi unauongelea ?!Lissu hafai hata kuwa Mkuu wa Wilaya. Sababu ni nyingi ila kwa uchache yeye si Mzalendo na licha ya ufahamu wake wa umajumui, lakini anajitoa fahamu kwa maksudi ama kimkakati, na kuamini kuwa maendeleo yetu bado yanategemea utegemezi wa kiakili na kifedha kutoka kwa mabeberu.
Ndio maana yupo radhi kutetea mirija ya mabeberu ( kwenye mikataba hovyo ya madini), kutoa siri za nchi kwa mabeberu, bila kujali athari zake kwa mustakabali wa nchi.
Kwa ukibaraka kama huo, iwapo kwa bahati au kwa ulevi tu wa kifikra, akapata fursa ya kuingia Ikulu ni hapana shaka tutarudishwa utumwani kwa mlango wa mbele kabisa, na hivyo kuchambia mafanikio ya Uhuru wetu yaliyopatikana kwa jasho la damu, tangu enzi zile za vita vya Majimaji, akina Mangi Meri, Mkwawa, Milambo nk.
Ubinafsi na uroho wa madaraka km wa Lissu et al, unawafanya wajiaminishe na kutaka kuwaaminisha wengine kuwa demokrasia ya kimagharibi ndio muarobaini wa matatizo ya nchi yetu, na kwa kudhani kuwa na uhuru tu kubwabwaja bila ya mipaka ndiko kunakoweza kutuleta shibe, maendeleo na kutuja mapeni mifukoni ni kujipumbaza kiakili.
Nchi inahitaji kufunga mkanda na kuachana na ukoloni mamboleo na kutengeneza mustakabali huru na wa dhati utakaotuwezesha SISI wenyewe kupanga njia na mbinu za kutuletea maendeleo yetu kwa kutumia vizuri fikra, utashi na raslimali zetu. Dr John Pombe Magufuli ameshaonyesha njia...Tumfuate.
Bonge moja la point. Ndiyo maan wakati mwingine namuonea huruma Anko Tundu Lisu. Kutetea maskini ni kazi sana. Maskini wengi ni wapumbavu sana.Kusema kweli tunajisumbua tu.. Tundu Lissu hawezi kuwa Rais sio kwasababu kura hazitatoshaa bali ni kwasababu ya corwadice ya Watanzania.
Mungu atupe uzima, October sio mbali tutarudi hapa..Mkuu hii ni level nyingine ya uhalisia sio ile ya mange ya kusadikika.
Siku Lissu anaingia nchini Jana yake tamko LA Polisi lingesababisha kila MTU kuingia mvunguni but what happened?
Issue ya Bomang'ombe kwa Sabaya ilikuwa mtego wa kuharibu zoezi zima la Lissu kutafuta wadhamini. Damu ingemwagika pale nyumbani kwa Mbowe picha ingesoma vibaya lakini Chadema waligundua hill na wakaruka kihunzi hicho.
Sisi ni waafrika na Afrika ni moja. Ile ni kauli ya kujenga umoja tuu, mbona kama tungekuwa tunaendekeza uadui hivyo huyu Mrundi angepata cheo chochote cha juu? Maana TL ile ni kauli huyu ni uhalisia!Ndio hatujawahi tangu Taifa hili liwe huru.
Tatizo siyo kuwekewa damu Tatizo Ni huyo yeye kuongea mbele za vyombo vya habari kuwa; "Mimi Ni mkenya mwenzenu kwasabab Nina damu nyingi ya wakenya" TL.
Je huyu ndo rais anaetufaa kuongoza nchi ya kizalendo Kama Tanzania?
Watu wanajipa matumaini ambayo hayapo kabisa..Bonge moja la point. Ndiyo maan wakati mwingine namuonea huruma Anko Tundu Lisu. Kutetea maskini ni kazi sana. Maskini wengi ni wapumbavu sana.
1. Lisu hana uadilifu - lilidhihirika katika sakata la kina kitila kinyume kabisa na anavyombagaza mh jpm1. Anaijua sheria ataongoza taifa kwa misingi ya haki
2. Hana tamaa ya mali, hatokimbilia kujenga mahekalu kwa na kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwao Mahambe, hawezi, hawezi hubadili msitu wa Mahambe kua hifadhi ya wanyama.
3. Ni muelewa mzuri wa masuala ya kimataifa, atasaidia kuimarisha diplomasia ya kimataifa
4. Hatorusu kuingia mikataba ya kinyonyaji kwa sababu ni mjuzi wa sheria
5. Hana rekodi ya ufisadi wala tuhuma zozote rushwa. Ni mwadilifu
6. Haturuhusu DPP kuchelewesha kesi mahakamani kusababisha mrundikano wa wafungwa
7. Hatoruhusu ubambikiaji wa kesi na uonevu unaofanywa na baadhi ya polisi
Serikali ya awamu ya awamu ya 6 licha ya kuzidi kujikita ktk kuyaendeleza mambo mazuri yaliyokwisha kuanza kutekelezwa kupitia kodi za wananchi, kwa namna ya pekee itunge sera rafiki zenye uwezo wa kuwakwamua kiuchumi wakulima maskini na hasa wengi wao waishio vijijini.
Awamu hii isije kutuletea tena miradi mingine mikubwa yenye kugharimu fedha nyingi kwa gharama ya kuwanyima haki makundi mengine ya watu mathalani wafanyakazi. Serikali iwe tayari kutoa majibu ya uhakika hata kama yatabeba ukweli mchungu, kuliko kutafuta visingizio vingi na porojo tupo zenye kubeba ahadi za uongo.View attachment 1540781
kweli siasa ni mbaya maana hata unayoyaandika yanaonyesha una hisia za kinjaa tu.wewe unajikuta heti huishi kwa Amani.
Kwa maisha gani uliyonayo yani wewe hata ukienda kulala polini ukiondoa kudhuliwa na wanyama wakali utabaki salama kabisa.
Mtu hujawahi hata kusikia mlio wa bunduki tangu uwepo hapa Tanzania ndo unakuwa wa kwanza kuleta unafiki wako hapa.
Siasa Ni Mbaya Sana .
Mtatatizo makubwa mara ngapi mbona tuna mtatizo makubwa tayari? Ccm must go!