Kwanini U-FM Jana walikata matangazo DW Wakati John Pambalu alipokuwa akizungumza?

KIKI CORAL

Senior Member
Joined
May 10, 2023
Posts
183
Reaction score
313
Jana Mchana DW SWAHILI katika Kipindi cha meza ya Duara waliwaalika wanasiasa watatu nchini Tanznaia akiwemo John Pambalu Mwenyekiti wa BAVICHA, Steven Wasira Kada wa CCM, na Abdul Nondo Mwenyekiti ngome ya vijana ACT.

Walikuwa wana mjadala kuhusu 4RS za Rais samia kama zinaishi ama zimejifia.

Wasira alianza kwa kufafanua vizuri sana maana ya hizo 4rs na kwanini na zinalenga nini n.k

Baadae John Pambalu akapewa nafasi naye ili atoe maoni yake U-FM wakakata matangazo wakaweka jingo zao za UFM tumekufikia, nikahamisha nikasikilzia Radio Tumaini ila usikivu haukuwa mzuri sana.

Alipoanza kuongea NONDO ufm wakarudisha matangazo tena, mtangazaji akamrudishia tena Pambalu afafanue hoja fulani hivi U-FM wakakata tena.

Baadae akapewa Wasira U-FM wakarudisha tena matangazo kama kawaida, Mwishoni John Pambalu akarudi ile afanye fact check kwa kile alichokuwa akizungumza wasira U-FM Wakakata tena matangazo yao.

U-FM ni kituo chenye watangazaji Nguli wenye uzoefu mkubwa sana kwenye tasnia ya habari na kinasimamiwa na nguli Baruani Muhuza ambaye ni kada wa CCM (2020 Aligombea ubunge Kigoma mjini kWa tiketi ya CCM kashindwa kura za maoni)

lakini nimeshangaa sana wao kupendelea habari za upande mmoja na hawataki kusikiliza upande waPili.

Je tuamini kuwa U-FM imeamua Kuungana na Radio Uhuru, TBC,CLOUDS NA WASAFI kuwa Chawa wa serikali? Je U-FM nao wamefika bei na kuamua kuegemea upande mmoja?

Weledi wao uko wapi licha ya kuwa na manguli kwenye tasnia?

Au kwa kuwa Mwenye UFM ni wa upande wapili wa muungano na wameamua kumuunga mkono Mzanzibar mwenzao?

kama manguli wale wamekuwa madalali wa CCM na serikali tasnia ya habri kwa sasa haina kitu tena inajifia.

Hata juzi kwenye Press ya CHADEMA vyombo vyote ukiachilia clouds,wasafi na hiyo ufm viliipa nafasi kubwa sana habari ya CHADEMA ila Azam tv na ufm walipa nafasi kidogo sana tena ni kama walifanya kuepeuka lawama maana waliweka kipande cha sekunde 30 tu kile alichozungumza mbowe kwenda kuwashtaki nyahoza na Awahi haji.

Kwa wale ambao hawakusikiliza au waliathiriwa na kukatishwa kwa matanagzo hayo na UFM nimekuwekea hapa link ya kusikiliza Matangazo ya Mchana: 17.08.2024 – DW – 17.08.2024

IFIKE MAHALI WATU WANAOKUMBATIA WATAWALA NA KUWABAGUA WENGINE KWA MISINGI YA ITIKADI ZA VYMA TUWAKATAE KWA VITENDO
 
Tz hakuna Waandishi wa Habari bali kuna WAHANDISI WA HABARI za kusifu na kuabudu watawala.
Nafikiri umeelewa sasa.
 
Chadema na hata wanachama na supporters wao wanashindwaje kufungua vituo vya habari kama wenzao ccm. Kwenye chaguzi hadi TBC inayoendeshwa na kodi za wananchi inageuzwa kuwa chombo cha habari cha ccm na Chadema walalamika kuhujumiwa tu badala ya kufungua vituo vyao vya habari.
 
Chadema na hata wanachama na supporters wao wanashindwaje kufungua vituo vya habari kama wenzao ccm. Kwenye chaguzi hadi TBC inayoendeshwa na kodi zq wananchi inageuzwa kuwa chombo cha habari cha ccm na Chadema walalamika kuhujumiwa tu badala ya kufungua vituo vyao vya habari.
Kumbuka: Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa milele hadi Mahakama ilipolitoa kwenye hicho 'kifungo' haramu.
 
Chadema na hata wanachama na supporters wao wanashindwaje kufungua vituo vya habari kama wenzao ccm. Kwenye chaguzi hadi TBC inayoendeshwa na kodi zq wananchi inageuzwa kuwa chombo cha habari cha ccm na Chadema walalamika kuhujumiwa tu badala ya kufungua vituo vyao vya habari.
Hivyo unasapoti TBC inayoendeshwa kwa kodi za wananchi iihujumu chadema ili CHADEMA wafungue ya kwao? Ila hoja yako hapo juu ni nzuri hata mimi nimewahi kushauri tatizo je hao maccm watawapa Leseni?
 
Mbowe anatuhujumu, tumemshauri waanzishe kituo huu mwaka wa ngapi-Kimya. Kama kina Kiba wanaweza kwa nini sisi tushindwe. Tena tungeanzisha likituo moja kali la vijana piga mziki mkubwa, baada ya hapo wanaitwa wenye mawazo kinzani kutema madini.
serikali hii hii iliyofungia mwanahalisi na tanzania daima siwangekuwa wanashinda kila siku kwenye korido za hiyo radio ku-control maudhui yao. TCRA wana sheria yao wanaweza hata kupiga simu na kukifungia kituo bila kukupa maelezo
 
Chadema na hata wanachama na supporters wao wanashindwaje kufungua vituo vya habari kama wenzao ccm. Kwenye chaguzi hadi TBC inayoendeshwa na kodi zq wananchi inageuzwa kuwa chombo cha habari cha ccm na Chadema walalamika kuhujumiwa tu badala ya kufungua vituo vyao vya habari.
Habari za kisiasa huwa na uzito, kuaminika, na kuthaminika zikitolewa na vyombo huru vya mawasiliano ya umma (independent media). Media za vyama vya siasa kazi yake ni kusambaza habari za chama, uhamasishaji, publicity na propaganda.

Ukitaka kujua mambo ya CCM husomi gazeti la Uhuru au kusikiliza Radio Uhuru, Channel 10 au hata TBC.
 
Mbowe anatuhujumu, tumemshauri waanzishe kituo huu mwaka wa ngapi-Kimya. Kama kina Kiba wanaweza kwa nini sisi tushindwe. Tena tungeanzisha likituo moja kali la vijana piga mziki mkubwa, baada ya hapo wanaitwa wenye mawazo kinzani kutema madini.
Mashetani wa CCM na serikali yao dhalim wataihujumu
 
Chadema na hata wanachama na supporters wao wanashindwaje kufungua vituo vya habari kama wenzao ccm. Kwenye chaguzi hadi TBC inayoendeshwa na kodi zq wananchi inageuzwa kuwa chombo cha habari cha ccm na Chadema walalamika kuhujumiwa tu badala ya kufungua vituo vyao vya habari.
Uhuru wa habari Tanzania ni kikwazo, chombo cha habari kikioekana kuwapa wapinzani airtime kwa uzani sawa na CCM ujue hawatapata matangazo kutoka serikalini hivyo lazima wajifanyie self censorship.

Vv
 
Redio zinabanwa na miongozo ya sheria, jana Pambalu alipoanza kuporomosha matusi ya nguoni, akitukana kila mtu kwa matusi mazifo, lazima matangazo yangekatwa. Hawa vijana wamefanya chama kimekuwa cha kihuni huni
 
Back
Top Bottom