Kwanini U-FM Jana walikata matangazo DW Wakati John Pambalu alipokuwa akizungumza?

Redio zinabanwa na miongozo ya sheria, jana Pambalu alipoanza kuporomosha matusi ya nguoni, akitukana kila mtu kwa matusi mazifo, lazima matangazo yangekatwa. Hawa vijana wamefanya chama kimekuwa cha kihuni huni
Hayo matusi ni gani mkuu maana mimi baada ya kukata nilikuwa ansikiliza U-FM na Tumaini Radio je hayo matusi ni yapi? hebu yataje au tuwekee sauti ya hayo matusi sikiliza hii clip kuanzia dakika ya kumi na kuendelea useme hayo matusi Matangazo ya Mchana: 17.08.2024 – DW – 17.08.2024
 
Jana Mchana DW SWAHILI katika Kipindi cha meza ya Duara waliwaalika wanasiasa watatu nchini Tanznaia akiwemo John Pambalu Mwenyekiti wa BAVICHA, Steven Wasira Kada wa CCM, na Abdul Nondo Mwenyekiti ngome ya vijana ACT.

Walikuwa wana mjadala kuhusu 4RS za Rais samia kama zinaishi ama zimejifia.

Wasira alianza kwa kufafanua vizuri sana maana ya hizo 4rs na kwanini na zinalenga nini n.k

Baadae John Pambalu akapewa nafasi naye ili atoe maoni yake U-FM wakakata matangazo wakaweka jingo zao za UFM tumekufikia, nikahamisha nikasikilzia Radio Tumaini ila usikivu haukuwa mzuri sana.

Alipoanza kuongea NONDO ufm wakarudisha matangazo tena, mtangazaji akamrudishia tena Pambalu afafanue hoja fulani hivi U-FM wakakata tena.

Baadae akapewa Wasira U-FM wakarudisha tena matangazo kama kawaida, Mwishoni John Pambalu akarudi ile afanye fact check kwa kile alichokuwa akizungumza wasira U-FM Wakakata tena matangazo yao.

U-FM ni kituo chenye watangazaji Nguli wenye uzoefu mkubwa sana kwenye tasnia ya habari na kinasimamiwa na nguli Baruani Muhuza ambaye ni kada wa CCM (2020 Aligombea ubunge Kigoma mjini kWa tiketi ya CCM kashindwa kura za maoni)

lakini nimeshangaa sana wao kupendelea habari za upande mmoja na hawataki kusikiliza upande waPili.

Je tuamini kuwa U-FM imeamua Kuungana na Radio Uhuru, TBC,CLOUDS NA WASAFI kuwa Chawa wa serikali? Je U-FM nao wamefika bei na kuamua kuegemea upande mmoja?

Weledi wao uko wapi licha ya kuwa na manguli kwenye tasnia?

Au kwa kuwa Mwenye UFM ni wa upande wapili wa muungano na wameamua kumuunga mkono Mzanzibar mwenzao?

kama manguli wale wamekuwa madalali wa CCM na serikali tasnia ya habri kwa sasa haina kitu tena inajifia.

Hata juzi kwenye Press ya CHADEMA vyombo vyote ukiachilia clouds,wasafi na hiyo ufm viliipa nafasi kubwa sana habari ya CHADEMA ila Azam tv na ufm walipa nafasi kidogo sana tena ni kama walifanya kuepeuka lawama maana waliweka kipande cha sekunde 30 tu kile alichozungumza mbowe kwenda kuwashtaki nyahoza na Awahi haji.

Kwa wale ambao hawakusikiliza au waliathiriwa na kukatishwa kwa matanagzo hayo na UFM nimekuwekea hapa link ya kusikiliza Matangazo ya Mchana: 17.08.2024 – DW – 17.08.2024

IFIKE MAHALI WATU WANAOKUMBATIA WATAWALA NA KUWABAGUA WENGINE KWA MISINGI YA ITIKADI ZA VYMA TUWAKATAE KWA VITENDO
Hivi chadema mnashindwa kuanzisha chombo cha habari?,hiyo Sacco's yenu ni hovyo sana,mtalalamika mpaka siku yesu atakaporudi
 
DW iache kushirikiana na U-FM, kuna yeyote mwenye mawasiliano ya DW ili tupeleke malalamiko yetu?!.

Tafadhalini yawekeni hapa. KICORA
 
Hivi chadema mnashindwa kuanzisha chombo cha habari?,hiyo Sacco's yenu ni hovyo sana,mtalalamika mpaka siku yesu atakaporudi
sioni kama ni jambo Rahisi wka serikali hii kuwapa hao chadema leseni ya kuanzisha radio
 
Hivi chadema mnashindwa kuanzisha chombo cha habari?,hiyo Sacco's yenu ni hovyo sana,mtalalamika mpaka siku yesu atakaporudi
Ingekuwakuanzisha radio nirahisi kama unavyofikiria leo wangekuwa tayari wanazo hata Kumi.
 
Redio zinabanwa na miongozo ya sheria, jana Pambalu alipoanza kuporomosha matusi ya nguoni, akitukana kila mtu kwa matusi mazifo, lazima matangazo yangekatwa. Hawa vijana wamefanya chama kimekuwa cha kihuni huni
Alimtukana nani? Hebu tupe hayo matusi aliyosema tukuamini. Na kama redio ilikuwa haisikiki umesikia wapi hayo matusi
 
Matusi mazito sana, nikipost hapa JF watanipiga ban, vijana hawana adabu kabisa
Nimekuwekea hiyo link nzima hapo haijaeditiwa tuambie hayo matusi aliyataoa wapi? maana hiyo link ina kipindi kizima
 
Alimtukana nani? Hebu tupe hayo matusi aliyosema tukuamini. Na kama redio ilikuwa haisikiki umesikia wapi hayo matusi
nimemuwekea link ya hicho kipindi kutoka kwenye tovuti ya DW atuambie hayo matusi yako wapi
 
Sio jana tu....siku moja katika kusoma maoni ya wasikilizaji kuhusu Lissu kukamatwa Mbeya,maoni yakaanza hivi..."LISSU AMEKAMATWA KWA VILE AMETANGAZA KUGOMBEA URAIS, WAMEONA MGOMBEA WAO (wa CCM) HANA MVUTO.."😂😂Ufm wakakata hapohapo na kuweka muziki!

Hawa jamaa wakisikia mtangazaji anasema...."LEO KATIKA MEZA YA DUARA TUTAKUWA NA....LISSU/MNYIKA/PAMBALU nk" tegemea tu KUKATWA kwa matangazo!
Baruhani Muhuza ananiangusha sana kwa hili💩
 
Sio jana tu....siku moja katika kusoma maoni ya wasikilizaji kuhisu Lissu kukamatwa Mbeya,maoni yakaanza hivi..."LISSU AMEKAMATWA KWA VILE AMETANGAZA KUGOMBEA URAIS, WAMEONA MGOMBEA WAO (wa CCM) HANA MVUTO.."😂😂Ufm wakakata hapohapo na kuweka muziki!

Hawa jamaa wakisikia mtangazaji anasema...."LEO KATIKA MEZA YA DUARA TUTAKUWA NA....LISSU/MNYIKA/PAMBALU nk" tegemea tu KUKATWA kwa matangazo!
Baruhani Muhuza ananiangusha sana kwa hili💩
Aisee mimi siwafuatiliaga sana ila hivi karibuni niliona usikivu wao ni mzuri sana nikaamua kuwa niwe nasikiliza DW kupitia wkao ila kwa haya basi niafadhali niwe nasikiliza live kupitia Tovuti ya DW SWAHIL.
 
Hazifai hizi raia!
 
Jana Mchana DW SWAHILI katika Kipindi cha meza ya Duara waliwaalika wanasiasa watatu nchini Tanznaia akiwemo John Pambalu Mwenyekiti wa BAVICHA, Steven Wasira Kada wa CCM, na Abdul Nondo Mwenyekiti ngome ya vijana ACT.

Walikuwa wana mjadala kuhusu 4RS za Rais samia kama zinaishi ama zimejifia.

Wasira alianza kwa kufafanua vizuri sana maana ya hizo 4rs na kwanini na zinalenga nini n.k

Baadae John Pambalu akapewa nafasi naye ili atoe maoni yake U-FM wakakata matangazo wakaweka jingo zao za UFM tumekufikia, nikahamisha nikasikilzia Radio Tumaini ila usikivu haukuwa mzuri sana.

Alipoanza kuongea NONDO ufm wakarudisha matangazo tena, mtangazaji akamrudishia tena Pambalu afafanue hoja fulani hivi U-FM wakakata tena.

Baadae akapewa Wasira U-FM wakarudisha tena matangazo kama kawaida, Mwishoni John Pambalu akarudi ile afanye fact check kwa kile alichokuwa akizungumza wasira U-FM Wakakata tena matangazo yao.

U-FM ni kituo chenye watangazaji Nguli wenye uzoefu mkubwa sana kwenye tasnia ya habari na kinasimamiwa na nguli Baruani Muhuza ambaye ni kada wa CCM (2020 Aligombea ubunge Kigoma mjini kWa tiketi ya CCM kashindwa kura za maoni)

lakini nimeshangaa sana wao kupendelea habari za upande mmoja na hawataki kusikiliza upande waPili.

Je tuamini kuwa U-FM imeamua Kuungana na Radio Uhuru, TBC,CLOUDS NA WASAFI kuwa Chawa wa serikali? Je U-FM nao wamefika bei na kuamua kuegemea upande mmoja?

Weledi wao uko wapi licha ya kuwa na manguli kwenye tasnia?

Au kwa kuwa Mwenye UFM ni wa upande wapili wa muungano na wameamua kumuunga mkono Mzanzibar mwenzao?

kama manguli wale wamekuwa madalali wa CCM na serikali tasnia ya habri kwa sasa haina kitu tena inajifia.

Hata juzi kwenye Press ya CHADEMA vyombo vyote ukiachilia clouds,wasafi na hiyo ufm viliipa nafasi kubwa sana habari ya CHADEMA ila Azam tv na ufm walipa nafasi kidogo sana tena ni kama walifanya kuepeuka lawama maana waliweka kipande cha sekunde 30 tu kile alichozungumza mbowe kwenda kuwashtaki nyahoza na Awahi haji.

Kwa wale ambao hawakusikiliza au waliathiriwa na kukatishwa kwa matanagzo hayo na UFM nimekuwekea hapa link ya kusikiliza Matangazo ya Mchana: 17.08.2024 – DW – 17.08.2024

IFIKE MAHALI WATU WANAOKUMBATIA WATAWALA NA KUWABAGUA WENGINE KWA MISINGI YA ITIKADI ZA VYMA TUWAKATAE KWA VITENDO
Hapana, kilichotokea ni kipazasauti na ukaaji wa Pambalu haukuwa sambamba, Pambalu alipokaa sawasawa sambamba na kipaza sauti aliendelea kuongea alipoachia na kuhitimisha akiwa ametumia muda mwingi kuliko wenzake.
 
Back
Top Bottom