Kwanini U-FM Jana walikata matangazo DW Wakati John Pambalu alipokuwa akizungumza?

Hapana, kilichotokea ni kipazasauti na ukaaji wa Pambalu haukuwa sambamba, Pambalu alipokaa sawasawa sambamba na kipaza sauti aliendelea kuongea alipoachia na kuhitimisha akiwa ametumia muda mwingi kuliko wenzake.
No, kuna muda simu ilikatika ya Pambalu ila U-FM walikuwa wameshamuondoa hewani muda mrefu. mimi nilikuwa nasikiliza ufm na tumain radio 96.5 zote kwa pamoja. ukitaka kujua kasikilize hiyo link niliyoweka kutoka DW. pambalu alipewa nafasi tatu kuongea na zote ufm walikata.
 
Redio zinabanwa na miongozo ya sheria, jana Pambalu alipoanza kuporomosha matusi ya nguoni, akitukana kila mtu kwa matusi mazifo, lazima matangazo yangekatwa. Hawa vijana wamefanya chama kimekuwa cha kihuni huni
Tusi gani alitukana?
 
Hatari sn
 
Ujinga wa aina hiyo ulikua unafanywa na RFA miaka ya nyuma.Walikipata walichokitaka.Na hao UFM waendelee hivyohivyo watavuna zawadi yao.
 
Redio zinabanwa na miongozo ya sheria, jana Pambalu alipoanza kuporomosha matusi ya nguoni, akitukana kila mtu kwa matusi mazifo, lazima matangazo yangekatwa. Hawa vijana wamefanya chama kimekuwa cha kihuni huni
Tuwe hapa hayo matusi tuyaone. Mi nilisikiliza hicho kipindi mwanzo mpaka mwisho.
 
Ninaposema alipoachia ni pale alipotakiwa akae sambamba na kipaza sauti ndipo walipomuondoa na kuendelea alipoachia, nakushauri thibitisha hilo kutoka kwa Pambalu.
 

Pole sana mkuu lakini hicho kitendo mbona ni kawaida kwa UFm sio mara moja au mbili.Huwa ikifika habari za Tz wakiwa wapo kikaangoni wao wanakata matangazo na sisi wasikilizaji tumeshazoea na pia tunawaelewa Kuwa wao ni chombo cha watawala sio wananchi.Mwisho hata tukisema hakuna mahali tutaenda kuwashtaki maana chombo ni cha kwao so ukiona hivyo badilisha frequency nenda radio station nyingine ili upate matangazo.
 
sawa mkuu
 
Ninaposema alipoachia ni pale alipotakiwa akae sambamba na kipaza sauti ndipo walipomuondoa na kuendelea alipoachia, nakushauri thibitisha hilo kutoka kwa Pambalu.
Mkuu mara ya kwanza ilikatika na wakati inakatika pia U-FM walikuwa wameshamtoa hewani, walimtoa hewani pale tu alipoanza kusema Mbowe alipewa kesi ya ugaidi. U-FM walimkata ila Tumain radio waliendelea nae.

Aliporudi hewani alimkuta Nondo anaongea na U-FM walimwacha nondo anaongea, Mtangazaji akasema naambiwa Pambalu amerudi tena akaanza kuongea U-FM wakamkatia tena wakaweka Jingo ya U-FM tumekufikia.

Tumain radio wakaendelea, alipomaliza kuongea wakarudi kwa wasira U-FM wakarudisha matangazo tena, Baaada ya wasira pambalu akaomba kufanya fact check kwa alichozungumza Wasira U-FM wakamkata tena hewan wakaweka Jingo zao ila Tumain Radio ikaendelea.

Mimi nilikuwa natumia Radio mbili kusikiliza baada ya kuambiwa na wadau kuwa U-FM wanakata matangazo wakiongea wapinzani, nikataka kupata Udhibitisho na kwlei ikawa Hivyo.
 
Fitna za msimu unaoonyesha uhovyo wetu na watu wake kupitia vyombo na watu kwa manufaa ya watu fulani fulani wenye kujipa ubora wasio nao.
 
Kwa U Fm sio mara ya kwanza. Sikuzote akianza kuongea mtu wa CHADEMA kupitia DW hawa U fm huwa wanakata matangazo.
 
Kwa U Fm sio mara ya kwanza. Sikuzote akianza kuongea mtu wa CHADEMA kupitia DW hawa U fm huwa wanakata matangazo.
safari bado ni ndefu sana kama media zitakuwa zinaegemea upande mmoja tena wa watawala dhalimu
 
Wapo biased, UFm, efm,clouds wote ni machawa wa ccm, wameshikwa pumbu na ccm, hawawezi kufurukuta,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…