Kwanini Ukristo unakataza kuoa wake wengi?

Kwanini Ukristo unakataza kuoa wake wengi?

Naangalia filamu hapa. Muislamu mmoja kashika bunduki, anamuelekezea padri anamwambia aseme "hakuna mungu pekee zaidi ya Allah". Padri kagoma, wakamuua na kwenye kundi hilo la waislamu wengine wanabaka.
Nani kakwambia Uislamu unaruhusu mambo hayo
Au tuseme una ushahidi gani kuwa mambo hayo yanaruhusiwa na Uislamu
 
Kama alishushiwa, kwanini huyo aliyemshushia hakumpa uwezo wa kujua kusoma na kuandika?
Wakati Mtume anashushiwa Qur’an alikuwa anasomewa na kuhifadhi kichwani hakukuwa na haja ya kuandika halafu yeye ndo alienda kuwasomea maswahaba zake ambao ndo waliiandika Qur’an kwenye ngozi,mifupa laini,majani ya mitende na sehemu nyingine
 
Nimekaa nikajuiliza kwanini hawa majiarani zetu(wakristo) hutumia nguvu kubwa saana mambo ya kuoa mke zaidi ya mmoja kama walivyo waislam wasukuma wamasai nk

But suala la ajabu wanaume kwa wanaume kuoana kanisa linabariki mara utasikia UK jamaa kaoa mbwa mara kuna mwanamke kao mwanamke mwenzie church

Usitukane just nimewaza kimaandishi
UKRISTO haujakataza kuoa mke zaidi ya mmoja,,,,,,,bali mtu huyo akiwa ASKOFU ni vyema akawa mtu wa mke mmoja.....mengine ni mapakeo na tafsiri pamoja na tamaduni za kizungu...
Wakristo wengi tuna mke zaidi ya mmoja toka enzi za mababu zetu...... waliwapokea wamisionari hali tayari wakiwa na mke zaidi ya mmoja....Hata baba yake Mwl.Nyerere alikuwa ni Mkristo lakini alikuwa na mke zaidi ya mmoja....Vivyo hivyo Machifu kadhaa akiwamo Mangi.....
Baba aliyemzaa babu yangu wake wanne
Babu yangu wake watatu
Baba yangu wake wawili
Mimi wake wawili rasmi na mmoja ni suria wa chobingo.
Mnaita nyumba ndogo
Au siyo VP Bwann
 
Unajua Uislamu ulianzishwa Vatican? Mafundisho ya Papa na ya uislamu hayana tofauti wote lengo lao ni kuuchafua ukristo. Unajua kabisa Biblia inasema watu waoe mke mmoja halafu wewe na dini yako unalazimisha. Ndiyo mambo ya papa
Mtu ambaye hajui kusoma na kuandika anawaambia Quran imeshushwa na nyinyi mkaamini. Kama Quran ilishushwa ilikuaje Allah asimpe uwezo wa Mohamad ajue kusoma na kuandika?
View attachment 3247968
Daaadeki sio hapa bao moja tu dakika tutatu.......miaka mil.28 kwa bao....
Balaa kubwa,,,,,
 
Embu weka Aya zinazoruhusu mambo hayo hapa. Vinginevyo una tatizo kichwani

Mkuu kasome:

1. Kumbukumbu la Torati 21:15

2. 1 Timotheo 3:2, 12

3. Titusi 1:6

ZINGATIA:

Kwenye agano la kale wazee wote wa imani walikuwa na wake zaidi ya mmoja.

Pili, kwenye agano jipya viongozi ndio wamehimizwa kuwa na mke mmoja sio muumini wa kawaida.
 
Ndivyo Mungu alivyoamuru,Mme Mmoja na Mke Mmoja,(Mwanzo2:21-24) na (Mathayo19:4-7)
(1Wakorintho7:1-2)- Kila mtu awe na Mkewe.
Biblia inakataza ndoa ya Mwanaume kwa Mwanaume,hayo ni machukizo mbele za Mungu,(Walawi20:13)-Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Ulawiti na Ufiraji unakatazwa na Neno la Mungu,huo ni udhalimu,(1Wakorintho6:9-10)- Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
Kanisa la Mungu haliwezi kubariki Ndoa za Jinsia Mmoja.
UCHAFU UNAOFANYWA NA WAZUNGU SIYO AGIZO LA KANISA LA MUNGU ULIMWENGUNI.

Mkuu kwanza umeanza hoja yako na maneno yasiyo ya kweli.

Maana hakuna kumbukumbu yoyote inayoonyesha kuwa Mungu alishusha biblia.

Biblia ni kumbukumbu ya hadithi za mila, imani, taratibu, desturi na tamaduni za wayahudi.

Na suala la mke mmoja lingekuwa na umuhimu huo wakati huo lingekuwa moja ya amri kuu katika biblia hiyo.

Mkuu usichanganye umagharibi na ukristo!
 
Nimekaa nikajuiliza kwanini hawa majiarani zetu(wakristo) hutumia nguvu kubwa saana mambo ya kuoa mke zaidi ya mmoja kama walivyo waislam wasukuma wamasai nk

But suala la ajabu wanaume kwa wanaume kuoana kanisa linabariki mara utasikia UK jamaa kaoa mbwa mara kuna mwanamke kao mwanamke mwenzie church

Usitukane just nimewaza kimaandishi
KAMA ULIVYOKAA KUJIULIZA HILO NINA IMANI UNAWEZA KUKAA NA KUJIULIZA MENGI ZAIDI AMBAYO NI CHANGAMOTO KWETU SISI WAISLAMU NA NAMNA GANI YA KUZITATUA.

Tulishaambiwa ndani ya Quran sisi tuna dini yetu na wao wana dini zao. Haina haja ya kupekua mabaya ndani yao, badala yake tunaweza kuchukua mazuri na kutumia kama mfano kuona wapi sisi tunakwama.

Swala la mke zaidi ya mmoja sio sifa au kipaumbele alichopewa mwanaume. Bali ni jukumu ambalo kesho tutakuja kuulizwa. Sisi wanaume tumelazimishwa kuwafanyia wake zetu mambo matano regardless wana kipato au hawana.
1. kumlisha
2. kumvisha
3. malazi
4. kumtibia
5. mapambo

Jiulize waislamu wangapi tunawalazimisha wake zetu ( wanaofanya kazi au biashara) kuchangia kodi, au kujitibia au kuchangia ratio ya chakula nyumbani? we unaona hili lipo sawa wakati sheria ishatutaka sisi wanaume ndio tuprovide hivyo vitu kwao?

Usia wangu kama muislamu mwenzako
"TUTIZAME MABAYA NDANI YETU (ili tuyarekebishe) na TUTIZAME MAZURI YA WENGINE.

Assalaam aleykum
 
KAMA ULIVYOKAA KUJIULIZA HILO NINA IMANI UNAWEZA KUKAA NA KUJIULIZA MENGI ZAIDI AMBAYO NI CHANGAMOTO KWETU SISI WAISLAMU NA NAMNA GANI YA KUZITATUA.

Tulishaambiwa ndani ya Quran sisi tuna dini yetu na wao wana dini zao. Haina haja ya kupekua mabaya ndani yao, badala yake tunaweza kuchukua mazuri na kutumia kama mfano kuona wapi sisi tunakwama.

Swala la mke zaidi ya mmoja sio sifa au kipaumbele alichopewa mwanaume. Bali ni jukumu ambalo kesho tutakuja kuulizwa. Sisi wanaume tumelazimishwa kuwafanyia wake zetu mambo matano regardless wana kipato au hawana.
1. kumlisha
2. kumvisha
3. malazi
4. kumtibia
5. mapambo

Jiulize waislamu wangapi tunawalazimisha wake zetu ( wanaofanya kazi au biashara) kuchangia kodi, au kujitibia au kuchangia ratio ya chakula nyumbani? we unaona hili lipo sawa wakati sheria ishatutaka sisi wanaume ndio tuprovide hivyo vitu kwao?

Usia wangu kama muislamu mwenzako
"TUTIZAME MABAYA NDANI YETU (ili tuyarekebishe) na TUTIZAME MAZURI YA WENGINE.

Assalaam aleykum
Hili makala ni kuwakumbusha maana kila kukicha kuchafua uslam wakati wanamambo yao kujadili na sio kuwasingizia ni kuwakumbusha mambo yao yanavyozidi kuharibia
 
Je, Mungu Aliruhusu Lakini Hakuhimiza Mitala?

Mitala ni jambo la kipekee kwa sababu Mungu hakulianzisha, lakini katika hali nyingi aliloruhusu, hakulilaani moja kwa moja. Hii hapa ni uchambuzi wake:

1. Mitala Haikuwa Mpango wa Awali wa Mungu

Katika Mwanzo 2:24, Mungu alianzisha ndoa kama muungano kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja:
“Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mke wake, nao watakuwa mwili mmoja.”

Hii inaonyesha kuwa ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ilikuwa mpango wa asili wa Mungu.


2. Mitala Ilianzishwa na Wanadamu

Mtu wa kwanza kurekodiwa kuwa na wake wawili ni Lameki, mzao wa Kaini (Mwanzo 4:19). Hili halikuonyeshwa katika mwanga mzuri.


3. Mungu Aliruhusu Mitala kwa Watu Mashuhuri

Abrahamu: Alimwoa Hagari kama mke wa pili kwa ushawishi wa Sara (Mwanzo 16:1-3). Ingawa hali hii ilisababisha migogoro, Mungu bado alimbariki Ishmaeli, mwana wa Hagari.

Yakobo: Alimwoa Lea na Raheli kwa hila ya Labani, kisha akaongeza wake wawili wa mitala (Mwanzo 29:21-30, 30:3-9). Watoto wake walikuwa kabila kumi na mbili za Israeli.

Daudi: Alikuwa na wake wengi (1 Samweli 25:42-43; 2 Samweli 3:2-5), lakini bado Mungu alimwita “mtu aliyeupendeza moyo wangu” (1 Samweli 13:14).

Solomoni: Alikuwa na wake 700 na masuria 300 (1 Wafalme 11:3), lakini alianguka kwa sababu wake wake wa kigeni walimwelekeza kwenye ibada ya sanamu, jambo ambalo Mungu alikemea.


4. Mungu Alitoa Sheria Kuhusu Mitala Lakini Hakuilaani Moja kwa Moja

Kumbukumbu la Torati 21:15-17: Mungu alitoa sheria kuhusu urithi katika familia zenye wake wengi ili kuhakikisha haki kwa watoto wa wake waliopendelewa na wale wasiopewa kipaumbele.

Kumbukumbu la Torati 17:17: Mungu aliwaonya wafalme wasiwe na wake wengi kwa sababu wangewapotosha mioyo yao kutoka kwake.


5. Agano Jipya na Mpango Halisi wa Mungu

Kufikia wakati wa Yesu, ndoa ya wake wengi ilikuwa kawaida kati ya Wayahudi. Yesu alithibitisha kuwa mpango wa Mungu tangu mwanzo ulikuwa ndoa ya mume mmoja na mke mmoja (Mathayo 19:4-6).

Kiwango cha Uongozi wa Kanisa: Paulo alisema kwamba askofu au shemasi anapaswa kuwa “mume wa mke mmoja” (1 Timotheo 3:2, 12; Tito 1:6), jambo linaloonyesha kuwa ndoa ya wake wengi haikupendelewa kwa Wakristo.


Hitimisho

Mungu hakulianzisha mitala, na mara nyingi lilisababisha migogoro katika familia (mfano, Sara na Hagari, Lea na Raheli, na hata anguko la Solomoni). Hata hivyo, aliliruhusu na akaendelea kufanya kazi kupitia ndoa za wake wengi bila kulaani moja kwa moja desturi hiyo—isipokuwa ilipopelekea dhambi. Mwelekeo wa Biblia, hasa katika Agano Jipya, unaonyesha kuwa ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ndiyo kiwango ambacho Mungu alikusudia tangu mwanzo.
 
Shida hamsomi Biblia. Mnakuwa kama mtu ambaye hajui kusoma na kuandika halafu anapewa kitabu anawaambia kimeshushwa na nyinyi mnaamini.
Kwahyo hiko kfungu cha kuoa mke mmoja tunatekeleza visivyo ?
 
Back
Top Bottom