sijawai kutaja dini hata maramoja kwenye mijadala hii wajinga wanjinga ndo mnaingiza dini huku na mambo ya moto au umeona hii mada ina mlengo wa kidini
ila nashukuru kwasababu wewe umesema haujui Mungu yupo au hayupo
inerest yangu ni watu wanaosema kwa uhakika Mungu hayupo. upande wako sina shida na wewe kabisa
Kwani wewe una uhakika yupo?sijawai kutaja dini hata maramoja kwenye mijadala hii wajinga wanjinga ndo mnaingiza dini huku na mambo ya moto au umeona hii mada ina mlengo wa kidini
ila nashukuru kwasababu wewe umesema haujui Mungu yupo au hayupo
inerest yangu ni watu wanaosema kwa uhakika Mungu hayupo. upande wako sina shida na wewe kabisa
Kwajibu linalotaka uthibitisho wa Sayansi nitasema sina uhakika kwasababu sayansi haina uwezo huo wa kuthibitisha. na atheist wengi wanataka uthibitisho wa sayasiKwani wewe una uhakika yupo?
We jamaa unashangaza sana. Unajiona unaelewa kiundani masuala ya ulimwengu kumbe hakuna kitu unajua.Kwajibu linalotaka uthibitisho wa Sayansi nitasema sina uhakika kwasababu sayansi haina uwezo huo wa kuthibitisha. na atheist wengi wanataka uthibitisho wa sayasi
sayansi ni chombo muhimu cha kuthibitisha lakini kwenye Swala la kuthibitisha Mungu yupo ni kama unataka kutumia thermometer kupimia uzito
Kwa nini unalazimisha hiyo Connection itoke sehemu fulani?unaongea ujinga hata hujui mada inasemaje
swala si nani anafuata kanuni ya nani swala ni hiyo
Connection inatoka wapi kama akili na ulimwengu vilitokea kwa bahati tena kwa muda tofauti ?
nitajifunika magome ya miti, nitakula matunda nitawasha moto kwa ulindi na ulimbombo.We jamaa unashangaza sana. Unajiona unaelewa kiundani masuala ya ulimwengu kumbe hakuna kitu unajua.
Labda nikuulize swali dogo sana. Hivi ikitokea duniani umebaki wewe hapo peke yako, ni kipi utaweza kukiunda chenye uwezo wa kukufanya usurvive? Namaanisha itokee upo kwenye dunia ambayo kila kitu unachokitumia kimetoweka ukajikuta upo uchi kama mnyama na vyote unavyotumia leo hii vikawa havipo.
Kuna chochote unaweza kuunda kutumia hizo hesabu unazozungumzia?
Au na wewe unajiona unatengeneza ndege kwakua ni binadamu kama walivyo wanaotengeneza hizo ndege?
Unajua kwanini walikuletea Mungu?
Hapa umemaliza kila kitu mkuu..
Wengine hatutaki kuamini tu. Potelea pote. Tumeshaona kuamini/kutokuamini hakumbadilishii mtu chochote.
Haya ni maswali mazuri kwanza nianze kwa kusema Infropreneur wewe ni moja ya atheist ninae muheshimu zaidi hapa jukwaani kutokana na uelewa wako mkubwa kwa kile unachokisimamia na nimefurahi kupata fursa ya kufanya mjadala na wewe.Kwa nini unalazimisha hiyo Connection itoke sehemu fulani?
Kwa nini unadhani ulimwengu ulitokea?
Kwa nini hudhani ulimwengu umekuwepo milele bila kutokea?
Kama ni lazima ulimwengu uwe ulitokea, huko ulipotokea, na kwenyewe kulitoka wapi?
ww nae n kiazi tu ulimwengu ufate hesabu za kibinadamu?? hivi ulimwengu na hesabu za kibinadamu nani alimkuta mwenzake??Physicist mkubwa Eugene Wigner aliandika makala maarufu sana aliita
"The Unreasonable Effectiveness of Mathematics in the Natural Sciences."
Alisema waziwazi na maneno yake ni haya kwa muhtasari:
"Ni ajabu isiyoeleweka kwa nini hesabu zilizoundwa bila kujali ulimwengu wa kimwili zinafanya kazi vizuri sana kueleza ulimwengu huo. Hakuna maelezo ya kawaida ya hili."
huyu ni mwanasayansi mkubwa anayeheshimika kwa mchango wake kwenye physics.
Swali kama ulimwengu ni bahati tu kwa nini unafuata hesabu za akili ya binadamu kwa usahihi huu?
Hesabu ni kitu kinachoishi akilini. Hakuna mtu aliyeona namba 7 ikitembelea barabarani. Hakuna aliyegusa equation kwa mkono.
Lakini ulimwengu wa kimwili mwamba, maji, nyota unafuata hesabu hizo kwa usahihi wa kushangaza.
hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuna uhusiano wa ajabu kati ya ulimwengu wa akili na ulimwengu wa kimwili.
Uhusiano huo unatoka wapi kama akili na ulimwengu vilitokea kwa bahati tena kwa muda tofauti
Mwaka 1846 mwanasayansi Urbain Le Verrier alitumia hesabu za mvutano (gravity) kuonyesha kwamba kuna sayari isiyoonekana inayovuruga mzunguko wa Uranus. kwa kutumia hesabu pekeyake akaonyesha kabisa ipo wapi angani.
Baadaye, mwanasayansi Johann Galle akaangalia kwa darubini sehemu hiyo na kweli sayari hiyo ikapatikana karibu kabisa na hapo ilipoonyeshwa. Sayari hiyo mpya ikaitwa Neptune
Newton alitoa theory yake ya gravity miaka ya 1687. Mwaka 1969 hesabu zake zikatumika kuwapeleka binadamu kwenye mwezi, na mpaka sasa hesabu zake zinatumika kurusha roketi angani
theory of relativity ya Einstein iliandikwa mwaka 1905 na 1915. Sasa hivi miaka 100 baadae hesabu zake ndo msingi wa GPS
miaka 1000 kabla ya satelite, Al-battani alitumia hesabu ili kujua dunia inatumia siku gapi kuzunguka Jua. Al-Battani akaja na jibu akasema:
Mwaka una siku 365, Masaa 5, Dakika 46 na sekunde24
nakuwekea video fupi kutoka kwenye documentary fulani ili uone kwa ufupi alivyofanya na kupata jibu hilo
View attachment 3573435
Leo kwa kuchunguza kwa Satelite tunaona dunia inatumia Siku 365, Masaa 5, Dakika 48 na sekunde 47
( Al-battani alikua nyuma kwa dakika 2 tu )
Paul dirac aliandika equation yake na hesabu zake zikamfanya agundue ulimwenguni kuna anti-particle. Wkati huo ilikua haiwezi kuthibitishwa kwa namna yoyote kwasababu tecnolojia ilikua chini. leo baada ya miaka 100 sasa tuna tecnolojia ya kisasa anti-particle tunaiona kila siku maabara.
Galileo Galilei alisema
“Mathematics is the language in which God has written the universe.”
NASA walikuja kuthibitisha hili walipokua wakituma golden disc wakajiuliza swali
je tukikutana na aliens leo tutatumia lugha gani kuwasiliana nao ?
wakasema ni hesabu, obviously kiumbe yeyote mwenye akili mahali popote ulimwenguni anajua 1 + 1 ni 2
Kuna uwezekano mbili tu wa kueleza hili:
Uwezekano wa kwanza ni bahati ya kushangaza sana kwamba akili iliyotokana na evolution inaweza kuelewa ulimwengu wa quantum, cosmos, na hesabu za abstract bahati ambayo haina maelezo.
Uwezekano wa pili akili na ulimwengu vina chanzo kimoja. Vimeundwa na kitu kimoja. Kwa hiyo vinafanana kama vitu viwili vilivyotengenezwa na fundi mmoja vinavyofanana.
Wigner mwenyewe alisema uwezekano wa kwanza hauridhishi akili.
Kama ulimwengu ni bahati tu akili ni bahati tu hesabu ni bahati tu basi bahati hiyo imefanya kitu ambacho hakuna bahati nyingine inaweza kufanya
Imeunda akili inayoweza kuuelewa ulimwengu ambao haikuhitajika kuuelewa.
Hilo linahitaji maelezo. Na maelezo rahisi zaidi ya kimantiki ni moja kulikuwa na akili kubwa kabla ambayo iliunda akili ndogo na ulimwengu na kuzifanya zifanane.
Stephen Hawkins Ambae ni Mwanasayansi maarufu ambae pia alikua Atheist, kwenye moja ya maandiko yake alijiuliza hivi:
"What is it that breathes fire into the equations and makes a universe for them to describe?"
swala si nani alimfuata mwenzake, ninauhakika umesoma tu kichwa cha habari ukaja kuandika ujinga wako hapa bila kuelewa unajibu nini na umeulizwa nini.ww nae n kiazi tu ulimwengu ufate hesabu za kibinadamu?? hivi ulimwengu na hesabu za kibinadamu nani alimkuta mwenzake??
Kama mchakato ulianza mahali fulani, Je mahali huko mchakato ulipoanzia, na kwenyewe kulianza vipi?Haya ni maswali mazuri kwanza nianze kwa kusema Infropreneur wewe ni moja ya atheist ninae muheshimu zaidi hapa jukwaani kutokana na uelewa wako mkubwa kwa kile unachokisimamia na nimefurahi kupata fursa ya kufanya mjadala na wewe.
Umeniuliza maswali na bila kujua kila swali uliloulizia linakuuliza na wewe pia.
Hebu tuende pamoja.
Mimi sijalazimisha connection ulimwengu wenyewe unailazimisha.
Hesabu zilizoundwa akilini zinafanya kazi ulimwengu wa kimwili hii si madai yangu ni ukweli unaoonekana. Wanasayasi nilionwa quote hawakusema hivi kwa sababu ya dini walisema kwa sababu waliona ukweli huo na kushindwa kuuelezea.
Pia umeniambia kwanini nisidhani kwamba Ulimwengu umekwepo milele hili swali zuri na kali sana, lengo la mjadala huu ni kupata maswali makali sana nami kuwachapa maswali makali sana ili mjadala huu ubaki kama reference kwa watu watakaokua wakisoma
swali lako hilo lina jibu la kisayansi na la kimantiki.
jibu la kisayansi: Second Law of Thermodynamics inasema ulimwengu unaelekea entropy disorder inayoongezeka daima. Kama ulimwengu ungekuwa wa milele kwa wakati uliopita tungekuwa tayari katika heat death hakuna nishati, hakuna mwendo, hakuna kitu. lakini tuko hapa nyota zinaungua nishati ipo hii inamaanisha mchakato ulianza mahali fulani.
jibua la kimantiki: ulimwengu wa milele una tatizo kubwa la kimantiki linaloitwa 'infinite regress of causation' ambalo tulilijadili awali kwenye mada fulani tukajubaliana hauwezi kufika leo kama ulikuja kutoka infinity ya zamani.
Je ili kitu kiwe cha milele ni lazima kiwe na mchafuko wa milele?
Lakini muhimu zaidi hata kama ulimwengu ni wa milele swali langu bado lipo palepale?
Kwa nini ulimwengu wa milele una kanuni badala ya mchafuko wa milele ?
Umesema infinite regress ni tatizo la jibu langu.Kama mchakato ulianza mahali fulani, Je mahali huko mchakato ulipoanzia, na kwenyewe kulianza vipi?
Huoni kwamba ukiweka mahali vinapoanzia vitu, Hata mahali huko na kwenyewe kutahitaji kuanzia mahali pengine?
Hivyo utatengeneza msururu mrefu wa mahali kwingi vinapoanzia vitu bila kukoma.
Infinite Regress.
Je ili kitu kiwe cha milele ni lazima kiwe na mchafuko wa milele?
Je kitu hakiwezi kuwa cha milele na kanuni zake?
Mkuu , tutajadili badae kidogo na changamsha kichwa na mvinyo hapa
nami pia muda huu tayari kichwa kimechangamka sana kwa kvant ndo maana nikakumbuka sijapata wasaha wa jujadiliana na wewe. ila mvinyo unaumiza kichwa bora kvant na konyagi au biaMkuu , tutajadili badae kidogo na changamsha kichwa na mvinyo hapa
Natumia ,cognac ( hennessy) wala sio mvinyo bwashee, pombe kali labda keshonami pia muda huu tayari kichwa kimechangamka sana kwa kvant ndo maana nikakumbuka sijapata wasaha wa jujadiliana na wewe. ila mvinyo unaumiza kichwa bora kvant na konyagi au bia
sawa mkuu pamoja sana.Natumia ,cognac ( hennessy) wala sio mvinyo bwashee, pombe kali labda kesho
Wewe ni mzigo mzito sana. Unajiona mjuaji lakini hujui kitu. Zaidi ya kukalili huna la kwako.nitajifunika magome ya miti, nitakula matunda nitawasha moto kwa ulindi na ulimbombo.
we jamaa unaabisha Atheist wenzako kuuliza maswali ya ki pimbi namna hii na maswali ya kipimbi inabidi yajibiwe kipimbi. unahitaji kwanza kubadilishwa mentality yako ya uelewa wa dunia kiujumla eti Mungu tuliletewa