Kwanini unajificha na kuchungulia kwa manati unapotaka kuonana na Rafiki ulimpata mitandaoni?

Kwanini unajificha na kuchungulia kwa manati unapotaka kuonana na Rafiki ulimpata mitandaoni?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Mathalani,
Umepata Rafiki au Mchumba kwenye miongoni mwa mitandao ya kijamii, kwa mfano ulipokea simu ya aliekosea namba au ulipiga simu kwa kukosea namba akapokea asie husika, then mpokea simu ama wewe mpiga simu kimakosa mkatamani mjuane zaidi na baada ya hapo mkawa Marafiki, tena huenda ni wa kimapenzi.

sasa kimbembe huwa ni siku ya kukutana na kuonana uso kwa macho...

ni kwanini watu huviziana kuonana physically katika eneo walilo kukubaliana kukutana bila kujiamini? au mitandao haiaminiki?

Mtu anamueleza kabisa mwenzie kwamba ameshafika eneo husika, wewe upo upande gani basi,?

Utaskia Jamaa aliejificha, aahaa, umeshafika kumbe, ndio wewe ulievaa nguo nyekundu na suruali ya njano hapo karibu na kibanda cha tigo pesa?

Geuka nyuma utaniona hapa kwenye badaboda walipo, nimevaa cape ya pink, usitoke nakuja hapo hapo ulipo dah.

Kumbe mtu kaambiwa ageuke ili jamaa asiejiamini a learn physical and facial language yake ilivyo dah, na huenda kuna uwezekano wa kupotea hewani, ikiwa atamsogelea kwa karibu zaid na kubaini yaliyomo kumbe hayamo dah,!

Nyie haya mahusiano na mitandao ya kijamii ni balaa 🐒

Umewahi kupitia songombingo hii ya kabokamchizi kwenye sehemu mahusiano wako wa kimapenzi?🐒
 
1724049529322.jpg
 
Sijawahi tafuta GF online.. Kuna mwanangu ilishamkuta hii... Kwenye Picha mtoto Mrefu kinoma . Kuja kukutana nae sasa.. Kafupi akooo 😂

Oyaa Msiamini urefu wa kwenye picha
😄😄
katoto kalijipiga filter za kutosha hadi kakarefuka,

ila kalipokutana na jamaa filed ikawa kama konda anamvusha mtoto nursery barabara dah 🐒
 
Jamaa ilibidi Aigize kama mpita njia..

Ni kama alipishana na Mtungi wa Gas unaotembea... 😄
na akaona kumblock haitoshi akaamua kuzima na simu kabisa, huku akitafakari maajabu na muujiza alokutana nao ukilinganisha na matarajio yake, dah 🐒

hii mitandaoni saa zingine basi tu aise ...
 
Kumbe watu wa Lumumba Fc ndio tabia yenu.

Shuda inakuja unataka kukutana na mtu na ushajenga taswira zako kichwani, tayari unataka kumla kabla ya kumuona...

Kwani mkionana kama marafiki tu kuna shida gani, kama kuna mengine yatajitokeza baadae huko.
 
na akaona kumblock haitoshi akaamua kuzima na simu kabisa, huku akitafakari maajabu na muujiza alokutana nao ukilinganisha na matarajio yake, dah 🐒

hii mitandaoni saa zingine basi tu aise ...
Kwasasa jamaa ndio binadamu pekee duniani asieamini chochote kwenye Mitandao..

Ukiachana na kumblock mitandaoni, Jamaa lilienda mpaka Posta, Likablock hadi Sanduku la Posta la Yule mtoto 😄
 
Kumbe watu wa Lumumba Fc ndio tabia yenu.

Shuda inakuja unataka kukutana na mtu na ushajenga taswira zako kichwani, tayari unataka kumla kabla ya kumuona...

Kwani mkionana kama marafiki tu kuna shida gani, kama kuna mengine yatajitokeza baadae huko.
gen z hawanaga subra hizo gentleman...

gen z wako chonjo sana na matumizi ya muda,

hawapendeleagi kuprolong mambo kwa muda mrefu. hiyo hawapendi kabisa.

wao ni mnakutana leo, mnamalizana baadae, na ikishindikana leo basi kesho mapema sana bila kuchelewa, mambo yanakamilika,

na hapo sasa mbivu na mbichi ndipo hujulikana 🐒
 
Back
Top Bottom