Kwanini utawala wa Nyerere ulikumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na utawala wa Mwinyi, Mkapa na wengine?

Kwanini utawala wa Nyerere ulikumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na utawala wa Mwinyi, Mkapa na wengine?

Aliingia kwenye siasa za kijamaa bila kuwa tayari kulipa gharama kubwa kuzifanya zifanye kazi na kutekelezeka kama ilivyokuwa China chini ya Mao ambaye aliwatoa kafara Wachina million 20 ili kuifanya China ipige maendeleo chini ya Ujamaa.
 
Zamani wananchi walikuwa na skili sana kulingana na vyakula walivotumia na waalimu waliowafundisha ukilinganisha na sasa , hata kija wa university hata kiongea hoja hajui.
 
Mnapomzodoa JKN, msisahau kwamba alikuwa akisafiri kwa baiskeli ya kuazima ili kuwahamasisha vijana wajiunge na TANU ili kuandaa harakati za kuikomboa nchi kutoka kwa Mzungu.

Badala ya kumsingizia uongo, jiulize wewe unalifanyia nini taifa? Linganisha umri wako sasa na ule wa JKN wakati huo, unaona uko sawa akilini kweli?

Eti Mwalimu alishindwa, Mwalimu alifeli, Mwalimu alikurupuka! Emu tokeni kule!
 
Wanafunzi wa Mihamed Said hawa, wamelishwa ujinga hadi wameshiba!!
Eti Mwalimu aling'atuka kwa kuogopa kupinduliwa!

Nchi hii kuna watu wamesambaza upumbavu kwa misingi fulani hivi ili watu fulani waendelee kulala na majizi kuanzia kina Mwinyi yaendelee kuneemeka!
 
jiwe angavu njoo utie neno huku.
JKN alipata kisuko suko mingi katika serikali yake kwanza ni sera yake ya ujamaa ambayo ilifeli vibaya dhidi ya sera za kibepari ukizingatia nchi ndio kwanza inaanza kusimama...

alipata upinzani mkubwa sana hasa ndani ya nchi mana wengi walijawa uchu wa madaraka na kuzionaa sera zake za kijamaa ni sera kandaminzi na za kimasikini mna wafanyabiashara wakubwa walinyangangwa mali zao nyingi zilitaifishwa na viongozi wa chama naserikari kuwekewa vizuizi vingi katika suala la umiliki wa mali kupitia azimio la arusha..

Vita vya uganda navyo viliangusha sana uchumi wa nchi...na kusababisha hali ngumu sana ya kiuchumi.

Ila he was and always will remain the best president mpaka sasa katika nchi hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mnapomzodoa JKN, msisahau kwamba alikuwa akisafiri kwa baiskeli ya kuazima ili kuwahamasisha vijana wajiunge na TANU ili kuandaa harakati za kuikomboa nchi kutoka kwa Mzungu.

Badala ya kumsingizia uongo, jiulize wewe unalifanyia nini taifa? Linganisha umri wako sasa na ule wa JKN wakati huo, unaona uko sawa akilini kweli?

Eti Mwalimu alishindwa, Mwalimu alifeli, Mwalimu alikurupuka! Emu tokeni kule!
Hizi ni mburula zilizolishwa ujinga makusudi hadi zmepofuka!

Awamu zilizofuatia baada ya Mwalimu zote zime/zilijaa marushwa makubwa...sasa yeye kwa ujinga wake anaona ndio maendeleo
 
Kawaulize makaburu na wareno popote walipo habari za "Nyerere kusema maneno tu" kama watakubaliana na wewe.
Nyinyi watu wengine vichwa ni kama mmejaza takataka tu!

"Alikuwa hapendi ukosoaji", wa kipumbavu? Hukusikia/kuona mijadala ya mambo mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika ndani ya chama katika ngazi zote toka juu hadi shinani?
Weka ushahidi wa ukosoaji unaousema hakuupenda tuone kama ulikuwa ni wa kijinga.

"Kujenga utaifa", hata kama lingekuwa hilo tu, wewe huoni kwamba ni jambo muhimu, pengine kushinda mengine yote? Lakini si hivyo tu, leo unakuja hapa unasahau baba yako alipata elimu na mengi mengine ambayo asingeyapata chini ya ukoloni; halafu leo unakuja hapa na kujifanya wewe mjuaji.
Hata kama ungekuwa mjuaji, bado ungekuwa mjuaji wa kipumbavu kama hujui chimbuko la ujuaji wako huo lilitokana na nini.

Lakini najua napoteza muda wangu tu hapa na "skunk", asiyejua lolote maishani mwake.
Huyu sunk msamehe tu ndio kwanza ana siku sio nyingi tangu atoke mirembe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na wewe uliwahi kuvaa viraka na kuimba zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti? 😂😂

Naona Babu umetokwa povu sio la Nchi hii.
Hata ningevaa viraka, leo hii watu kama wewe huna uwezo wa kufikia nilipofikia mimi niliyevaa viraka!

Hopeless kabisa.
Hii inaonyesha katika mabandiko yako mengi ya kipuuzi unayoweka humu jukwaani.
 
JKN alipata kisuko suko mingi katika serikali yake kwanza ni sera yake ya ujamaa ambayo ilifeli vibaya dhidi ya sera za kibepari ukizingatia nchi ndio kwanza inaanza kusimama...

alipata upinzani mkubwa sana hasa ndani ya nchi mana wengi walijawa uchu wa madaraka na kuzionaa sera zake za kijamaa ni sera kandaminzi na za kimasikini mna wafanyabiashara wakubwa walinyangangwa mali zao nyingi zilitaifishwa na viongozi wa chama naserikari kuwekewa vizuizi vingi katika suala la umiliki wa mali kupitia azimio la arusha..

Vita vya uganda navyo viliangusha sana uchumi wa nchi...na kusababisha hali ngumu sana ya kiuchumi.

Ila he was and always will remain the best president mpaka sasa katika nchi hii.

#MaendeleoHayanaChama
Mkuu, bado hukuelewa lengo la siasa ya ujamaa lilikuwa nini. Huwezi kusema ujamaa ulifeli huku huonyeshi ubepari ulipofanikiwa wakati huo wa hali duni sana kiuchumi duniani kote.

Ni rahisi sana watu kusema ujamaa ulifeli, ujamaa ulileta matatizo, lakini hawana uwezo wa kueleza kwa vipi.
Sana sana ni kurudia propaganda zile zile za enzi za vita baridi.
 
Sera za ujamaa hazikuwa mbaya ila Kambarage alipoteza mapato ya nchi kusaidia wengine wapate uhuru wewe fikiria kule Kongwa walikuwa wanalishwa tu bure bure na hizo nchi kwa Sasa hazina hata shukrani kwa Watanzania ,unakijua kisa Cha Kambarage kuuza Meli ya serikali kimyakimya na Sokoine akataka kumtumbua bosi wake.
Duh, hadithi za ajabu sana hizi. "Sokoine amtumbue Nyerere"?

Tueleze hiyo "stori" ya meli iliyouzwa kimya kimya!
 
Umeandika vizuri mnoo... ila kawawa hakuwahi fungwa na mauaji yaliyomfanya mwinyi ajiuzuru hayafikii yale ya mkapa 2000
 
Hizi ni mburula zilizolishwa ujinga makusudi hadi zmepofuka!

Awamu zilizofuatia baada ya Mwalimu zote zime/zilijaa marushwa makubwa...sasa yeye kwa ujinga wake anaona ndio maendeleo
Wakishika smartphone mtandaoni sasa hivi na kushinda miguu juu kwenye sofa na chumba chenye AC mchana kutwa usiku kucha, wanadhani maisha ndivyo yalikuwa tangu mwanzo.

Usahaulifu huu ni wa kiwango cha Mchina.
 
Ubepari Ulifanikiwa huku

Ujerumani Magharibi
Korea Kusini
Japan
Zimbabwe
Botswana.
Mkuu, bado hukuelewa lengo la siasa ya ujamaa lilikuwa nini. Huwezi kusema ujamaa ulifeli huku huonyeshi ubepari ulipofanikiwa wakati huo wa hali duni sana kiuchumi duniani kote.

Ni rahisi sana watu kusema ujamaa ulifeli, ujamaa ulileta matatizo, lakini hawana uwezo wa kueleza kwa vipi.
Sana sana ni kurudia propaganda zile zile za enzi za vita baridi.
 
Sera za ujamaa hazikuwa mbaya ila Kambarage alipoteza mapato ya nchi kusaidia wengine wapate uhuru wewe fikiria kule Kongwa walikuwa wanalishwa tu bure bure na hizo nchi kwa Sasa hazina hata shukrani kwa Watanzania ,unakijua kisa Cha Kambarage kuuza Meli ya serikali kimyakimya na Sokoine akataka kumtumbua bosi wake.
😂😂🤣🤣 Hii ya kuuza meli kimya kimya hadi kunusurika kutumbuliwa na Sokoine sikuwahi kuisikia hiyo mkuu. Dah kweli JF ina wajuzi wengi wa kimya kimya.
 
😂😂🤣🤣 Hii ya kuuza meli kimya kimya hadi kunusurika kutumbuliwa na Sokoine sikuwahi kuisikia hiyo mkuu. Dah kweli JF ina wajuzi wengi wa kimya kimya.
Ilikuwa balaa jamaa alienda dodoma ,akasema nikifika dsm mkuu wa nchi atangaze la sivyo ama yeye au mimi........
 
Ilikuwa balaa jamaa alienda dodoma ,akasema nikifika dsm mkuu wa nchi atangaze la sivyo ama yeye au mimi........
😂😂😂😂 Oh kwahiyo baada jamaa kusema hivyo, alipokuwa anarudi Dar kutoka Dodoma ndo yakatokea yale yaliotokea au nimewaza tofauti?
 
Pole mkuu. Nchi nyingi za kiafrika zilipata uhuru bila ya kuwa na human resources za uhakika za kusaidia uendeshaji wa serikali.
Muda mfupi baada ya nchi hizi kupata uhuru, zilijikuta zikiendelea kutegemea resources za kikoloni kama jeshi, mahakama na hata katiba.
Mwaka 1964 jeshi lilipoasi moja ya sababu kubwa lilipinga kuongozwa na wazungu. Kumbuka mpaka tunapata uhuru, jeshi lilikuwa chini CDF mzungu Brigedia Douglas, na wakati huo jeshi lilikuwa likiitwa KAR-Kings African Rifles. Na ndilo lililoasi mwaka 1964 kwa madai ya kupinga kuongozwa na wazungu na kutaka nyongeza ya mshahara. Mwalimu alitafuta msaada akianzia Kenya na baadaye Uganda na alikuta kote hali ni tete ni Kama wanajeshi waliambiana.
Ilimlazimu kuomba msaada uingereza ambako alipata msaada wa makomandoo 60 na ndio walifanikiwa kuzima uasi 1964. Na baadaye Mwalimu alivunja jeshi lote na kuanza kuunda upya chini ya Cdf wa kwanza wakati Kanali Hagai Mirisho Sarakikya na inasemekana kulikuwa na wanajeshi watatu tu wenye elimu za kijeshi kutoka vyuo vilovyoheshika Kama Sandhurst Uingereza. Mwalimu aliunda jeshi tulilonalo sasa JWTZ. Sasa history ni ndefu Sina hakika naweza kueleza yote, hata hivyo uasi ulitokea tukiwa hatuna itikadi ya ujamaa na utaona nchi nyingi za kiafrika zilizopata Uhuru miaka hiyo bila kujali itikadi zao zilipitia pagumu Sana hususani Africa ya magharibi.
Wakati kina Mwinyi wanaongia mambo yalikuwa yamebadilika Sana, angalau human resources ilikuwa imeongezeka, jeshi limestabilize na hata mahakama.
Lakini viongozi pia kutokana na waliyopitia bila shaka walijawa na woga, na siku zote mtu akiwa muoga hata maamuzi mengi yatakuwa na sura ya kujihami. Nadhani wengine wataongezea au kusahihisha.
Kwa comment hii nafikiri mleta mada sambamba na sisi tuliongia kusoma uzi huu tutakuwa tumekuelewa vizuri mkuu.
 
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salamu, ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu zangu watanzania, baba yetu wa Taifa mwl Julius K Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa muda wa miaka 25. Kwa muda wote huo wa uongozi wake, nchi yetu ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo haikuja kutokea katika tawala zingine. Mfano wakati wa utawala wa Nyerere tuliona majaribio mawili ya mapinduzi yalioshindwa, hali iliyopelekea mzee wetu aamue kung'atuka mwenyewe kabla haja ng'atuliwa, maana kwa hali ya nchi ilivyokuwa kipindi kile bila shaka mwenyewe aliona kwamba asingeweza kumaliza miaka mingine mitano akiwa madarakani.

Lakini pia ukiachana na hayo ya mapinduzi pia kulikuwa na misuko suko mingine, mfano yale mauaji yaliosababisha waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule mzee wetu mh Ally H Mwinyi kujiuzulu uwaziri. Pia kulikuwa na misuko suko mingine iliyopelekea kina mzee Kawawa, bibi Tito Mohammed na wengineo kufungwa jela. Lakini kama hiyo haitoshi, wapo waliamua kukimbia hata nchi na kwenda kuishi ughaibuni, mfano mzee wetu hayati Oscar Kambona na wengineo.

Hapo sijagusia ukosefu wa vitu muhimu nchini kama vile chakula, mafuta ya kupikia na ya taa, ukosefu wa madawa hospitalini, usafiri kuwa washida mpaka yakaletwa yale magari yalioitwa chai maharage, mzunguko wa pesa mtaani ukawa wa mdondo. Nguo, viatu, soksi, mafuta ya kupaka, sabuni navyo vikawa havipatikani.

Cha kushangaza alipoondoka mwl Nyerere na kuingia Mwinyi, hali ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliethubutu kuwaza tena mapinduzi, bidhaa zote muhimu zilipatikana kwa urahisi mitaani. Mzunguko wa pesa ukawa mkubwa, mitumba ya nguo, viatu, soksi kila kona, madawa yakawa mengi hospitalini mpaka watu wakaamua kufungua na zahanati zao. Pia hakuna aliewaza tena kukimbia nchi, isipokuwa tuliishuhudia wale waliokimbia utawala wa kwanza wanaaza kurejea katika utawala huu wa pili nk.

Hali hii aliyoanza nayo Mwinyi, naona imeendelea hadi leo. Je, ni kwanini misuko suko ilikuwa zaidi wakati wa awamu ya kwanza na sio awamu zingine? Je mwl Nyerere alihujumiwa au sera zake mwenyewe ndio zili muhujumu? Inamaana mzee Mwinyi kwa kutumia uwezo wake na cheo chake aliweza kulisuka vizuri jeshi letu na kurejesha utiifu wao kwa serikali yao na raisi wao? Je inamanaa MwinyiK hakufungwa jela. hakuwa na maadui wa kuitingisha serikali yake, hadi kupelekea wengine kukimbia kama walivyokimbia awamu ya kwanza? Mwenye kujua zaidi sababu zilizopelekea mwl Nyerere kushindwa kuituliza hali, hadi kuamua kung'atuka anakaribishwa kutujuza. Asanteni sana kwa kunisoma?
Kawawa hakufungwa jela.
 
Back
Top Bottom