thesym
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 3,843
- 4,796
Legacy kubwa ya Mao ni kuanzisha serikali ya kikomunist ambayo iliweza kuiondoa serikali ya komintang ulivyokuwa Chini ya Chieng Kai shek.Mao alifanikisha kitu gani China hadi amekuwa na historia kubwa hivyo duniani??!
Legacy yake ni ipi hasa?
Chieng Kai shek alikuwa raisi WA China, serikali yake ilipendwa Sana na wafanyabiashara na matajiri wakati huo China ilikuwa na tatizo kubwa la ardhi.
Watu wachache walimiliki maeneo makubwa, huku watu wengi wakiwa hawana ardhi.
Mao aliwahidi mageuzi ya ardhi watu waishio vijijini hivyo wakomyunisti wakapata uungwaji mkono WA kiwango cha juu vijijini na watu maskini wengi.
Na wakati huo Japan aliivamia China, Rai's China Cheng Kai shek alikataa kuingiza jeshi Kwa lengo la jeshi lake kupambana na wakomyunisti, huku akitumai USA kupambana na Japan.
Wakina Mao waliendelea kupambana na Japan mpaka pale Raisi WA China alipotekwa na walinzi wake na kulazimisha kuingiza jeshi na kupambana na wavamizi.
Pia serikali ya China kabla ilinuka rushwa.
Makosa Chei Kai Shek aliyoyafanya China yalimpa somo na hakurudia makosa walipokimbilia Taiwan, na baadae Taiwan ikawa ina maendeleo makubwa kuliko China bara.
Mao alikuwa ni mtu anayejua kushawishi watu Ila kuhusu uchumi ulikuwa ni changamoto kwake.