Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #41
Hahaha..Kwa comment hii nafikiri mleta mada sambamba na sisi tuliongia kusoma uzi huu tutakuwa tumekuelewa vizuri mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha..Kwa comment hii nafikiri mleta mada sambamba na sisi tuliongia kusoma uzi huu tutakuwa tumekuelewa vizuri mkuu.
Huna unachojua kuhusu utawala wa Nyerere zaidi ya stori za kijinga kijinga tu.Yule si alikuwa anaongea maneno mengi sana huku utekelezaji hakuna,misemo na nahau zisizoisha..
Alikuwa hapendi ukosoaji na hataki changamoto za wasomi ndio maana hakutaka kusambaza elimu kwa watu wengi,aliwafanga watu wengi kuwa wajinga Ili awatawale kirahisi.
Miaka 25 ya utawala alichofanikiwa kikubwa ni kujenga utaifa na yeye binafsi kuwa muadilifu ila hakuna succession aliyofanya na aliondoka madarakani kutokana na Hali mbaya ya uchumi na sera zake mbovu za Uchumi..
unamdanganya nani hapa Kwamba Sokoine alitaka kumtumbua bosi wake ?.Sera za ujamaa hazikuwa mbaya ila Kambarage alipoteza mapato ya nchi kusaidia wengine wapate uhuru wewe fikiria kule Kongwa walikuwa wanalishwa tu bure bure na hizo nchi kwa Sasa hazina hata shukrani kwa Watanzania ,unakijua kisa Cha Kambarage kuuza Meli ya serikali kimyakimya na Sokoine akataka kumtumbua bosi wake.
Kawawa hakuwahi kufungwa.Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salamu, ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu zangu watanzania, baba yetu wa Taifa mwl Julius K Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa muda wa miaka 25. Kwa muda wote huo wa uongozi wake, nchi yetu ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo haikuja kutokea katika tawala zingine. Mfano wakati wa utawala wa Nyerere tuliona majaribio mawili ya mapinduzi yalioshindwa, hali iliyopelekea mzee wetu aamue kung'atuka mwenyewe kabla haja ng'atuliwa, maana kwa hali ya nchi ilivyokuwa kipindi kile bila shaka mwenyewe aliona kwamba asingeweza kumaliza miaka mingine mitano akiwa madarakani.
Lakini pia ukiachana na hayo ya mapinduzi pia kulikuwa na misuko suko mingine, mfano yale mauaji yaliosababisha waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule mzee wetu mh Ally H Mwinyi kujiuzulu uwaziri. Pia kulikuwa na misuko suko mingine iliyopelekea kina mzee Kawawa, bibi Tito Mohammed na wengineo kufungwa jela. Lakini kama hiyo haitoshi, wapo waliamua kukimbia hata nchi na kwenda kuishi ughaibuni, mfano mzee wetu hayati Oscar Kambona na wengineo.
Hapo sijagusia ukosefu wa vitu muhimu nchini kama vile chakula, mafuta ya kupikia na ya taa, ukosefu wa madawa hospitalini, usafiri kuwa washida mpaka yakaletwa yale magari yalioitwa chai maharage, mzunguko wa pesa mtaani ukawa wa mdondo. Nguo, viatu, soksi, mafuta ya kupaka, sabuni navyo vikawa havipatikani.
Cha kushangaza alipoondoka mwl Nyerere na kuingia Mwinyi, hali ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliethubutu kuwaza tena mapinduzi, bidhaa zote muhimu zilipatikana kwa urahisi mitaani. Mzunguko wa pesa ukawa mkubwa, mitumba ya nguo, viatu, soksi kila kona, madawa yakawa mengi hospitalini mpaka watu wakaamua kufungua na zahanati zao. Pia hakuna aliewaza tena kukimbia nchi, isipokuwa tuliishuhudia wale waliokimbia utawala wa kwanza wanaaza kurejea katika utawala huu wa pili nk.
Hali hii aliyoanza nayo Mwinyi, naona imeendelea hadi leo. Je, ni kwanini misuko suko ilikuwa zaidi wakati wa awamu ya kwanza na sio awamu zingine? Je mwl Nyerere alihujumiwa au sera zake mwenyewe ndio zili muhujumu? Inamaana mzee Mwinyi kwa kutumia uwezo wake na cheo chake aliweza kulisuka vizuri jeshi letu na kurejesha utiifu wao kwa serikali yao na raisi wao? Je inamanaa Mwinyi hakuwa na maadui wa kuitingisha serikali yake, hadi kupelekea wengine kukimbia kama walivyokimbia awamu ya kwanza? Mwenye kujua zaidi sababu zilizopelekea mwl Nyerere kushindwa kuituliza hali, hadi kuamua kung'atuka anakaribishwa kutujuza. Asanteni sana kwa kunisoma?
Huwezi kuita mbinu za Japan na Korea kusini za maendeleo kuwa ni ubepari, nakupinga hiloUbepari Ulifanikiwa huku
Ujerumani Magharibi
Korea Kusini
Japan
Zimbabwe
Botswana.
Alieleta mageuzi ya maendeleo China ni Deng Xiaoping, China Chini ya Mao ilikuwa na Hali mbaya.Aliingia kwenye siasa za kijamaa bila kuwa tayari kulipa gharama kubwa kuzifanya zifanye kazi na kutekelezeka kama ilivyokuwa China chini ya Mao ambaye aliwatoa kafara Wachina million 20 ili kuifanya China ipige maendeleo chini ya Ujamaa.
Kote huko ni mchanganyiko. Hakuna mahali popote penye wenyewe ulipofanikiwa.Ubepari Ulifanikiwa huku
Ujerumani Magharibi
Korea Kusini
Japan
Zimbabwe
Botswana.
Nakudanganya weweunamdanganya nani hapa Kwamba Sokoine alitaka kumtumbua bosi wake ?.
Huna unachojua.Nakudanganya wewe
Nakujua weweHuna unachojua.
Get lost dude.Nakujua wewe
Umeshadokoa mboga Toto la mamaGet lost dude.
Inaonesha Historia ulilamba zero wewe.Umeshadokoa mboga Toto la mama
Mimi mwenyewe nimeshangaa, Kawawa kafungwa lini?Umeandika vizuri mnoo... ila kawawa hakuwahi fungwa na mauaji yaliyomfanya mwinyi ajiuzuru hayafikii yale ya mkapa 2000
Kote huko ni mchanganyiko. Hakuna mahali popote penye wenyewe ulipofanikiwa.
Alieleta mageuzi ya maendeleo China ni Deng Xiaoping, China Chini ya Mao ilikuwa na Hali mbaya.
Hapa siyo Facebook ZuZu weweInaonesha Historia ulilamba zero wewe.
"ZuZu" ndio nini ?.Hapa siyo Facebook ZuZu wewe