Kwanini utawala wa Nyerere ulikumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na utawala wa Mwinyi, Mkapa na wengine?

Huna unachojua kuhusu utawala wa Nyerere zaidi ya stori za kijinga kijinga tu.
 
unamdanganya nani hapa Kwamba Sokoine alitaka kumtumbua bosi wake ?.
 
Kawawa hakuwahi kufungwa.
 
Ubepari Ulifanikiwa huku

Ujerumani Magharibi
Korea Kusini
Japan
Zimbabwe
Botswana.
Huwezi kuita mbinu za Japan na Korea kusini za maendeleo kuwa ni ubepari, nakupinga hilo
 
Aliingia kwenye siasa za kijamaa bila kuwa tayari kulipa gharama kubwa kuzifanya zifanye kazi na kutekelezeka kama ilivyokuwa China chini ya Mao ambaye aliwatoa kafara Wachina million 20 ili kuifanya China ipige maendeleo chini ya Ujamaa.
Alieleta mageuzi ya maendeleo China ni Deng Xiaoping, China Chini ya Mao ilikuwa na Hali mbaya.
 
Ni mchanganyiko ila ubepari ulikiwa mwingi zaidi. Hata Marekani na Ulaya za leo kuna elements za ujamaa kwenye chumi zao ila yanatambulika kama mataifa ya kibepari.

Tunapozungumzia ujamaa tunaongolea ule ujamaa wa maduka ya Ushirika, mashamba ya kijiji na viwanda vya serikali kuzalisha sukari, sabuni na khanga. Hatuzungumzii ujamaa wa serikali kuchukua sehemu ya kodi ya matajiri kulipia huduma za afya maskini au kuwapa scholarships na misaada ya chakula.
Kote huko ni mchanganyiko. Hakuna mahali popote penye wenyewe ulipofanikiwa.
 
Mao alifanikisha kitu gani China hadi amekuwa na historia kubwa hivyo duniani??!
Legacy yake ni ipi hasa?
Alieleta mageuzi ya maendeleo China ni Deng Xiaoping, China Chini ya Mao ilikuwa na Hali mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…