Kwanini utawala wa Nyerere ulikumbwa na misukosuko mingi ukilinganisha na utawala wa Mwinyi, Mkapa na wengine?

Mao alifanikisha kitu gani China hadi amekuwa na historia kubwa hivyo duniani??!
Legacy yake ni ipi hasa?
Legacy kubwa ya Mao ni kuanzisha serikali ya kikomunist ambayo iliweza kuiondoa serikali ya komintang ulivyokuwa Chini ya Chieng Kai shek.

Chieng Kai shek alikuwa raisi WA China, serikali yake ilipendwa Sana na wafanyabiashara na matajiri wakati huo China ilikuwa na tatizo kubwa la ardhi.

Watu wachache walimiliki maeneo makubwa, huku watu wengi wakiwa hawana ardhi.

Mao aliwahidi mageuzi ya ardhi watu waishio vijijini hivyo wakomyunisti wakapata uungwaji mkono WA kiwango cha juu vijijini na watu maskini wengi.

Na wakati huo Japan aliivamia China, Rai's China Cheng Kai shek alikataa kuingiza jeshi Kwa lengo la jeshi lake kupambana na wakomyunisti, huku akitumai USA kupambana na Japan.

Wakina Mao waliendelea kupambana na Japan mpaka pale Raisi WA China alipotekwa na walinzi wake na kulazimisha kuingiza jeshi na kupambana na wavamizi.

Pia serikali ya China kabla ilinuka rushwa.

Makosa Chei Kai Shek aliyoyafanya China yalimpa somo na hakurudia makosa walipokimbilia Taiwan, na baadae Taiwan ikawa ina maendeleo makubwa kuliko China bara.


Mao alikuwa ni mtu anayejua kushawishi watu Ila kuhusu uchumi ulikuwa ni changamoto kwake.
 
Hivyo watu milioni 40 wanaokadiriwa kufa katika utawala wake kutokona na sera na mipango yake mbalimbali kama "great leap forward" na "cultural revolution" walikufa bure!
 
Hivyo watu milioni 40 wanaokadiriwa kufa katika utawala wake kutokona na sera na mipango yake mbalimbali kama "great leap forward" na "cultural revolution" walikufa bure!
Kabisa, Unapolazimisha kuendesha vitu Kwa mtindo WA One Man Army kinachofuata huwa ni majanga.
 
Shida ya Nyerere ilikuwa kumuona kila tajiri ni mwizi kitu ambacho hata chizi hawezi kukifurahia
 
Bila shaka huyo aliyeanzisha mada kwa lengo lake maalum, hawezi kamwe kusoma na kuelewa ulichoandika hapa.
Kwa sababu kinapingana na malengo aliyonuia kuyafikia.
 
Aliingia kwenye siasa za kijamaa bila kuwa tayari kulipa gharama kubwa kuzifanya zifanye kazi na kutekelezeka kama ilivyokuwa China chini ya Mao ambaye aliwatoa kafara Wachina million 20 ili kuifanya China ipige maendeleo chini ya Ujamaa.
Uh - Oh!
Hii nayo ni moja ya nadharia ya kufanya 'ujamaa' ufanikiwe, "kutoa kafara"?
 
Mao kwenye uchumi alijitahidi kwa nafasi yake lakini kiuhalisia hakufanikiwa sana ndio maana sera zake Kama great leap forward na cultural revolution zilipata upinzani hata ndani ya chama na kuzalisha faction kukawa na wanaosupport sera na wanaopinga sera Mao Zedong, zhuo enlai, hua Guefeng na gang of four walizisupport sera na kulazimisha kutekelezwa huku Deng Xiaoping , Xi Zhongxun [ baba yake na Xi Jinping ] walizipinga sera kwa Sana ilipelekea kusimamishwa na chama na kufungwa vifungo vya nyumbani wengine waliuliwa na gang of four. Baada ya Deng Xiaoping kuchukua hatamu baada ya Mao Zedong kufa aliwafyeka gang of four wote
 
Ni kwasababu, hatuoni picha kubwa. Picha kubwa ni kwamba raisi yoyote wa afrika akiwa na hulka ya kujenga nchi wakoloni/mabeberu wanamsumbua kupitia watu wanaitwa mercenaries. Hawa watu alikua anawaongelea nyerere kipindi kile cha utawala wake. Alikua anasema kuna watu "malaya malaya hivi", wanafanya chochote kwa kununuliwa na pesa za wakoloni. Rudi tafuta hotuba za nyerere utazipata.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Nakudanganya wewe
Kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba nyerere alikua anapambana na mabeberu/wakoloni. Waliondoka lakini bado walikua wanawatu wao nchini wa kuhakikisha utawala na unyanyaji unaendelea kisirisiri. So kwa nn mwinyi hakukutana na matatizo. Ni simple, ni kwa sababu alikua alikua hasumbuani na wakoloni. Aliwapa ruksa

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Mbona wachina walifanikiwa na sera za kijamaa kama ni za kimasikini.
Kwa kifupi mzee alikua amekaliwa shingoni na mabeberu. Kama mgabe alivokua amekaliwa

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Shukrani mkuu kwa kutuwekea kile unachokijua kuhusu uongozi ule wa awamu ya kwanza. Bila shaka washauri wake pia hawakuwa wazuri, maana walishindwa kumshauri mwl asome alama za nyakati kuhusiana na siasa za kijamaa.
Wangemshauri nini na katika Nick names zake, moja ni "haambiliki"
 
Mbona wachina walifanikiwa na sera za kijamaa kama ni za kimasikini.
Kwa kifupi mzee alikua amekaliwa shingoni na mabeberu. Kama mgabe alivokua amekaliwa

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
China hawakufanikiwa na mfumo WA kijamaa kama unavyodai.
Tangu mwaka 1978 China ilianza kufanya mageuzi ya kiuchumi. Moja ya reforms waliofanya ni kuanzisha special economic zones kwenye majimbo manane ya kusini.


Haya majimbo yalkiuwa Kwa ajili ya kujaribu market economy(ubepari) ambalo serikali za majimbo zilipewa mamlaka ya utekelezaji WA Sera za kibepari kuvutia wawekezaji kutoka nje na ndani

Na mwaka 1984 China ikaanzisha Nation Economic and Technology Development Zones kwenye mikoa 14

Moja majimbo hayo ni Shenzhen na Guangzhou kiujumla, na hiyo mikoa Nane ikatokea ikawa inachangia zaidi ya 50% ya GDP ya China wakati huo.

Shenzhen ilikuwa ni kijiji cha wavuvi lakini Leo inaitwa silicon valley ya china
Ni kipindi hiko kampuni nyingi za USA, Europe, Japan walihamisha uzalishaji kwenda China, na serikali ikawa ina-transfer teknolojia na kuiba pia kupitia makampuni yaliyotaka kuwekeza China.

Kiujumla China inafuata model ya Japan
 
60s to late 80s,that was cold war era,west against eastern block,USA,UK against Soviet blocs
 
Bila Nyerere kuweka misingi ya amani hakuna kiongozi ambaye angekuja kufanya lolote.
Nyerere alikazania utaifa ndio.maana alifanya maamuzi magumu ya kutaifisha shule ili watu was imani zote wasome bila kufanya hivyo ai ajabu mtoa mada ungekuwa madongo kuinama.
Alihakikisha rasilimali za taifa zitumike kwa manufaa ya taifa ndio maana pamoja na kujua uwepo was dhahabu na madini mengine aliamua kusoma wataalamu badala ya kuingia mikataba ya kitapeli ingawa Nate kama binadamualikuwa na mapungufu mambo mengi alifanya kwa manufaa ya ya taifa.
 
60s to late 80s,that was cold war era,west against eastern block,USA,UK against Soviet blocs
Oh ndo maana nchi nyingi za Africa ikiwemo Tanzania ziliathiriwa na cold war zile. Kwahiyo hii ilisababisha kwa namna fulan nchi isitawalike?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…