Hili swala la matokeo ya oral ni muhimu sana hata kama sio kwa kuonesha exactly pass marks basi uwepo utaratibu wa kujua pass marks nilifikisha but ufinyu wa nafasi ndio umenifanya nikose placement.
Unakuta unajipa stress kufatilia placement kumbe hata pass mark ukufikisha lakini kama ukijua nilifeli ni rahisi kuulizia kwa wadau wao walijibu vipi ili next time nikiitwa usaili nijiupgrade kwa zile weakness ambazo nahisi zilinikosesha kufaulu.
Unakuta unaenda kupiga oral interview nyingine unarudia makosa yaleyale yaliyo kufelisha mwanzo yote hii ni kwasababu ukujua kama ulifeli au ulifaulu.
Mfano kwenye written mtu unafeli pepa ya kwanza unafatilia kwa wadau unagundua tatizo labda points zangu hazikuwa direct au niliandika sana mpaka muda ukaniishia bila kumaliza maswali hii inakufanya next pepa haurudii makosa ambayo uliyafanya mwanzoni hii imesaidia wengi kwenda kwenye oral baada ya kupokea ushauri kutoka kwa wadau
Lakini sasa hii ya mtu anafungia matokeo kabatini sio sawa hata kidogo na inatoa mianya ya kuyapika [emoji16] maana hakuna anaeyajua