Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mimi naomba kutoa comment kuhusu hili, ntaongelea experience yangu, mwaka jana ndo nlimaliza law school, nlikuwa sina hamu kabisa na kazi za serikalin maana tyar nlikuwa na biashara yangu iliosimama asikwambie mtu, inshort nlikuwa sikwami kwa lolote, baadae mwezi wa 12 mwanzoni panya road walinipitia aisee, inshort waliniacha mtupu, nlitamani kujinyonga, hapohapo sisi wadada wa vikoba tukatapeliwa huko, nami nikawa na madeni since nlikuwa nategemea hela vikoba baada ya duka kuyumba nmalizie hayo madeni ambapo kipindi hicho nliona hela ndogo sana.
Duka nikafunga kabisa, inshort nlichanganyikiwa na mipango yote ilisimama, nliona ata Dar hapanifai nkarudi kijijini kwanza maana nlikuwa naona nakufa kwa depression, hapo sehem nlipokuwa nafanya intern babu yule pia alizingua kila siku kunitaka kumkataa ikawa kesi, nalipwa hela kidogo ila kazi ninazofanya acha tu, na mimi nlitaka tu experience kwa hiyo mwanzo sikujali muda ulivyoenda, babu anasumbua hapohapo nina mihuri yangu kazi karibia asilimia 80% nafanya mimi na mateso nakaa hadi saa mbili sometimes nkaona niache tu.
Nlirudi kijijini nikakaa hadi mwezi wa tatu, mdogo wangu ambae kiukweli sitamsahau huyo dada, hatuna undugu kabisa ni rafika tu ndo alikuwa ananipa moyo, aliomba hadi nitoke home nikakae nae kwao niwe na mtu karibu maana familia yangu kuna namna siwez ongea zaidi hapa, nkawa naona anaapply kazi na mimi nkaanzia hapo kuapply kazi za psrs, mwezi wa nne nkaona kama nimepona naweza rudi Dar nianze biashara yangu since nmeshaijua na nina wateja wangu wa kutosha siwez kulala njaa, mwanzon ilikuwa ngumu kwa mtu ambae ashazoea kuwa na duka then anaanza upya tena kuuza online, ila sasa hivi namshukuru sana Mungu maisha yanaenda though sio kama mwanzo ila nlikubali matokeo na siwazi tena kitu, ata interview zikifika nauli siwazi, interview ya kwanza ndo nlifanya mwezi wa tano na nikafika oral ndo mpaka leo hawajahi kuplace tetesi zikawa kuwa walishaitwa kwa juu juu ila sijawahi kukata tamaa.
Lengo la maelezo haya ni kuwa hapa duniani usije ukakaa na kutegemea kitu kimoja, ukiwa na biashara kama mtaji unatosha kuwa nazo ata mbili tofauti kabisa, ukiwa na kazi kuwa ata na biashara pemben kwamba kimoja kikikwama bado maisha yataendelea,
Nlipopata matatizo kwenye biashara yangu ndo hiyo pekee nlikuwa naitegemea, ndo nikawa kama wale from 100 to 0, lakini nkaimagine ningekuwa na kazi ya kueleweka mshahara wa mwezi mmoja tu au miwili ungenipa kianzio na biashara yangu ikaendelea kama kawa ata kama sio kama mwanzon lakin nisingehangaika vile.
Mimi nawashauri tu tusikate tamaa, kama una mishe zako unafanya na zimeshaeleweka kitaa tafuta ata kazi ata huku psrs tunakohangaika nako uwe na security ya kutosha, siku kazi imezingua biashara ako ipo, au siku biashara imezingua kazi ipo. Tusitegemee kitu kimoja wadau.
Samahani kwa uzi mrefu[emoji16]
Pole sana mkuu.

Hiki kitu ndio nimejifunza kwenye uwekezaji.

Panya road ni watu wabaya sana, hawa tunaoona wanachomwa moto huku Dar huwa natamani achomwe halafu aipuliwe kabla hajakata roho ili ayasikilizie maumivu halafu arudishwe tena jikoni amalizikie.

Kwa hiyo katika kuwekeza, security ni kipaumbele, iwe ulinzi wa goli au ulinzi wa backup ya mtaji.

Ukiwa na kazi rasmi angalau pana unafuu hata kama mambo yakizingua hautaweza kulala njaa.

Tuendelee kupambana kwa namna mbalimbali tunazoona zinafaa ili tuweze angalau kuwa stable kwenye vijisenti
 
Safi sana kwa kumkataa Babu nipo hapa kijana mwenzio nikubalie mie nakupenda sana jamani Hadi naumwa
Pole sana baby kwa kuandika uzi mrefu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ongezea pia "Kwa sasa nasubiri mchakato wa kazi umalizike nikaanze kazi" [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kumbe huwa hubeti mkuu, sasa nauli za kwenda Dom unatoa wapi?. Kumbuka sisi ni majobless na weng wetu umri wa kuomba nauli ulishapita.
Hiyo kubeti nilimaanisha mkeka upi utatoka kati ya hii ambayo bado haijatoka ya kuitwa written.

Kwenye suala la nauli za kwenda kukandwa, vijiwe vinatuokoa huku kitaa.

Imagine muda huu ndio nimetoka kijiweni ninapopatia vijisenti naelekea kupumzisha fuvu nyumbani[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom