Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ma legend wa uzi huu tumepotea au tumeshasahaulishwa na hizi asali tulizolamba??

Mkuu mfwende sawadogo upo wapi siku hizi ndugu yangu ulikuwa mchangiaji mzuri umepotea mazima, na wengine wengi tu.

Au ni zama zilishapita, kizazi kipya kimekuja na hasira za kutukana ila silaumu najua uchungu wa kuwa jobless inakera sana yaani... Ila ni swala la mda tu kila kitu kitaenda sawa.
Mkuu,baadhi tulibahatika kulamba hiyo vijana tunaita asali,ila mazingira tuliyolamba hiyo asali imegeuka shubiri. Kuna Baadhi ya Wilaya katika hii nchi ukipangwa kwenda kufanya kazi unatamani bora ungebaki kwenu Chalinze ulime nanasi.
 
Mishahara mingine ya February kuendelea unamuachia nani mzee? Au huko hata usafiri niwa punda?
Nadhani ni kwasababu mimi si mfuatiliaji sana wa jukwaa hili,ila laiti ningejua hali halisi ya Halmashauri nyingi,nisingekubali kuja huku.
 
kwa hiyo mnata kutuaminisha kua kwa hiyo asali ya halmashauri ni ya nzi wa chooni..
Kama una uhakika na mishe zako za huko mtaani,huku hapakufai. Ni kupotezeana tu muda. Katika maishi nimejifunza kusimamia na kukamilisha kile ulichokianza. Haya mambo ya kuhama leo huku unafanya jambo hili kesho kule unafanya jambo lile yanaturudisha sana nyuma.
 
Mkuu,baadhi tulibahatika kulamba hiyo vijana tunaita asali,ila mazingira tuliyolamba hiyo asali imegeuka shubiri. Kuna Baadhi ya Wilaya katika hii nchi ukipangwa kwenda kufanya kazi unatamani bora ungebaki kwenu Chalinze ulime nanasi.
kwanini
 
Back
Top Bottom