Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wakuu aminini nawaambia nyie ambao sijui mnaitwa interview, sijui mnaenda mpaka oral, mnabaki kweny database mna afadhali wakuu, sisi wengine toka tumalize miaka hiyo hatujawahi omba ajira yeyote kupitia Ajira Portal, kiufupi tunawaonea donge nyie ambao atleast mnaishi kwa matumain flani huenda kuna siku mtalamba asali....[emoji88]
Mkuu ulisoma coz gani?
 
Ndugu katika mapambano tuendelee kuongeza received mapambano yaendelee, #consistence is the key

Wengine ata received ni tatizo… nimemaliza chuo 2020 kazi zetu zilitoka mara moja tena nafasi 4. Mpaka leo bilabila….

Ila wakati mwingine ni mbaya sana kusoma course ambayo inatolewa na chuo kimoja tu🥲
 
Mkuu iko hivi: Recategorization ni kubadilishiwa muundo wa utumishi. Kila kada ina muundo wake wa utumishi unaoainisha ngazi ya chini hadi ya juu. Kwa hiyo ukibadilisha kada ni lazima ubadilishiwe muundo wa utumishi.

Kwa mfano: Muundo wa utumishi wa walimu wenye degree unaanzia TGS D hadi TGS I. Kama kulikuwa na mtumishi ambaye ni mhudumu, muundo wake wa utumishi unaanzia TGOS A na kuendelea. Kama akajiendeleza na kuomba kwenda kusomea diploma ya ualimu.

Muundo wa utumishi wa walimu wenye diploma inaanzia TGS C hadi TGS G. Huyu aliyekuwa mhudumu na amepata diploma ya ualimu na mwajiri wake anayo nafasi ya ualimu, basi atambadilishia muundo wake wa utumishi toka TGOS hadi TGS.

Kitendo hicho cha kubadilishiwa muundo wa utumishi baada ya kuongeza sifa ndicho kinaitwa RECATEGORIZATION
Kwa mtu aliyeajiriwa kwa dip ingali ana bachelor akifika kazini akataka kufanyiwa recategorization inawezekana?
 
Back
Top Bottom