Kwanini vitabu vya dini havijataja sayari zingine zaidi ya Dunia?

Dini zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu kwa maelfu ya miaka, zikitoa mwongozo wa kimaadili na kiroho. Hata hivyo, kuna hoja mbalimbali zinazotumiwa kuonyesha kwamba dini ni utapeli. Moja ya hoja hizi ni kwanini vitabu vya dini havijataja sayari nyingine zaidi ya Dunia.

Vitabu vya dini, kama vile Biblia, Quran, na vingine, vimeandikwa na watu wa zamani ambao walikuwa na uelewa mdogo sana wa sayansi na anga za mbali. Wakati wa kuandikwa kwa vitabu hivi, sayari nyingine hazikujulikana na hazikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watu. Hii inaonyesha kwamba vitabu hivi vilikuwa ni tafakuri ya maarifa na imani za watu wa wakati huo, badala ya kuwa na ufunuo wa kweli kutoka kwa nguvu za juu zinazodaiwa kuwa na maarifa yote.

Zaidi ya hayo, ukweli kwamba vitabu vya dini havijataja sayari nyingine unazua maswali kuhusu uhalali wa madai yao ya kiroho na kiufunuo. Kama kweli vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa kwa mwongozo wa nguvu za juu, ni kwa nini hazikuweka maarifa ya msingi kuhusu ulimwengu unaotuzunguka? Hii inaongeza wasiwasi kwamba dini zinaweza kuwa zimeundwa ili kudhibiti na kuongoza jamii, badala ya kutoa maarifa ya kweli na sahihi.

Kwa mtazamo wa kisayansi, maendeleo mengi yamefanywa tangu wakati wa kuandikwa kwa vitabu vya dini. Sayari kama Mars, Jupiter, na Saturn zimegunduliwa, na tumeweza hata kutuma vyombo vya anga kwenye baadhi ya sayari hizi. Hii inaonyesha kwamba maarifa ya kisayansi yanabadilika na kupanuka, wakati maarifa ya kidini yamebaki kuwa yale yale kwa maelfu ya miaka.

Hitimisho ni kwamba, hoja ya kwanini vitabu vya dini havijataja sayari nyingine zaidi ya Dunia inaweza kuonekana kama ushahidi kwamba dini ni utapeli. Inaonyesha kwamba vitabu hivi ni bidhaa za maarifa ya wakati wao, na si ufunuo wa kweli kutoka kwa nguvu za juu zinazodaiwa kuwa na maarifa yote.
Kama dunia tu ilikuwa inafikiriwa ipo kama meza,unadhani sayari nyingine zingetambulika?Binadamu amepewa uelewa lakini ili kupembua mambo,muda ulihitajika.
 
Quran imejaa Aya za Anga, na Wana sayansi wengi wa Mwanzo walikua inspired na Quran na kuanza kufanya Exploration Ya Anga.

Baadhi ya Aya za Quran zinazohusu Anga

1. AND IT IS We who have built the universe with [Our creative] power; and, verily, it is We who are steadily expanding it. Quran 51:47

Hapo Mwenyez Mungu anaelezea yeye ndio Ameumba Universe na yeye ndio anaeitanua, hii ni Ugunduzi wa karibuni tu kwamba Universe ina Expand

2.And We made heaven as a guarded roof. Yet they are ones who turn aside from its signs. QURAN 21:32

kila mtu sasa hivi anajua kwamba Anga ni kama paa linalotulinda na vilivyo nje ya Dunia kama mwanga wa jua etc.

3.and [fail to see that] it is He who has created the night and the day and the sun and the moon - all of them floating through space Quran 21:33

Hio Aya inayo jibu swali lako

4. ARE, THEN, they who are bent on denying the truth not aware that the heavens and the earth were [once] one single entity, which We then parted asunder? – and [that] We made out of water every living thing? Will they not, then, [begin to] believe Quran 21:30

Hapo Mwenyez mungu anaelezea Universe ilikua ni kitu kimoja na kikajiachia, theory ambayo inaelezewa kama Bing bang, Pia anaelezea kuhusu viumbe vyote hivyo

Kuna Aya nyingi za Anga na nyengine zinaingia deep zaidi, hivyo si kweli kwamba vitabu vya dini havijazungumzia, it's just vijana wa siku hizi ni much know sana, Ego 99.9999% na kujifanya mnajua kila kitu na Elimu 0.0001%

Nisingependa kujielekeza kuongelea hadithi za Sumerians na Hindu ambazo zilikuwepo miaka elfu nyingi kabla ya Quran lakini hiyo Big bang yenyewe hapo inavyoelezewa ni kituko kitupu. Bing bang inaelezea expansion ya universe from singularity sio kujiachia au kuwa parted asunder kama vile unakata mnofu kwenye pande la nyama🤣
 
Quran imejaa Aya za Anga, na Wana sayansi wengi wa Mwanzo walikua inspired na Quran na kuanza kufanya Exploration Ya Anga.

Baadhi ya Aya za Quran zinazohusu Anga

2.And We made heaven as a guarded roof. Yet they are ones who turn aside from its signs. QURAN 21:32

kila mtu sasa hivi anajua kwamba Anga ni kama paa linalotulinda na vilivyo nje ya Dunia kama mwanga wa jua etc.
Sina uhakika hata unapozungumzia heavens unamaanisha nini lakini itoshe kusema hii sio sayansi unayozungumia hapa, ozone layer sio space.
 
Kazi ya kuzitaja majina tumepewa sisi binadamu tuchunguze.
Alafu hizo sayari ni chache sana.tunazozijua
 
Huwa unasoma mwenyewe au unaokoteza stori za mtaani? Kaini alipofukuzwa aliondoka na mke wake tayari sio kwamba alienda kuoa kule alikoenda na mke alikuwa ni dada yake kwa sababu Adamu alikuwa na watoto wa kike na Mungu wakati huo aliruhusu wazaane kwa sababu wao ni watu wa kwanza, amri ya kuzuia ndugu kuoana ilikuja baadae sana

Ukisoma Mwanzo 1:1 inasema, Mungu aliumba mbingu na nchi halafu ndo inaendelea kukwambia nchi ilikuwa ukiwa na utupu sasa unachoshangaa hapo ni nini? Yani bado unauliza vimetokea wapi kwani ushasahau kwamba ulisoma Mstari wa 1?

Yani hata watu wa zamani walioandikwa kwenye Biblia hiyo hiyo walikuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja kuliko mwanasayansi wewe
nyie akili mlishaazimisha kwengine kama unaona huo ndio mwanzo baki hivyohivyo, kutoka huko mtu anatoka na fikra zake so bado hujafikia hiyo hatua
 
😂🤣😂🤣😂🤣
 
Dini imetaja ulimwengu yaani universe na ndani ya ulimwengu ndimo mlimo sayari zingine.

Kwahiyo ulivyoambiwa umeubwa uje uutawale ulimwengu inamaanisha Dunia pamoja na vyote vilivyopo nje yake, ila dini imeongelea sana Dunia kwakua ndimo wewe ulimo ila ukijiongeza na kutoka nje ya mipaka hii ya Dunia still bado utakua ndani ya universe so baba yako wa mbinguni atafurahia kwamba alichokutuma unakitimiza vyema 😆😆

Ulimwengu ni jumla ya vitu vyote vilivyopo. Inajumlisha Dunia yetu pamoja na kila kitu ndani yake, jua letu, mfumo wa jua, sayari, nyota, galaksi n.k. Ni jumla ya mata, nishati na anga la Dunia pamoja na anga-nje.
Saaasaa kama ndivyo, kwanini alikasirika wakati watu wa babeli walipotengeneza mnara? Si angewaacha tuu ilihali anajua kabisa hawataifikia mbingu yake
 
Naongea na atheist ama? If so, goodbye.
Am not Atheist..
Tatizo la watu wengi wakiona hawawezi kujibu Maswali bhasi lazima wasingizie Kuhsu atheist..

Nimeuliza maswali ambayo yanahitaji majibu yako wewe..

Fuatilia Post zangu mimi sio atheist na siwezi kuwa atheist ila swala ni kwamba kwanini mnapoulizwa maswali magumu bhasi mnakimbilia Kuhusu Atheist??

Ukiulizwa swali ambalo unahisi Una jibu iwe limeulizwa na Agnostic (Atheists) au Ignostic au Gnostic mwenzako kwanni usilijibu kwanza ?
 
Saaasaa kama ndivyo, kwanini alikasirika wakati watu wa babeli walipotengeneza mnara? Si angewaacha tuu ilihali anajua kabisa hawataifikia mbingu yake
Sasa hii ni another case kwasababu kama mnara wa babeli ilikua ni wakutoka nje ya mipaka ya dunia tu basi hata hizi project ambazo zinaendelea Sasa hivi kama zile za space ☓ huko kwenye sayari ya Mars zisingeendelea.
 
nyie akili mlishaazimisha kwengine kama unaona huo ndio mwanzo baki hivyohivyo, kutoka huko mtu anatoka na fikra zake so bado hujafikia hiyo hatua
Ni ajabu kama mtu ameazimisha akili halafu bado anakuzidi wewe uliyenazo zote, kama unajua huo sio mwanzo tupe elimu ya huo mwanzo
 
Quran imejaa Aya za Anga, na Wana sayansi wengi wa Mwanzo walikua inspired na Quran na kuanza kufanya Exploration Ya Anga.

Baadhi ya Aya za Quran zinazohusu Anga

1. AND IT IS We who have built the universe with [Our creative] power; and, verily, it is We who are steadily expanding it. Quran 51:47

Hapo Mwenyez Mungu anaelezea yeye ndio Ameumba Universe na yeye ndio anaeitanua, hii ni Ugunduzi wa karibuni tu kwamba Universe ina Expand
Bila hata kuingia kwenye mjadala mrefu wa translation gani ya Quran umetumia(maana hii sio tafsiri ya Yusuf Ali au Shakir), hakuna kitu kama "universe" kwenye Quran, wewe hapo ni chumvi tu umeongezea. Kitu mtume wako alikuwa anajua kuzungumzia ni sky na heavens.

Halafu embu tuambie Quran 51:48 inasema "As for the earth, We spread it out. How superbly did We smooth it out! And the earth We spread it out, How well We smoothed it out"

Hii spread out inamaanisha ni expanding earth au flat earth??
 
Quran imejaa Aya za Anga, na Wana sayansi wengi wa Mwanzo walikua inspired na Quran na kuanza kufanya Exploration Ya Anga.

Baadhi ya Aya za Quran zinazohusu Anga

1. AND IT IS We who have built the universe with [Our creative] power; and, verily, it is We who are steadily expanding it. Quran 51:47

Hapo Mwenyez Mungu anaelezea yeye ndio Ameumba Universe na yeye ndio anaeitanua, hii ni Ugunduzi wa karibuni tu kwamba Universe ina Expand

2.And We made heaven as a guarded roof. Yet they are ones who turn aside from its signs. QURAN 21:32

kila mtu sasa hivi anajua kwamba Anga ni kama paa linalotulinda na vilivyo nje ya Dunia kama mwanga wa jua etc.

3.and [fail to see that] it is He who has created the night and the day and the sun and the moon - all of them floating through space Quran 21:33

Hio Aya inayo jibu swali lako

4. ARE, THEN, they who are bent on denying the truth not aware that the heavens and the earth were [once] one single entity, which We then parted asunder? – and [that] We made out of water every living thing? Will they not, then, [begin to] believe Quran 21:30

Hapo Mwenyez mungu anaelezea Universe ilikua ni kitu kimoja na kikajiachia, theory ambayo inaelezewa kama Bing bang, Pia anaelezea kuhusu viumbe vyote hivyo

Kuna Aya nyingi za Anga na nyengine zinaingia deep zaidi, hivyo si kweli kwamba vitabu vya dini havijazungumzia, it's just vijana wa siku hizi ni much know sana, Ego 99.9999% na kujifanya mnajua kila kitu na Elimu 0.0001%
Baba Mwajuma,
1. Concept ya universe imekuwepo miaka 500 BCE.
Huko ugiriki, wakina Pythagoras na Anixamander walishazungumzia universe mamia ya Karne kabla kurani haijaandikwa.
Vilevile, wakati kurani inaandikwa, tuyari wakina Mt. Augustine na Boethius walikuwa wameshaandika kuhusu ulimwengu kama muunganiko wa dunia na mbingu (space).
Hivyo basi, mungu wa kurani hakusema chochote kipya kuhusu anga. Waandishi wa kurani walichukua tu ideas za anga zinazokubalika wakati huo.

2. Kuhusu universe kuexpand:
Kurani kudai Mungu anapanua anga haina mahusiano ya moja kwa moja na cosmic expansion inayozungumzwa kwenye contemporary science ambayo unajaribu kuhusisha hapa.

3. Kurani imeandika concept nyingi tu ambazo ni unscientific. (Labda enzi hizo zilidhaniwa kuwa sahihi)
Mfano:
  • Jua kuzama matopeni
  • Kuchukulia anga kama Mbingu. Tena mbingu saba. Where is mbingu in the universe?
  • Kuchukulia Dunia kama tambarare inayoimarishwa na milima.
  • Kudhani kwamba jua linatembea (lina-move)
  • Kudhani kwamba viumbe vyote vipo viwiliviwili. Bacteria tu au amoeba wanaiprove kurani wrong.
  • Na Kadhalika.

Hivyo basi, kurani haina maajabu yoyote ya kuifahamu science. Waliandika kwenye vitabu vyao kilichoaminika na wanasayansi na jamii ya enzi hizo tu.
 
Sina uhakika hata unapozungumzia heavens unamaanisha nini lakini itoshe kusema hii sio sayansi unayozungumia hapa, ozone layer sio space.
Ayah za anga zipo nyingi , Qur an ina elimu ya anga kabisa kama ulikuwa hujui ....Elimu hii hata ukitaka tafuta wavuvi pale kigamboni watakuambia .
 
Baba Mwajuma,
1. Concept ya universe imekuwepo miaka 500 BCE.
Huko ugiriki, wakina Pythagoras na Anixamander walishazungumzia universe mamia ya Karne kabla kurani haijaandikwa.
Vilevile, wakati kurani inaandikwa, tuyari wakina Mt. Augustine na Boethius walikuwa wameshaandika kuhusu ulimwengu kama muunganiko wa dunia na mbingu (space).
Hivyo basi, mungu wa kurani hakusema chochote kipya kuhusu anga. Waandishi wa kurani walichukua tu ideas za anga zinazokubalika wakati huo.

2. Kuhusu universe kuexpand:
Kurani kudai Mungu anapanua anga haina mahusiano ya moja kwa moja na cosmic expansion inayozungumzwa kwenye contemporary science ambayo unajaribu kuhusisha hapa.

3. Kurani imeandika concept nyingi tu ambazo ni unscientific. (Labda enzi hizo zilidhaniwa kuwa sahihi)
Mfano:
  • Jua kuzama matopeni
  • Kuchukulia anga kama Mbingu. Tena mbingu saba. Where is mbingu in the universe?
  • Kuchukulia Dunia kama tambarare inayoimarishwa na milima.
  • Kudhani kwamba jua linatembea (lina-move)
  • Kudhani kwamba viumbe vyote vipo viwiliviwili. Bacteria tu au amoeba wanaiprove kurani wrong.
  • Na Kadhalika.

Hivyo basi, kurani haina maajabu yoyote ya kuifahamu science. Waliandika kwenye vitabu vyao kilichoaminika na wanasayansi na jamii ya enzi hizo tu.
Namba 3 ulichoandika hakina ukweli , nioneshe kweny Qur an jua linazama kweny matope ? Hlafu nitakufundisha kila kitu ! Hizo nyingine kama dunia tambarare ni kwamba wewe ndio huelewi .

Hakuna kiumbe aliyopo duniani akaona dunia ni duara , dunia ni tambara kweny surface ya juu pakiwa na milima ,tambarare ni usawa tuliokuwa nao ndio maana tunajenga majengo ...Achana na concepts kwamba dunia ni Duara hata iwe duara ila ndani yake ipo tambarare 😀 😛
 
Tunamaanisha kapigwa ngwara
Hapo umeelewa kuwa hakuna mtama wala hakuna kukatwa chochote, ni kupigwa ngwara. Nini kinachokufanya usielewe msemo wa "jua linazama matopeni"?

kama huelewi hilo muulize aliyenukuliwa alimaanisha nini aliposema hivyo?
 
Dini zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu kwa maelfu ya miaka, zikitoa mwongozo wa kimaadili na kiroho. Hata hivyo, kuna hoja mbalimbali zinazotumiwa kuonyesha kwamba dini ni utapeli. Moja ya hoja hizi ni kwanini vitabu vya dini havijataja sayari nyingine zaidi ya Dunia.

Vitabu vya dini, kama vile Biblia, Quran, na vingine, vimeandikwa na watu wa zamani ambao walikuwa na uelewa mdogo sana wa sayansi na anga za mbali. Wakati wa kuandikwa kwa vitabu hivi, sayari nyingine hazikujulikana na hazikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watu. Hii inaonyesha kwamba vitabu hivi vilikuwa ni tafakuri ya maarifa na imani za watu wa wakati huo, badala ya kuwa na ufunuo wa kweli kutoka kwa nguvu za juu zinazodaiwa kuwa na maarifa yote.

Zaidi ya hayo, ukweli kwamba vitabu vya dini havijataja sayari nyingine unazua maswali kuhusu uhalali wa madai yao ya kiroho na kiufunuo. Kama kweli vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa kwa mwongozo wa nguvu za juu, ni kwa nini hazikuweka maarifa ya msingi kuhusu ulimwengu unaotuzunguka? Hii inaongeza wasiwasi kwamba dini zinaweza kuwa zimeundwa ili kudhibiti na kuongoza jamii, badala ya kutoa maarifa ya kweli na sahihi.

Kwa mtazamo wa kisayansi, maendeleo mengi yamefanywa tangu wakati wa kuandikwa kwa vitabu vya dini. Sayari kama Mars, Jupiter, na Saturn zimegunduliwa, na tumeweza hata kutuma vyombo vya anga kwenye baadhi ya sayari hizi. Hii inaonyesha kwamba maarifa ya kisayansi yanabadilika na kupanuka, wakati maarifa ya kidini yamebaki kuwa yale yale kwa maelfu ya miaka.

Hitimisho ni kwamba, hoja ya kwanini vitabu vya dini havijataja sayari nyingine zaidi ya Dunia inaweza kuonekana kama ushahidi kwamba dini ni utapeli. Inaonyesha kwamba vitabu hivi ni bidhaa za maarifa ya wakati wao, na si ufunuo wa kweli kutoka kwa nguvu za juu zinazodaiwa kuwa na maarifa yote.
Dini haijasema kwamba kitabu ndio mwisho wa maarifa. Wakatoliki tunaamini katika sayansi na ndio maana utagundua kuwa big bang theory ni padri aligundua, crater kibao za mwezini zina majina ya mapadri. Don't get it twisted. Dini ni lazima. Ni hulka ya Kila mwanadamu kutafuta a higher being
 
Alijitoa nafsi na uhai kuupigania,kuulinda na kuutetea uislamu. Kupitia yeye leo tumepewa Tawfiq za kutosha. Tuna uhakika wa jannah na firdaus.

Allah azidi kumfanyia wepes na aendelee kumpa qauli thabeet kipenzi chetu cha dhati Imaam Hussein Ibn Ali A.S.

Kwenye picha hapo chini kipenzi chetu cha dhati Imaam akimuaga kwa mara ya mwisho kabla ya umauti mke wake wa mwisho Shaharbanu bint Yezdegerd ni mama ya Imam Ali Al-Sajjad, peace be upon him.

View attachment 3063963

adriz Malaria 2 Code 255 Titicomb ephen_ dronedrake Yazidi Salim
si tumekubaliana picha ni haramu sisi timu kobazi?
 
Dini haijasema kwamba kitabu ndio mwisho wa maarifa. Wakatoliki tunaamini katika sayansi na ndio maana utagundua kuwa big bang theory ni padri aligundua, crater kibao za mwezini zina majina ya mapadri. Don't get it twisted. Dini ni lazima. Ni hulka ya Kila mwanadamu kutafuta a higher being
Hata Galileo alikuwa Mkatoliki.
 
Back
Top Bottom