zawadi special
JF-Expert Member
- Sep 30, 2026
- 211
- 247
Huwezi kubali ukweli,ccm kwa sasa hivi imepoteza imani ya watu wengi sana.ni ukweli mchungu ambao viongozi wengi wa chama tawala hawapendi kuusikia.Hata vikifutwa ni sawa tu maana hata ujio wao ulikuwa wa kulazimisha tu baada ya 80% ya wananchi kuvikataa kwenye ile white paper. Vyama vyenyewe havina sera mbadala zaidi ya kuikumbusha CCM na serikali kuhusu orodha ya mambo ambayo hayajafanyiwa kazi bado.
Asikwambie tu, kama wananchi wangekuwa hawaipendi CCM kwelikweli hakuna mtu angeweza kuiba kura zao. Hakuna mtu anaeweza kuiba kura za wananchi, ukiona mtu anasema zetu zinaibiwa ujue zilikuwa ni chache sana zinazoibika. Hivyohivyo, ukiona maandamano yamezimwa kama kibatali ujue walikuwa wakora tu hao, sio wananchi wenyewe kabisa.
Hata maoni mengi mitandaoni,unaona jinsi ambavyo hawaisapoti ccm,ni wachache sana wanaoisapoti ccm tena kwa maslahi binafsi.