Tafadhali ndugu naomba tupe somo hapo kwenye Nyerere kupinduliwa sisi wapenzi watazamaji
Nyerere baada ya nchi kuwa rais 1962 alishiriki chaguzi mbili tu za kidemokrasia 1962 na 1965.
Baada ya hapo alifuta vyama vya siasa na kuibakiza TANU kama chama pekee halali na chenye kuruhusiwa kufanya siasa.
Miaka ya 1960 & 1970 baada ya safari zake kwenda nchi za kijamaa kujifunza na kuomba misaada alijikuta anaingia kwenye sera za ujamaa hapo ndio aliaanza kutofautiana na viongozi wengine wa chama na hata raia.
Mfano wa sera ya kuanzishwa vijiji vya ujamaa ni watu kulazimishwa kutoka maeneo yao wanayoishi kwenda kukusanywa eneo moja kwa amri ya rais.
Nyerere alijitengenezea sheria ya preventive detention act kupitia sheria hii rais aliweza kuamuru mtu yoyote kuwekwa kizuizini mpaka pale atakapoamua aachiwe kupitia sheria hii tulipotezan watu wengi tu waliofichwa nyumba za siri kwa miaka mingi bila kujulikana wako wapi na hata kutofikishwa mahakamani kwa sababu hakukua na kosa wala sababu bali utashi wa Nyerere tu.
Jaribio la kwanza lilitokana na mambo wanajeshi wazawa kutopata maslahi sawa kijeshi , lilizimwa na jeshi la Uingereza na ndio ikaundwa JWTZ upya 1964.
Jaribio la pili kubwa ni wale wanajeshi na raia 1983 ambapo ilitokana na ukata na mdororo wa kiuchumi kwenye nchi baada ya vita ya Uganda 1979 , bidhaa ziliadimika na hata zikipatikana ilikua kwa mgao na kuporomoka kwa thamani ya shilingi na uchumi vilichangia huku Nyerere alipokua akishauriwa kuachana na sera za ujamaa zilizofeli yeye aliendelea kushikilia misimamo yake na aliyejaribu kumpinga aliwekwa kizuizini na hakukuwepo na uwanja wa mabadiliko maana hakukua na demokrasia wala uchaguzi ambao ungeleta mawazo mbadala maana chama kilichokuwepo na kuruhusiwa kufanya siasa ni CCM na yoyote ili upate nafasi hata chuo kikuu lazima upate kadi ya CCM.
Nimejaribu kueleza kwa ufupi athari na majaribio ya mapinduzi siku zote ni kutokana na kuminya demokrasia na uhuru wa mawazo mapya na kinzani hali ambayo hufanya watu kutaka kutumia njia nyingine kuingiza serikali mpya madarakani .