Kwani KANU walishindwaje uchaguzi 2002,?
KANU ndio ilikua kama CCM imeshika dola kila mkenya alilazimishwa kusema baba na mama yake ni KANU na kuimbishwa KANU JUU NYAYO JUU JUU KABISA.
Moi hakuwa anaitwa rais Moi au mheshimiwa Moi bali aliitwa Mtukufu Rais Moi.
Moi alikua na machawa hata sidhani kama Samuya amemkaribia, ndio maana wakenya wanatuona tunaishi 2026 maisha waliyoishi miaka ya 1980 hadi 1990.
KANU licha ya kuwa na dola , polisi, usalama wa taifa na jeshi chini ya miliki yao chaguo na mrithi wa Moi , Uhuru Kenyatta alishindwa uchaguzi mapema tu na Kibaki ambaye hata wakati huo alikua uhamishoni kwa matibabu baada ya ajali , kwa ufupi wakenya walichagua mtu ambaye hawakujali atarudi akiwa hai au mlemavu ndio maana Kibaki aliapishwa kwenye kiti maalum cha walemavu wa viungo.
Muda wa mabadiliko ukifika mazezeta kama wewe hamna tofauti na yule mama aliyekua akifanya kazi ikulu anaitwa Saly Koagei alilia sana siku Moi anaondoka ikulu maana hakuamini amekabidhi madaraka kwa chaguo la wananchi alitegemea angetumia jeshi na polisi kimabavu kuendelea kutawala.
Hii hapa ni video ya mgombea wa KANU , Uhuru Kenyatta akikubali kushindwa uchaguzi hata kabla tume haijatoa matokeo ya mwisho kumtangaza Kibaki kuwa mshindi na chaguo la wakenya na kuhitimisha miaka 39 ya utawala wa KANU.
View: https://youtube.com/shorts/yc6xgq92hjY?si=44CvMZB1aHgtZ6CM
Wajinga kama nyie ni jukumu langu kuwakumbusha kwamba kuna siku CCM itatoka madarakani msijisahau na kujiona mnayo hatimiliki kuongoza nchi.