Tz tuko watu 65,000 000, Kwahiyo wewe unadhani walipiga kura watu wangapi? Mimi hapa nilipiga kula kwenye mji ambao vurugu zilitokea kubwa tu pamoja na wale mliowakata vidole vyenye wino. Sasa kama mnabisha kuwa watu hawakupiga kura hao mliokata vidole vyenye wino mliwapata wapi?. Watu wengi wanaishi kwenye Mikoani, wilayani, tarafani, kwenye kata, vijiji na mitaani/vijijini. Nipe takwimu kuhusu vurugu zenu zile za mapinduzi zimetokea kwenye majiji mangapi, mikoa mingapi, wilaya ngapi, tarafa, kata, vijiji na vitongoji vingapi nchini?. Wewe na wenzio hamna maarifa ya kufanya calculation, analysisi, na evaluation, ndiyo maana mlishindwa kwenye jaribio lile, wananchi waliwagomea, hawakushiriki kwenye upuuzi wenu sasa mnahaha namna ya kuimaliza movie yenu iliyodunda sokoni. Na kumbuka kuwa hakuna movie inaisha kwa uhalifu na wahalifu kushinda.
Hawakutangaza matokeo ya uongozi kwakuwa watu walipiga kura kwenye vitongoji, motaa, vijiji, kata, tarafa, wilaya, na mikoa. Hata miji iliyokumbwa na vurugu watu walipiga kura kwelikweli ndiyo maana mkapata kirahisi mitaani watu wengi wa kukata vidole vyenye wino wa kupigia kuonyesha walipiga kura wengi sana.
Mtu kama wewe huwezi kutetea hoja yako kwanini unasema watu hawakupiga kura lakini hapohapo kuna watu mliwakata vidole vyenye wino. Kwahiyo huo wino walijipaka wenyewe majumbani kama hina?