Kwanini vyama vya upinzani havishindi, na hata vikishinda havishindi?

Huwezi kubali ukweli,ccm kwa sasa hivi imepoteza imani ya watu wengi sana.ni ukweli mchungu ambao viongozi wengi wa chama tawala hawapendi kuusikia.


Hata maoni mengi mitandaoni,unaona jinsi ambavyo hawaisapoti ccm,ni wachache sana wanaoisapoti ccm tena kwa maslahi binafsi.
 
Mimi ni kati ya wapenda vyama vingi kwakuwa najua faida yake kwa maisha ya mtu mmojammoja. Lakini sisi hapa hatuna upinzani wa maana bado. Tuna watu wanaoweza kutukana na kukejeli CCM na viongozi kwa kivuli cha upinzani.

CCM walijaribu kutaka juandika katiba mpya inayokidhi mazingira ya sasa lakini ikafikia UKAWA wakaikwamisha eti wanataka lazima Tanganyika ifufuliwe hadi mchakato ukafa kifo cha mende mpaka leo. Ilikuwa katiba yenye kila kitu cha vyama vingi isipokuwa aina ya Muungano wa serikali 2. Tulipoteza fedha nyingi kwa katiba ambayo haikupatikana. Eti tupoteze ela nyingine kuandika Katiba ambayo itavunjikia palepale ilipovunjikia ile nyingine.
 
Hata kule Libya kuna watu walidhani Gadafi hafai tena lakin sasa hivi wanajiona walikosea sana. Sisi hapa hatusubiri tufike walikofika Libya.
 
Wasiojua hawa hapa

View: https://www.youtube.com/live/pSumg8yOqMk?si=y7t86iVouVxu2peN
 
Tupia takwimu kuhusu hilo. Kuna vyama ambavyo wafuasi wake wengi ni wabwia unga na wavuta bhangi. Hawapigi kura wala kusikiliza sera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…