Uchaguzi 2020 Kwanini Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vimeanguka vibaya sana katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani

Uchaguzi huu umedhulumiwa.Hilo liko wazi kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na wewe.Baada ya CCM kulawiti uchaguzi huu jiandae kwa wananchi wote kuanza kulawitiwa ikiwa ni pamoja na wana CCM wote.Kwenye hilo hakutakuwa na ubaguzi.Shetani(dikteta) huwa hana rafiki.Kuzimwa kwa internet/mitandao ya kijamii ni manyunyu tu,the worst is yet to come!Usifikiri kuwa upo salama kwa sababu upo CCM.

Stephano Mgendanyi haupo salama wewe wala familia yako wala ndugu zako wala marafiki zako.Njia pekee ya wewe kuwa salama ni kusimamia haki,kupinga dhuluma hii na kuwa upande wa wale wote wanaopinga ulawiti huu wa demokrasia Tanzania uliofanywa na CCM.
 
Chadema ni lazima ife
IMG_20201030_111711.jpg
 
Uko wapi nikupitie twende barabarani?
Uchaguzi huu umedhulumiwa.Hilo liko wazi kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na wewe.Baada ya CCM kulawiti uchaguzi huu jiandae kwa wananchi wote kuanza kulawitiwa ikiwa ni pamoja na wana CCM wote.Kwenye hilo hakutakuwa na ubaguzi.Shetani(dikteta) huwa hana rafiki.Kuzimwa kwa internet/mitandao ya kijamii ni manyunyu tu,the worst is yet to come!Usifikiri kuwa upo salama kwa sababu upo CCM.

Stephano Mgendanyi haupo salama wewe wala familia yako wala ndugu zako wala marafiki zako.Njia pekee ya wewe kuwa salama ni kusimamia haki,kupinga dhuluma hii na kuwa upande wa wale wote wanaopinga ulawiti huu wa demokrasia Tanzania uliofanywa na CCM.
 
kama hawana sera mbovu kwanini imebidi mtumie mabeki ya kura feki ili kushinda??
Hamna mabegi feki ya kura mkuu, uchaguzi huu ulikuwa wa wazi kabisa angalia tangu kipindi Cha kampeni ccm walikuwa wamepania sana walifanya kampeni kwa kishindo, magufuri alikuwa anatembea na gari percent kubwa ya wilaya kapita na watu walikuwa wengi, siasa ni sayansi. Wakati ccm wanaangaika na wapiga kura, cdm na atc wanapambana na membe
 
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.
Una mahaba binafsi na CCM ila ukweli unaujua. Umetumia muda wako kuandika waraka mrefu ukijizungumzia wewe mwenyewe ukirefer watanzania.

Sisi tulio huku kwenye field ndo tunajua uhalisia jinsi mambo yalivyoenda, naomba niishia hapa.
 
Hamna mabegi feki ya kura mkuu, uchaguzi huu ulikuwa wa wazi kabisa angalia tangu kipindi Cha kampeni ccm walikuwa wamepania sana walifanya kampeni kwa kishindo, magufuri alikuwa anatembea na gari percent kubwa ya wilaya kapita na watu walikuwa wengi, siasa ni sayansi. Wakati ccm wanaangaika na wapiga kura, cdm na atc wanapambana na membe
Siku zote mnajitia upofu na ukiziwi, sikuwahi kuamini kama kura huwa zinaibwa na CCM. Ila uchauguzi huu nimejionea kwa macho yangu.
 
Sehemu gani umeona? Au zile karatasi walizokuwa wanazichoma Moto kawe.
 
Nikulipe mshahara! Nikujazie mafuta ya gari! Halafu umtangaze mpinzani! Hii ndiyo siri ya mafanikio. Huku Neccm na policcm wakitimiza wajibu wao ipasavyo!

Vyombo vya habari na NGO's kupigwa mkwara mzito iwapo watawapa nafasi wapinzani kufanya siasa, nk.
Huu ndio msingi wa haya yoote tunayoyaona leo, mleta mada ameamua kufurahisha watawala (mabwana) zake tu!
 
Sehemu gani umeona? Au zile karatasi walizokuwa wanazichoma Moto kawe
Mengine siwezi kusema hapa, ila nimeshuhudia mengi uchaguzi huu na roho inaniuma sana kwa yote yanayotendeka na chama changu pendwa cha CCM.
 
Kwanini upinzani umeanguka vibaya:

1) Hakuna Mtanzania yeyote anayeweza kuchagua mbunge ambaye anashauri mashirika ya fedha na wadau wa maendeleo wasiipe fedha Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa nchi yetu, hili liwe funzo watu wabishane kwa hoja lakini si kuchoma nyumba tunayoishi sote.

2) Hakuna Mtanzania anayeweza kuchagua mbunge ambaye hadi leo anaamini Corona ipo na akili zake ni kufanya lockdown, nasema Watanzania hawako tayari kwa hilo kabisa.

3) Hakuna Mtanzania anayeweza kukipigia kura chama kilichojipambanua wazi kwamba kitaweka rehani rasilimari za nchi yetu kama mafuta, madini, gesi na mbuga ili kuweza kukopa fedha nje kwa ajili ya kuleta maendeleo hapa nchini, watu wanaogopa kuweka rehani nyumba zao sembuse mali za nchi, hii ni sera mbovu sana kuwahi kutokea.

4) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukubali kukipigia chama kinachopanga kubinafsisha miradi ya kimkakati kama Bwawa la Umeme, SGR inayoendelea kujengwa na kuwapa watu binafsi ambao ni wao wenyewe, tumeshatoka huko na hatutaki kurudi tena kwenye ujinga huo. Being there done that no turning back.

5) Hakuna Mtanzania ambaye anaweza kuchagua chama kinachotaka kuzidi kufukarisha maskini kwa kurasimisha madalali kama kangomba, chama cha ACT kiliifanya hii kuwa sera yao kuu kwenye uchaguzi huu, na wananchi wameweza kuwajibu vizuri.

6) Wananchi wanapenda viongozi wenye hofu ya Mungu sio wale viongozi wanaobeza kumtegemea Mungu kama Tundu Lissu alivyokuwa anajidai kutumia science ya kuiga kuthibiti Corona huku akikejeri wito wa maombi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli, akidai Mungu yuko busy hawezi dili na upuuzi huo. Bado aliacha kuvaa barakoa pamoja na matusi yake yote na kukusanya watu bila kujali taratibu za kujikinga na Corona.

7) Hakuna Mtanzania anayeweza kumchagua mbunge ambae anapinga na hana wazo la kuwajengea Wananchi Hospitali, Bandari, Meli, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Shule bure, na mengine kama hayo, hakuna kabisa. Hivi wao wanaviita ni vitu na si maendeleo ya watu kwahiyo kwao havina maana wakati wananchi wanavitaka.

8) Wananchi wanapenda vitu vinavyowatatiza viongelewe na vipewe suluhu, sasa wapinzani wanapoongelea kuwapa wananchi uhuru, sera ngumu sana kueleweka kwasababu watu wako huru unawezaje kuwaahidi uhuru, uhuru upi wa kutukana matusi ama upi, kwahiyo hapa upinzani hawakuwa na agenda ya msingi na walipoteza muda mwingi kulihubiri hili kumbe ni tatizo lililopo vichwani mwao tu na wananchi wameshindwa kuwaelewa.

9) Kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya kuhubiri ilani, mgombea wa CCM alikuwa akifika sehemu anakuwa anayajua matatizo halisi ya eneo husika, kama ni maji, hospitali, uhitaji wa mji, mambo ya ardhi n.k na amekuwa akiyaongelea hayo matatizo halisi wakati Tundu Lissu ataanza kuongelea uhuru wakati wananchi wa eneo husika wanahitaji Hospital ama shule ama maji, ni ngumu kuchagulika ni ngumu sana. Tunawachagua wanaoyajua matatizo yetu halisi kabisa si matatizo yao kuyafanya ni ya kwetu.

10) Mimi kutomchagua Lissu, Mbowe, Sugu, Msigwa ama Lema hakunisumbui chochote kwa sababu kwanza hawana mahusiano mazuri na serikali, hawawezi kuongea na Rais kwa maana hiyo hawawezi lobby matatizo ya jimbo letu yatatuliwe, kwahiyo ntajisikia vizuri nikiwa na mbunge ambaye ana access na waziri husika na hata Rais inapobidi si mtu ambaye anapayuka na kubwabwaja bila mpango wowote, so napenda nipate mbunge mwenye mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ili matatizo yetu yatatuliwe haraka.

Wenu katika ujenzi wa nchi.

Mwanakijiji Mpenda Nchi.
Hao wamechaguliwa na NECCCM, POLICCM, nk.. siyo wananchi
 
Vimeanguka kwasababu tume ya uchaguzi ya Tanzania si tume huru Bali Ni mawakala wa CCM. Kwahiyo walihakikisha wanaina kura kwa namna yoyote ile. Upinzani ulishanda zaidi ya uchaguzi mwingine wiwote uliowahifanyika nchini tangu vyama vingi vianze.
CCM ingekuwa inakubalika kwa jinsi hii mnavyojaribu kutuaminisha, msingekuwa na sababu ya kuwatumia.

1. Tume kutunga kanuni za kishenzi za kuwalinda.
2. Tume kuwapendelea CCM na kuwaengua wavombea wa upinzani kwa kiwangi kill.
3. Tume inaona kasoro zinazohusu upinzani tu, ccm hawafanyi makosa.
4. Police wanakandamiza wapinzani na kulinda CCM.
6. Police badala ya kulinda amani wanasaidia kuiba kura.
7. Mawakala wa upinzani wanazuiliwa kusimamia kura zao.
8. Mnaingiza kura feki kwenye mzunguko.

Kama mnakubalika si mngeacha uchaguzi ufanyike kwa Uhuru muone Ni kitu gani kingetokea? Halafu eti mnajisifu mmeshinda u haguzi wakati mnajua mumeiba kura.
 
Nikulipe mshahara! Nikujazie mafuta ya gari! Halafu umtangaze mpinzani! Hii ndiyo siri ya mafanikio. Huku Neccm na policcm wakitimiza wajibu wao ipasavyo!

Vyombo vya habari na NGO's kupigwa mkwara mzito iwapo watawapa nafasi wapinzani kufanya siasa, nk.
Swali la ziada "Kwanini matangazo ya matokeo YA KURA YANASHABIHIANA MIKOA TOFAUTI?"
Mpaka imeitwa saresare maua!

Walipoambiwa "msinichanganyie betri na gunzi..."maccm ina maana hayakujua maana ya hayo maagizo.
 
Vimeanguka kwasababu tume ya uchaguzi ya Tanzania si tume huru Bali Ni mawakala wa CCM. Kwahiyo walihakikisha wanaina kura kwa namna yoyote ile. Upinzani ulishanda zaidi ya uchaguzi mwingine wiwote uliowahifanyika nchini tangu vyama vingi vianze.
CCM ingekuwa inakubalika kwa jinsi hii mnavyojaribu kutuaminisha, msingekuwa na sababu ya kuwatumia
1. Tume kutunga kanuni za kishenzi za kuwalinda.
2. Tume kuwapendelea CCM na kuwaengua wavombea wa upinzani kwa kiwangi kill.
3. Tume inaona kasoro zinazohusu upinzani tu, ccm hawafanyi makosa.
4. Police wanakandamiza wapinzani na kulinda CCM.
6. Police badala ya kulinda amani wanasaidia kuiba kura.
7. Mawakala wa upinzani wanazuiliwa kusimamia kura zao.
8. Mnaingiza kura feki kwenye mzunguko.

Kama mnakubalika si mngeacha uchaguzi ufanyike kwa Uhuru muone Ni kitu gani kingetokea? Halafu eti mnajisifu mmeshinda u haguzi wakati mnajua mumeiba kura.
Kama kweli wanajiamini zipigwe kura za mlolongo mtaani wajionee matokeo.
 
Naona mna halalisha UJAMBAZI.
Sasa Kari ya ccm na chadema ni nani aliyechokwa na wananchi?.
Mnaposema upinzani wamechokwa na wananchi lakini mnatumia wizi kwa kuwa kuwaondoa si Sawaaa.
Ilitakiwa wananchi wenyewe wapige kura.
Bado hoja zenu hazina mashiko.

Screenshot_20201028-191013.jpg
Screenshot_20201029-061237.jpg
 
Point is wizi wa hali ya juu !
Mtalipa dhuluma hizi, hata kwa pacemaker kuacha kufanya kazi !
Ubunge CCM

QUOTE="Mr_X, post: 37168685, member: 321847"]
Tatzo lao walikuwa na fikra kwamba Watanzania bado wajinga vilevile Kila kitu kupinga kisa wao wapinzani, washaonyeshwa makali sasa & hope 2025 watajipanga kwa sera nzuri.
[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom