Kwanini Waafrika hatulimi matunda yetu ya asili?

Kwanini Waafrika hatulimi matunda yetu ya asili?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Katika matunda ya asili ya Afrika ni matikiti tu ndiyo yanalimwa sana. Mengine yameachwa maporini na yanazidi kupotea. Kwanini Afrika hatulimi matunda yetu ya asili? Ni matunda gani ya asili yanapatikana kwenu na ungependa kuona yanalimwa?

1714659045365.jpeg
 
Katika matunda ya asili ya Afrika ni matikiti tu ndiyo yanalimwa sana. Mengine yameachwa maporini na yanazidi kupotea. Kwa nini Afrika hatulimi matunda yetu ya asili? Ni matunda gani ya asili yanapatikana kwenu na ungependa kuona yanalimwa?

View attachment 2979094
Haya sio ya asili, yenyewe ni seedless watermelons; modified.
 
Orodhesha hayo matunda ya asili kwanza labda naweza kujipatia fursa hapa 🤒😎
 
Haya sio ya asili, yenyewe ni seedless watermelons; modified.
Ila Kwasasa Kuna Neno Wanatumia Sana Hawa Wataalam Wa Kilimo
Hasa Wanaposema Mbegu Zilizoboreshwa Huleta Mazao Mengi Kwa Muda Mfupi Hapo Ndiyo Mbegu Asili Zinapotea/Zimepotea Kwa Kasi Sana.
Nadhani Masuala Ya GMO Kutoka Kwa Mabeberu Hatutaweza Kuzikwepa
 
Mara nyingi, matunda ya asili yanaweza kuwa magumu kupatikana katika maeneo fulani au msimu fulani wa mwaka na yanaweza kuwa ghali mno kulingana na eneo na msimu. Bei ya juu inaweza kufanya iwe vigumu kwa watu wengi kuwa na upatikanaji wa kutosha wa matunda haya katika lishe yao ya kila siku.
Katika baadhi ya maeneo, watu hawana uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa matunda ya asili katika lishe yao.

Katika baadhi ya maeneo, kuna hatari ya matunda ya asili kuambukizwa na magonjwa au viuatilifu vilivyozidi kiasi hata hivyo mabadiliko ya maisha ya kisasa yanaweza kusababisha watu kugeukia vyakula vya kusindika au visivyo vya asili, kama vile vyakula vyenye sukari nyingi au vyakula vyenye mafuta mengi.
 
Back
Top Bottom