Sikatai ila sio watumwa na fikra mbovu za ubaguzi wa kidini km sisi wapogolo ww angalia wahindi wana dini yao ama wachina wana dini yao hawataki na hawakubagui kwa ajiri ya dini na wanapambana na elimu sasa wako juuu.
Kwa hiyo waafrika wana dini ipi inayofanana.?
Mana kila kabila lilikua na dini yake na mila zake.
Na kabla ya dini za leo waafrika walibaguana sana.
Walidhulumiana sana.
Waliibiana sana.Mpaka leo Wafugaji na wakulima hawaelewani . Mpaka leo wafugaji wanaibiana sana.
Wazungu walikua hivyo hivyo kwa karne nyingi lakini waliketi chini na kurafakari juu ya haki wao kwa wao baada ya kutandikana sana.
Waafrika tuna ubinafsi mkubwa sana.
Dini sio tatizo tatizo ni ule ubinafsi tulio nao. Watu wana roho mbaya Mpaka wanatamani waende peke yao huko Mbinguni. Yaani MTU ameshasikia kuwa Mbinguni ni mahali pazuri anaanza kupigania nafasi ya huko kwa kuua wengine wakati hata hajawahi kufika.
Madaraka watu wanauana kuyatafuta kwa ajili ya kupata maisha mazuri.
Kumbuka Alfonce Mawazo aliuawa na makada wa CCM kwa sababu ya Ubunge. Ubunge ungekua hauna chochote watu wasingeua wengine kwa sababu ya Ubunge.
Waafrika karne hii bado wanauana ndugu kwa sababu ya vyama vya siasa ambavyo havina nafsi wala roho. Ni jina tu KANU. MTU unamuua mwenzako au unamfunga gerezani kwa kesi za uongo na kuumiza familia yake kwa sababu ya neno KANU au CCM. Wenzetu walishaondoka kwenye huo ujinga wa imani Kali za kisiasa kwa watawala ndio maana wanawaza maendeleo zaidi.
Dini ni imani na ni asili ya binadam wa kila taifa. Dini zetu hazikujipambanua juu ya kesho ya mwanadam ndio maana hazikuweza kufua dafu mbele ya dini za Mashariki ya Kati.
Warumi na wagiriki na wamisri ni jamii zilizokuwa zimeendelea na kuelimika sana na zilikua na dini zao lakini walizipima dini za mashariki ya Kati na kuzikubali mana zilizungumzia haki.
Huwezi kuendelea kama hauna jamii inayotenda haki.
Haki ni msingi wa maendeleo kwenye jamii.
Ukipita kwenye shule za serikali baada ya Uhuru utaona vichekesho vitupu. Shule imejengwa ina mwaka mmoja ina nyufa kila mahali. Lakini shule iliyojengwa miaka mia moja iliyopita ipo imara. Ina vyoo vya maji ,n.k. Hapo mzungu na mwafrika anajipambanua wazi kuwa mwafrika ana ubinafsi na roho mbaya.
Dini inakatazo hayo yote.
Watawala wanatumia muda mwingi kulimbukiza Mali kwa ajili ya familia zao bila kujali kundi kubwa la waafrika maskini wanaozaliwa na watakaohitaji vitu kama Afya, makazi,elimu na ajira. Ukiwauliza wanakuambia wazungu wanatuibia. Mtu huyo huyo ni kada wa Chama tawala. Alikua meneja wa chama cha ushirika akaiba na kujenga hoteli. Kwa sababu ni mtandao wa kichama ,akaenda akagombea udiwani akawa Meya au Mwenyekiti wa halmashauri ,akawa anashirikiana na Mkurugenzi ambaye ni kada wa chama wakawa wanajipa tenda za kumwaga matope barabarani kwa kutumia kampuni zao za ujenzi wa barabara . Kila Mwaka wanamwaga vifusi na barabara inaharibika mana wamenunua magreda kwa kujua kuwa barabara wataijenga kwa kiwango duni ili kazi ya kuliibia taifa iendelee. Mzunguko unakua hivyo. Diwani anagombea Ubunge anapata kwa sababu ya rushwa na kupendelewa.
Baadae anakua waziri wa Elimu. Anashirikiana na wahindi kuweka mashine za kuchapisha vitabu.
Anabadili mitaala kila mwaka ili auzie serikali vitabu. Matokeo yake wazazi kila mwaka wananunua vitabu mana vya mwaka jana havimsaidii tena mwanafunzi anayeingia darasa hilo. Waziri huyo anasomesha watoto wake nje. Anatumia fedha nyingi kulipoa ada huko ulaya. Fedha za maskini zinapotelea ulaya.
Mtoto wake anamaliza shule ulaya anakuja kuwa Mkurugenzi wa Ewura. Kampuni inayowanyonya waafrika bila kuzalisha chochote.
Tulitegemea afanye kazi huko Ulaya atuibie teknolojia lakini wapi. Anakuja anaandaliwa kuwa mbunge au mkuu wa Wilaya.
Mzunguko wa kundi la watu wanaonufaika na umaskini na elimu duni ya mwafrika linazidi kuwa kubwa.
Wanaonufaika na umaskini na elimu duni ya mwafrika ni watawala wa Wafrika zaidi kuliko wazungu.
Wazungu watabaki kuwa juu kwa sababu ya roho mbaya za waafrika.
Mfano tu miamala kwenye simu. Mzungu amegundua teknolojia ya mawasiliano lakini waafrika wanaitumia kukomoana na kuchaji pesa nyingi kuliko mgunduzi.
Gari Japan ni bei rahisi kuliko kodi wanayokamua waafrika kwa waafrika wenzao.
Dawa zinatoka India kwa bei Rahisi sana. Lakini zikishakanyaga ardhi ya Afrika zinauzwa ghali sana Mara tatu ya bei yake.Asiyeweza kununua afe.
Halafu wanapumbaza watu kwa kusema Mzungu ndiye adui.
Kubadilika ni kuondokana na mawazo ya kijinga ya kumlaumu Mzungu asiyepo kwenye Hazina wala picha ya fedha za mataifa ya Afrika.
Leo Wasomali na Waethiopia wanataka kwenye zao Afrika ya kusini kutafuta maisha ndani ya Afrika lakini wanakamatwa kama wahujumu uchumi na kugungwa na waafrika wenzao.
Mwafrika analima bangi yake kama zao la asili na lina soko ulaya lakini shamba linafyekwa na mwafrika mwenzake.
Unataka Utajiri gani wa asili wakati uliopo kuna sheria kandamizi kila kona na zimewekwa na waafrika wenzetu tuliowapa madaraka wakageuka kuwa wakoloni.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app