ANKO JEI
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,302
- 2,462
Wengi hapa tatizo sio ukubwa wa mshahara wala ughali wa maisha.Ni akili haioni uwezekano wa kusave, ndio mana ikija mada kama hii mtu anaona anatukanwa, mana hawezi save hata buku.
Mimi nashauri mtu ukitaka kusave, kwanza amua kusave, kisha kaa chini angalia ni gharama gani isiyo ya muhimu kwenye maisha yako.
Inaweza kua ya jambo dogo sana, mfano kama una mazoea ya kunywa soda 2 kila siku, punguza moja weka 500 pembeni.
Kama umezoea kupanda bodaboda na umbali si mrefu, jaribu kutembea kama mazoezi pia unasave hilo Buku au buku mbili.
Utasema, Jero na buku zitanipeleka wapi? Lengo hapa sio amount unayo tunza, ni kujenga Tabia ya kusave.
Tabia ikishajengeka, huku unazidi kukagua ni matumizi gani unayoweza punguza, kiwango cha kusave kinaongezeka.
Nimeishi na watumishi wengi, ndugu na hata marafiki, ile wiki akipokea mshahara matumizi yake unaweza hadi shangaa, ni kama sherehe.
Hela ikishapungua na mwezi upo kati kati ndo bajeti kali zinaanza.
Anza kidogo kidogo utafika, waswahili wanasema Haba na haba hujaza kibaba.
Kila la kheri.