Nimejaribu kufanya tathmini na nimegundua watanzania hasa hawa waajiriwa wa Serikalini hawana tamaduni za kutunza pesa, Wazungu wanaita savings.
Ni vema watanzania wengi tukaanza kupiga mfumo wa Wazungu kuwa unapopata kamshahara kako basi angalau asilimia 20 itunze, halafu ndo uanze matumizi kwa hiyo 80 iliyobaki. Hali hii ya kutotunza pesa imekuwa mbaya kiasi kwamba mtu amefanya kazi miaka 10 lakini akisimamishwa kazi Mwezi mmoja anageuka kuwa omba omba, na anashindwa kuendesha familia hata kwa miezi miwili Bali ni mizinga tu.
Hali hii pia inachangiwa na ugonjwa unaoitwa spending/shopping addiction yaani ukipata pesa unakuja na kimuhemuhe Cha kuzitumia. Pia kutunza pesa kwa waajiriwa ni changamoto wengi wakisema extended family zinawanyonya sana kiasi kwamba huwezi kutunza shilingi kumi.
Wafanyabiashara Tanzania kwenye hili wanajitahidi sana, na wengi ni watunza pesa wazuri kuliko waajiriwa.
Na Hali ya uhakika wa kupata pesa kila mwisho wa Mwezi unafanya watu kubweteka.
Ukitunza pesa itakusaidia wakati wa emergency na kukuondolea aibu ya kuomba omba pindi unapopata na shida.
Mnaonaje wadau, je ni muhimu kutunza angalau asilimia 20 ya mshahara wako wa Mwezi au ni kuzitandika zote?
Wazo huenda likawa zuri lakini ujue kuwa mfumo wetu wa maisha ni tofauti na wa Wazungu.
Sisi tunaongozwa na matukio,yani,panapokuwa na tukio ndiyo tunawajibika. Kwahiyo,haijalishi kuna matukio mangapi. Huwezi kubajeti. Hapa muda si mrefu nimepigiwa simu baba mkubwa ni hoi taabani. Ana watoto wake,lakini, wamechoka. Mimi mtoto wa mdogo wake ndiyo naokoa jahazi hapo. Huku nina watoto wa dada ambao baba zao hawajawahi kujitokeza ninawasomesha.
Aidha, nikija afya yangu mwenyewe. Bima ya afya haitoi huduma kwa 💯. Nikiugua hapa gonjwa kuubwa, mshahara huohuo uniuguze.
Hapo mke wangu ni mama wa nyumbani, zigo la home mke na watoto ni mimi.
Mzungu anafanikiwa kwakuwa wao mfumo wao wa maisha ni nyoofu, linear. Mzungu anaweza kujua katika miaka mitano ijayo ,ataishi na watu wangapi. Anajua kabisa mtoto wake X ,ikifika mwaka Y anaondoka home. Sisi fanya tathmini tu, kwa mfano, hili kundi limemaliza vyuo mtaani wanaishi wapi.
Haya ni machache tu, hiyo akiba tunaweka haikai. Ndiyo maana baadhi wanakuwa wabadhirifu. Pesa ya mbongo haiwekeki kwenye bajeti. Wengi wakipata fursa wanajilimbikizia mali ili kukabiliana na majanga yasiyotabirika.Sisi unaweza kuwa mbunge au waziri na bado ukafa masikini. Maana jamii nzima inakutazama wewe.
Ungeshauri tujiongeze labda, kuwa na vyanzo vingine vya mapato.Hii inasaidia sana.