Kwanini waajiriwa wengi hawana utamaduni wa kufanya savings nchini?

Kwanini waajiriwa wengi hawana utamaduni wa kufanya savings nchini?

Kipato Tsh 500,000. Mahitaji Tsh 700,000.
Hapo savings inatoka wapi?
Savings inaweza kupatikana iwapo baba na mama wanaoamka asubuhi kwenda kazini wanagawana majukumu... Baba akilipia umeme, mama alipie maji!
Tatizo wanawake wengi siku hizi ni goi goi. Kazi za nyumbani anatakiwa azifanye yeye. Basi kama yeye kaamua kwenda kazini kutafuta basi mama ndio alitakiwa amlipe house girl mshahara kwa kumsaidia majukumu yake lakini kinyume chake unakuta baba ndio anamlipa house girl mshahara. Huu ni unyonyaji.
Kwenye familia za kiafrika, baba ni mtu anayenyonywa sana kwa kuwa yeye ndie anayebebeshwa mzigo mkubwa wa kuendesha familia hata kama mama ana kipato kizuri unakuta contribution yake ni ndogo sana...
Ndio maana nawafurahia waarabu walioamua kuwa 'mama awe ni mtu wa kukaa nyumbani'! It saves cost.
Piga picha mtu anakaa Tegeta, ana mke anafanya kazi Posta, unakuta badala ya mke aweke mafuta kwenye gari yake kwa mshahara anaopata kazini, baba wa watu anajipiga hapo unakuta kiwese kinamgharimu laki tatu. Pia house girl anamgharimu laki.
Unaona! Kama huyu mama angekaa tu nyumbani huyu baba wa watu angeokoa Tsh laki nne! Ya mafuta na ya kumlipa house girl... Hivyo kumfanya awe na savings...
Hii kitaalamu inaitwa kufumua mshono.


Wale feminist uchwara wooote wataipita hii comment kimya kimya wakiongoza na dada yao cariha , ila subiri uone wakianza kelele zao za haki sawa.
 
Kupigia bajeti mshahara wa mwanamke huo ni upungufu wa nguvu za kiume
Kwanini ?!!


Hebu nipe sababu za msingi kabisa,

Yaan kwa mfano wewe ni mke wangu wa ndoa na wote tuna kipato, kwanini mshahara wako usipigiwe budget.
 
je ni muhimu kutunza angalau asilimia 20 ya mshahara wako wa Mwezi au ni kuzitandika zote?
Watu wengi wanashindwa kusave kwa sababu ya asilimia zinazowek2a na watoa ushauri wa saving.


Mtu anapokea mshahara 400,000 alafu anaambiwa asave 20% yaani 80000 nzima wakati huo ana majukumu kibao yanamsubiri.

Tuangale mtu kama huyu wa kipato hiko anaweza akasave asilimia tano inatosha kwa sababu hakuna akiba ndogo kamwe.

Mtu anapokea laki nne sio mbaya akaweka pembeni 20000 ambayo hatoigusa kwa lolote,lakini akiiweka 80000 akilini mwake itakuwa anasema ipo 80000 ipo 80000 ipo 80000 ipo 80000 yaani akipata shida kidogo tu anarudi kwenye 80000 anaanza kuitawanya.

aatleast ukiweka 20000 au hata 15000 inatosha sana hakuna akiba ndogo kamwe wakuu.

usifuate ushauri wa watu wanaosema weka 20% au 30% wakati hawajui unaishi vipi na unapokea pesa ngapi na una majukumu gani.

Hakikisha unaweza akiaba hata kama ni 5000 kwa mwezi hiyo ni kubwa na ni yako.

Haya mambo ya asilimia tusiyazingatie sana..
 
Fikiria mtumishi analipwa take home 500,000
Weka mchanganuo wa matumizi utakaobakisha saving
Hivi ndio watumishi wanavyofanya kamchezo ka-savings🐒
20210904_070640.jpg
 
Za kusave zitatoka Wapi Mzee?? MATAJIRI wenyewe wanafanya dili kubwa wanatajirika ukisimamisha matajiri hao ukajua mambo yao kuanzia ukwepaji kodi..kupata tenda kubwa kwa ujanja na kutotimiza hizo kazi ni wizi sana...ila sasa ukasikia mtumishi kaiba mil 50 utaona magazeti yoote yanaandika
 
Tunashukuru kwa ushauri. Je, vipi kuhusu wewe mtoa mada? Tupe uzoefu wako wa kufanya savings. Isije ikawa wewe ni miongoni mwa wale "motivational speakers/writers" ambao wamekuwa kama fashion siku hizi. Wanaongea na kuandika wasiyoyatenda.
 
Za kusave zitatoka Wapi Mzee?? MATAJIRI wenyewe wanafanya dili kubwa wanatajirika ukisimamisha matajiri hao ukajua mambo yao kuanzia ukwepaji kodi..kupata tenda kubwa kwa ujanja na kutotimiza hizo kazi ni wizi sana...ila sasa ukasikia mtumishi kaiba mil 50 utaona magazeti yoote yanaandika
Unaongelea wafanyabiashara umewasahau wanasiasa..hao ndio hatari kwa wizi na ufisadi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hatari sana...mshahara 50k matumizo 200k...unasave nini kama sio kujidanganya tu.

#MaendeleoHayanaChama

#MaendeleoHayanaChama
Na hiyo 200k ni matumizi ya kawaida bado halijaja janga ambalo linahitaji 500k ya papo kwa hapo
 
Na hiyo 200k ni matumizi ya kawaida bado halijaja janga ambalo linahitaji 500k ya papo kwa hapo
Mimi naona kusave angalau 5% ya kipato inatosha kwa mtu wa hali ya chini asijitutumue kutaka kusave 20% watakuwa wanatumia daily.

Mtu anachukua 300,000 kwa mwezi alafu asave 60000 nzima kisa tu ni 20% no asave japo 20000 kwa mwezi inatosha kwa mwaka ana 240000 ambayo ipo tu imetulia.

Watu hawajui siri moja ya saving ili uizoee basi lazima uanze na kuweka kiwango ambacho hautakiwazia hata kidogo kama sio mzoefu.

.mfano mtu Anaweza akawwa anapokea 500,000 kwa mwezi akiweka laki moja kwa mkupuo ghafla kama akiba yaani ataiwazia sana hiyo pesa na hatokaa aisahau,mwezi ujao anaweza ingine na ingine na ingine mwisho wa siku anaenda kuchukua anatumia.

Ila kwenye hiyo 500k wewe weka akiba 10000 tuu tuone kama utaiwazia kwamba inaweza kukutatulia shida yako,haitakuwa akilini mwako kabisa kwamba eti kuna pesa nimeweka akiba itanisaidia nikipata shida ,na utaoionea huruma kuitoa.

Ukiweka 10000 kila mwezi itafikia hatua utataka kuongeza utaweka 20000.

Kitu chochote ambacho hujakizoea kianze taratibu saana kwa kiwango cha hali ya chini ambacho hautaweza kuhisi kama umefanya kitu.

Hata mazoezi anza kukimbia mita 200 badala ya kuanza kukimbia 2km.

Ukianza taratibu na kudumu kidogokidogo basi unatengeneza tabia imara itakayodumu milele na milele.

"Kinachofanywa kwa mkupuo basi kitaachwa kufanywa kwa mkupuo pia"
 
Back
Top Bottom