TUMEKUSIKIA,
SASA , LETE HOJA KWA USHAHIDI WA BIBLIA AU QURAN
BWANA PAULO ANAWAAMBIA 1COR
15:14 na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana.
15:15 Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua--kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi.
15:16 Maana, ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristo hakufufuka.
15:17 Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu.
YEYE KAJITOA ANAWAAMBIA IMANI YENU , NA SIO IMANI YETU
NO CRUCIFIXION NO CRISTIANITY
Kwa uchache ni kwamba, Yesu hakusulubiwa wala hakuuawa na hivyo hakuna "kufufuka" na wanaoamini kinyume na hivi wanafuata dhana tu. Kwani Biblia inasemaje?
Mathayo anatufahamisha katika Injili yake:
"Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia, kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. (Mt. 12:38-40) (Rejea Yona 1:15 –2:1).
Kwa maelezo haya ya Yesu ni kwamba hatakufa kama vile ambavyo Yona hakufa, ila atakaa kaburini siku tatu, mchana na usiku kwa kila siku, na hivyo kusingekuwa na ufufuko. Lakini Mathayo anaeleza katika 27:45 – 28:1-6 kwamba Yesu alikufa, akazikwa kisha akafufuka. Kanisa nalo linafundisha kwamba Yesu alikufa Ijumaa jioni na akafufuka Jumapili alfajiri, yaani kukaa kaburini siku moja na nusu tu.
Bado kuna hitilafu nyingi kuhusu mwisho wa Yesu baada ya kukamatwa. Kwa mfano, Marko anasema Yesu alisulubiwa saa tatu asubuhi (Mk. 15:25) lakini Yohana anasema alisulubiwa baada ya saa sita mchana (Yn. 19:14). Luka anapingana anaposema kwamba Yesu alipaa siku ile ile aliyofufuka (Lk. 24:13-51). Lakini katika kitabu chake cha Matendo ya Mitume akaeleza kuwa alipaa siku ya arobaini baada ya kufufuka (Mdo 1:1-12).
Tatizo lenu ni kwamba mumeegemea zaidi kwenye itikadi ya Kanisa kuliko maandiko ya Biblia na hivyo kulazimika kuchagua vifungu vya Biblia vinavyohami imani yenu tu kwa vile Kanisa haliifuati Biblia yote.
Biblia ni bahari pana yenye vifungu vingi vinavyopingana na visivyofahamika asili yake.
Na Waislamu hatutilii shaka maneno ya Mwenyezi Mungu katika Qur’an Tukufu anaposema kwamba imani ya Yesu kusulubiwa msalabani na kufa ni dhana.
Tunaposema migongano kama nilivyoelezea juu kwa uchache, tunazidi tu kukumuamini Mwenyezi Mungu.
Kwani mna uhakika gani kwamba Yesu alisulubiwa msalabani (saa tatu au sita?) na kukaa kaburini siku moja na nusu tu na sio kwamba ni siku tatu mchana na usiku tena akiwa hai kama alivyowaambia Waandishi na Mafarisayo.
Licha ya hayo, hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kama Waandishi wa Injili nne walikuwa watu wa kutumainiwa na walioongozwa na Mungu. Kwa mfano, Biblia Takatifu, Agano Jipya, UBS 1990, inaeleza katika uk. 13 "utangulizi wa Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo":
Injili ya Mathayo haisemi chochote kuhusu mtungaji wake. Kadiri ya mapokeo ya zamani, Mathayo mtoza ushuru na mmoja wa Mitume kumi na wawili aliandika maneno ya Yesu katika lugha ya Kiaramu. Bahati mbaya mtungaji wa Injili yetu ya sasa aliyeandika katika lugha ya Kigiriki (ambaye habari zake maalum hatuna) aliongozwa na mawaidha ya Mathayo, mfuasi wa Yesu).
Na kuhusu Injili ya Luka tunaelezwa:
Kadiri ya mapokeo ya zamani Injili ya tatu imeandikwa na Luka aliyezaliwa Antokia akawa Daktari. Alikuwa mpagani (au wa asili ya mazingira ya Kigiriki) si Myahudi kama walivyokuwa akina Mathayo, Marko na Yohana (Uk. 84 wa Biblia hiyo hiyo).
Nayo Biblia Takatifu T.M.P. Book Department Tabora, 1967, uk, 911 inaeleza kwamba Marko hakuwa mwanafunzi wa Yesu, na Injili yake ni muhtasari wa mafundisho ya Petro. Na ama Injili ya Yohana inajishuhudia yenyewe kwamba waandishi wake ni wengi na wala hawafahamiki:
Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. (Yn. 21:24).
Na hii ikawa ndio sababu ya wasomi wa juu wa Kikristo kusema kwamba mwandishi wa Injili hii sio Yohana, huenda labda ni wanafunzi wake (Dictionery of the Bible, John Mackenzie; 1981 maelezo kuhusu Injili ya Yohana).
Kwa hiyo, mnapodai kutaka kufundisha Waislamu juu ya kifo cha Yesu inabidi mjiulize maswali kadhaa, kwamba, je, mnaifahamu Biblia yake vyema?
Mnatambua tofauti kati ya Ukristo na Biblia?
Mnaifahamu Qur’an inavyotakiwa kuifahamu? Na zaidi ya yote mnatakiwa kuacha fikra lemavu ya kutaka kujaribu kulinganisha Ukristo na Uislamu.
Napenda kuwafahamisha kwamba Waislamu hatuna lolote la kujifunza kwenu kuhusiana na somo hili, ila tu mtupe hoja kuthibitisha kwamba itikadi mnayoitetea haikujengeka juu ya dhana.
Pia kwa Waislamu kupinga kifo cha Yesu sio kumpinga Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu hajasema mahali popote kwamba Yesu kafa.
Hayo ni madai ya watu wasiofahamika (kwa wanahistoria wa Kikristo na Wakristo wenyewe) pamoja na Wapagani.
Tuzingatie tahadhari aliyoitoa Mwenyezi Mungu katika Qur’an Tukufu:
Basi adhabu kali itawathibitikia wale wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema, "hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu". (Wanasema uwongo huo) ili wachukue thamani ndogo ya kilimwengu. Basi ole wao kwa yale walivyoyaandika kwa mikono yao (wakasingizia kuwa ya Mungu). Na ole wao kwa yale wanayoyachuma. ( Qur’an Tukufu 2:79).