Najua huwezi kutoa ushahidi wa kielimu juu ya haya uyasemayo.JIHAD kwetu sisi waislamu ni ibada kama ilivyo,ibada huwa ina masharti na ina nguzo mzee.Huwezi kupigana JIHAD bila bila kuzingatia masharti na nguzo.
JIHAD ni tamko la kiarabu lanye maana ya juhudi kilugha na ibada kisheria.Jihadi imegawanyika takribani vipengele vinne kama alivyosema Imaam Ibn Qayyim al Jawz Allah amrehemu.
1.Kuna jihad nafsi hii ni kuipigania nafsi yako isitende maovu na hii ndio jihad kubwa kuliko zote.
2.Kujihadi ya kupambana na shetani,hii vita kati yako na shetani yaani kumpiga vita shetani asikushawawishi na kutenda maovu na kuacha dini ya Allah.
3.Jihadi ya kupambana na makafiri wale waliokufuru na waharibifu
4.Jihadi ya vita hii imegawanyika sehemu mbili jihadi kwa ajili ya kujilinda na uvamizi wa adui na jihadi ya kumvamia adui yako,jihadi hizi hazifanyiki mpaka zikidhi masharti.
Mengi tunayoyasikia juu ya uislamu zama hizi hasa ya hawa bokoharamu,alqaeda na mfano wao ni fitna zilizoambatana na ujinga.Na wanazuoni wa haki huwakanya wafanyavyo hivyo lakini hawasikii.Katika uislamu ni haramu kujitoa muhanga,haramu kufanya migomo,haramu kuandamana.Ukweli huu wengi hawaujui isipokuwa wale wachache waliorehemewa na Mola mlezi.