Sijui hata chama tawala wenyewe wanajisikiaje kwa jambo hili. Hivi dhamira zao haziwasuti ? Lakini wakumbuke tu kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha na mwisho wa ubaya ni aibu.Hizi ni dalili za wazi dhidi ya upinzani. Haiwezekani tangu mchakato wa uchaguzi uanze chama tawala hawajahi kufanya makosa. Tunajidanganya tu kwani wananchi sio wajinga na wanaona unyanyasaji wa wazi dhidi ya vyama vya upinzani.