'' Mtu kupata elimu sio kwa ajili ya kuuondoa umasikini bali ni kwa ajili ya kupambana na huo umasikini''...........mwl Nyerere mwisho wa kunukuu.
Wahaya shida yao wameelimika lakini hawana mbinu za kutumia kupambana na huo umasikini.
Shida yao kubwa ni majivuno na majigambo yasiyo na tija hapa ndio wachaga wanapowapiga bao maana wenzao wana vyote.
Mhaya akipanda ndege kujishaua utaona anavaa suti na tai.Mchaga anaweza panda ndege amevaa jeans
Hizi tabia za kihaya utasikia professor wa kwanza mtanzania ni mhaya lakini ukiuliza alifanya nini hakuna.
Namfagilia sana Marehemu Laurian Rugambwa ndio Kardinali wa kwanza muafrica na mtanzania alijitahidi sana kuleta elimu kwa shule ya Rugambwa na Bugando kwa wasiojua mchango wake mkubwa sana ulitokana na yeye ikajengwa Bugando japo ilikuwepo lakini inasemekana Vatican waligundua anapata U papa sasa ubaguzi wa wazungu wakaona haiwezekani ikabidi wamuambie tukujengee hospitali tujenge wapi ndio vile Bukoba ni mpakani wakaona yeye na Nyerere waijengee Mwanza yaani kurekebisha majengo ya iliyo sasa.Mungu amuweke salama huyu mzee.
Mkuu wa mkoa mmoja aliyepita wa Kagera alipata kuwapiga madongo waache uvivu unakuta mtu anafungua duka saa tano akawaambia tatizo lenu nyie kila mtu ni mwanasheria hawapendi kazi ngumu.
Dada mmoja Mhaya rafiki yangu alipata kuniambia kaka zangu tatizo lao ni wavivu sana hawapendi kufanya kazi ngumu wanapenda kazi za kwenye makaratasi tu lakini mchaga kuuza supu,nyama choma ni kitu cha kawaida kabisa na anaingiza mhaya hawezi.
Picha chini angalia ma judge Kina Nshomile na Mangi Massawe
Judge Nshomile anasubiri hadi mwisho wa mwezi alipwe milioni chache.Mangi Massawe akimaliza huyo Mbuzi alivyomuandaa analipwa lakini tano sababu ni tender za harusi.Chukulia kwa mwezi anafanya mara 10 anapata millioni 5
Tofauti ilianzia hapa