Kwanini Waislamu wengi wanaota ndoto za Yesu huko Mashariki ya Kati?

Kwanini Waislamu wengi wanaota ndoto za Yesu huko Mashariki ya Kati?

Mbona sisi wabongo hatumuoni huyo Brian Deacon kwenye ndoto zetu
Nyinyi mnayo nafasi ya kusikia Injili hapa JF, Youtube, Facebook, kwenye TV na redio. Hao hawana fursa hiyo maana Injili hairuhusiwi katika nchi hizo. Hivyo ndoto ni njia nzuri kwao ya kusikia habari za Yesu bila kizuizi.
 
Na Bibi yangu hana nafasi ya kusikia injili jf wala FB vipi na yeye
 
Na Bibi yangu hana nafasi ya kusikia injili jf wala FB vipi na yeye
Kuna mikutano ya Injili mingi sana vijijini. Isitoshe kuna wahubiri wanaopita nyumba kwa nyumba wakitangaza habari za Yesu. Kwa vyovyote vile atakuwa amesikia. Mwambie asikawie kutubu na kumwamini Yesu. Ni neema kuishi na kuufikia ubibi.
 
Tangu mwanzo, wanasema hakufa wala hakufufuka. Tena wanasema Yesu sio Mungu wakati ushahidi upo mwingi
Uislamu haumpingi Yesu na Mtume Muhammad (s.a.w) alisema:
"Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake atateremka juu yenu mwana wa Maryam kama hakimu wa haki...".
(Sahih Bukhari & Muslim)

Kwa hivyo kurudi kwa Nabii Isa(Yesu) (a.s) ni miongoni mwa alama kubwa za (Kiyama)"siku ya mwisho" na ni imani ya msingi katika itikadi ya Uislamu .
 
Kwani lini walimkataa?

Kuna waislam, sijui wanajiita nani, nimesahu dhehebu lao, wao wanasema ni waislam wanaomfuata Yesu Kristo masiha, na wanadai kuwa kuna wenzao wamekosea kupata tafsiri sahihi na Quran.

Katika mambo ya kiimani, lolote linaweza kutokea. Hao waislam tunaodhani wanamkataa Yesu Kristo kuwa masiha, mteule wake Mungu, aliyepewa mamlaka yote Duniani na mbinguni, wanaweza kugeuka na wakawa mbele ya wakristo wanaiamini wanamfahamu na kumfuata Kristo Kimamilifu.

Hao waislam wanaoamua kumkiri na kumfuata Yesu Kristo, wakiwa katikati ya watu wanaomwona Yesu ni mwanadamu mwenzao sawa na wao, na bado wakasimama imara katika neno ka Bwana, wanakuwa na imani thabiti kuliko tio wakristo katika mazingira yasiyo na tishio lolote.

Ifahamike kuwa kwa mataifa mengi haya ya waarabu, kumtambua Yesu Kristo kama mwokozi, au kuukana uislam, ambao kimsingi unamtweza Yesu Kristo, adhabu yako ni kifo.

Mathayo 28:18-20​

Yesu akaja karibu, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”
 
Utasubiri sana. Mimi najiandaa kunyakuliwa na Yesu, soon na kwenda kwenye arusi kubwa ya kifahari. Kama hukupata mwaliko wa arusi, huu hapa.
min -me umepata mwaliko wa bwana harusi ? 👆
 
Kuna mikutano ya Injili mingi sana vijijini. Isitoshe kuna wahubiri wanaopita nyumba kwa nyumba wakitangaza habari za Yesu. Kwa vyovyote vile atakuwa amesikia. Mwambie asikawie kutubu na kumwamini Yesu. Ni neema kuishi na kuufikia ubibi.
Lakini sisi tumeisikia injili ila tumeona haina jipya ni porojo tu
 
Wazungu wapo very positive kwa wale wanao silimu na kuingia katika uislamu. Unakuta anafuatilia kabisa in and out

Tangu mwanzo, wanasema hakufa wala hakufufuka. Tena wanasema Yesu sio Mungu wakati ushahidi upo mwingi

Yesu mwenyewe anasemaje kuhusu Mungu ili tuondoshe utata
Marko 12:29
“Sikiliza Ee Israeli Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja".

Je Yesu ni mjumbe au Mungu
Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma”.

Kwa andiko 👆🏽madai ya Yesu ni Mungu unapingana na andiko hilo ?

Mungu ana mamlaka kuliko Yesu
Yohana 14:28
“Baba ni mkuu kuliko mimi".

Kwa andiko hilo👆🏽 Yesu yupo chini ya mamlaka ya Mungu

Na hapa andiko linaonyesha Yesu akimuomba Mungu
Mathayo 26:39
“...akaanguka kifudifudi, akaomba akasema Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke...”.

Na hapa Yesu hakujua saa ya mwisho akiashiria kunyenyekea kwa Mungu
Marko 13:32
“Lakini kuhusu siku hiyo au saa hiyo hakuna ajuaye... wala Mwana ila Baba peke yake".
 
Tangu mwanzo, wanasema hakufa wala hakufufuka. Tena wanasema Yesu sio Mungu wakati ushahidi upo mwingi
Na hapa utasema Uislamu umekosea kuwa Yesu siyo Mungu
Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma".
 
Achana na huyo mgonjwa wa akili,

Upweke pia unamtesa sana,anatafuta faraja JF kwa nyuzi za kijinga jinga tu na mambo ya kufikirika.
Soma afu potezea km haijakugusa,hachana na kometi zisizo na hekima.
 
Nendanae kwa taratibu tu usimpeleke puta 🙏🏽
Usipoteze time yako bure kwa huyo mtu,
Hawa lengo lao hua nikukashifu Uislamu,usijiongopee nafsi yako eti utamfahamisha na atakubaliana na wewe au kukuelewa,

Lengo lao kuu hua sio kutaka kujua bali ni kukashifu.
 
Alafu jf uongozi wake sijui ukoje Leo nimeanzisha Uzi wa kufundisha kuhusu Uislamu wameufuta.
 
Back
Top Bottom