Mbona anafanya harakati zake kwa kushambulia wenzake wanaofanya zao kupitia vyama vyao?
Anapanga , anaamua anaweka ratiba na kupelekea wengine ili wafuate alichoamua.
Yeye na kichwa chake ndiye Halmashauri kuu, ndiye Kamati ndogo ya Halmashauri Kuu, Yaye ndiye Kamati Kuu. Wenzake wana uzoefu, yeye bado ni toddler.
Anayoyataka sasa wenzake walishayafanya mara nyingi tu back then.
Anapaswa kujifunza kujadiliana na kusikilizana pia awe tayari kupoteza.
Ili jambo lako lifanikiwe haupaswi kuwa mbinafsi.
Unaweza ukawa na vision, mission na objectives zako nzuri tu, ukishakaribisha watu ili mshirikiane, wataanza kuzipangua ibjectives moja mpaka nyingine, wataingia kwenye mission kote watasambaratisha, muda wote unatakiwa uwe mvumilivu, as long as Vision is still intact.
Sasa watu ukigusa tu objective ya kwanza, vita inaanzia hapo, maana kwenye objectives mdipo kwenye ulaji (pesa), ndipo kwenye ujiko (visibility) , ndipo penye connections, kwa kifupi pana vitu vingi vya kuweza kumpa mtu vingi na kubadili kabisa maisha yake binafsi huku vision , wakati mwingine vision vikibaki vipovipo tu.