Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono

Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono

20231002_192528562.jpg

Saa ya ukombozi ni sasa!!
 
Mimi pia naunga mkono hizo harakati. Ila aipendezi kukebehi wengine wenye harakati zao.

Kwa bahati mbaya "kukebehi" kumekaa ki hisia zaidi. Kwanini tusijikite kwenye hoja, Yaani ya msingi?

Wakati huo huo tukawa na namna nyingine bora zaidi ya kusuluhisha chochote tunachodhani kuwa ni kebehi?
 
well said! Slaa kamwe msimwamini, kama alishiriki ukandmizaji wa magufuli, huyo ni takataka. Maria shangazi nimeanza kumdharau kwa mbali, maana she can not intergrate and differentiate issues! Slaa siyo wa kuandamana naye! Nilisema na kuuliza swali, Je, kama Ubalozi ungeliendelea, angelikuwa katika kundi lao?
Inatuonyesha wazi UIMARA wa Dr. Slaa ulivyo na alivyo tishio kwa wale wasio tayari kuachana na ulaghai uliozagaa karibia nyanja zote, ulioshika mizizi na umekomaa, unaoitesa nchi kwa sasa.
 
Mwabukusi,Slaa na Mdude wameamua kwenda Mbeya na sisi CHADEMA tutakuwa huko.

Samia kapanick hahaha...

Kwenda Mbeya kwa waungwana hawa ni kukomaa kisiasa, kama ambavyo haipaswi kuacha kuungwa mkono jitihada zozote za vitendo kudai Katiba mpya bila kujali mwasisi wake.

Agenda ni vyote. Si personalities. Kwani tunatafuta wachumba?

Katiba mpya haitapatikana majukwaani. Katiba mpya haitapatikana kwa maneno matupu. Katiba mpya itapatikana kwa vitendo.
 
Ninaamini unajua tumedhamiria kweli kweli. Hii si ngoma ya vyama. Ushauri wote unakaribishwa.

"Maneno matupu hayavunji mfupa.

Kina Mwabukusi wanastahili kuungwa mkono, siyo kubagazwa."

Walipo tupo!
"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya UWT kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

Nimeiona hii. Jee wewe umeiona? Una maoni gani?
 
Jitihada za kina Mwabukusi ni zenye mlengo wa kuwakabili maadui zetu kwa vitendo.

Kina Mwabukusi hawaongelei agenda za vyama. Kina Mwabukusi wanaongelea agenda za wananchi.

Nini kilicho bora kuliko agenda za wananchi?

Ikumbukwe ukombozi hauhitaji watu wote:

View attachment 2773394

Hapa ndipo zilipo tofauti zetu na kwingine pote.

"Mwoga yeyote asitwambie watanzania ni waoga. Mwoga yeyote asitwambie sisi ni tofauti na Kenya."

Tuwakumbushe waoga hawa kuwa Kwingine hawana urafiki wala uadui wa kudumu. Pia kwingine, na vigogo huwepo kwenye maandamano.

"Kwamba hakuna katiba mpya, hakuna chaguzi? Hiyo ndiyo agenda yetu peke ya turufu kwenye mustakabala wetu kama taifa, na inawezekana."

Jambo la kheri ni kuwa, vuguvugu la kina Mwabukusi limetuonyesha nani ni nani baina yetu.
sasa unadhani kwa kauli za dharau walizonazo dhidi ya makundi mengine ya kisiasa na kiraia kuna mahali watafiki kwa hapa TZ?

si watabaki hivyo hivyo watatu yaani Mwambukusi, Dr. Slaa na Mdude labda na wewe ingawa pia utawakimbia mwanzoni
 
"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya UWT kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

Nimeiona hii. Jee wewe umeiona? Una maoni gani?

Haya yalikuwa maneno yako:

"Ni sawa, ila lazima tuone kwa vitendo na sio maneno matupu. Binafsi sijaliona hilo ila bado nangojea. Nilishauri nini cha kufanya. Huenda wahusika bado wanatafakari."

Bila shaka hujayasahau. Au umebadilisha mawazo?

Nikurejee sasa kwenye hoja zako mpya:

"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya UWT kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

UWT ni nani? Mengine yote uliyoandika hapo ni ramli chonganishi zile zile za ma CCM na vibaraka wao.

Mimi nikidhani kuwa wewe ni kibaraka wa CCM kudhoofisha damira za wananchi, utasema je?

Kuhisiana hakutatufikisha popote ndugu.

Kuna misahafu inasema:

"Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La!"

Sasa hapo taabu iko wapi? Kumbe kulikoni kuanza kuandikia mate au hIzi ramli chonganishi zitatufikisha wapi?

Nimeiona hii. Jee wewe umeiona? Una maoni gani?

Hiki sasa si kichekesho? Kwani wewe ni Mola, malaika, jini au shetani, au wao kuyajua ya kwao ukiwa Kizimkazi Zanzibari, huko?

Wewe kama ni binadamu tu kulikoni kumsemea mtu ambaye hajasema hivyo na kwa hisia zako tu?

Tusimame na tuhoji katika hoja zao. Kushukiana uchwara huku ni kwa faida ya ma CCM tu.

Kushukiana hakuna lolote la faida. Kumbe nani atakuwa salama basi.

Hayo ndiyo "majungu" sasa.
 
sasa unadhani kwa kauli za dharau walizonazo dhidi ya makundi mengine ya kisiasa na kiraia kuna mahali watafiki kwa hapa TZ?

si watabaki hivyo hivyo watatu yaani Mwambukusi, Dr. Slaa na Mdude labda na wewe ingawa pia utawakimbia mwanzoni

Ziweke hapa kauli hizo tuzione. Itapendeza pia kuziona kama zinaharamisha agenda zao.

"Egoism" haitatufikisha popote.
 
Ziweke hapa kauli hizo tuzione. Itapendeza pia kuziona kama zinaharamisha agenda zao.

"Egoism" haitatufikisha popote.
sawa tutawaona mnaposonga mbele kujiona bora na wema zaidi ya wengine,

muda utasema ikiwa nanyi ni watetea wanyonge au matonge.....
 
Chadema wanaona wivu eti watawapaisha akina Mwabukusi endapo wataunga mkono maandamano. Shabash!!!!

Mkuu tofautisha chawa na wazalendo wamo wazalendo wengi tu mle ..
 
sawa tutawaona mnaposonga mbele kujiona bora na wema zaidi ya wengine,

Nani kajiona bora au mwema zaidi? Kwamba kumbe kuna u star unao au mnao u mind mno hapa?

Watu wa namna gani nyie?

muda utasema ikiwa nanyi ni watetea wanyonge au matonge.....

Kuna hili la "sisi," kwani uko katika kum address nani kumbe?

Basi hata tuseme hata kama ulimaanisha "wao," yaani kina Mwabukusi, kulikoni kutokukaa angalau hata kimya tu, kama kuwatia moyo au kuwaunga mkono huwezi au hamuwezi?
 
UWT ni nani? Mengine yote uliyoandika hapo ni ramli chonganishi zile zile za ma CCM na vibaraka wao.

Mimi nikidhani kuwa wewe ni kibaraka wa CCM kudhoofisha damira za wananchi, utasema je?
Kwanza tuweke kumbukumbu sawa. Maneno niliyoyanukuu ni kichwa cha habari cha mwana JF Uzima Tele alichokiweka leo milango saa 10 jioni. Ndo maana nikakuuliza ikiwa umekiona na hivyo si maneno yangu. Maneno yangu yamo kweny swali "umeiona hii?"
Baada ya utangulizi huo nirudi kwenye mada. Mimi nilidhani ungekuja kwenye mada yako na mjadala wangu. Kwamba ungeniambia kwamba umeiona au la. Ni bahati mbaya wakati kama huu mambo huwa mengi hivyo yanahitaji utulivu.
Mimi nirudie tu lile swali langu la kwamba umeiona? Na nini maoni yako? Ukijua kwamba hiyo habari sio yangu.
 
Mkuu ni kweli mambo ni mengi na hivyo nikiri sikuwa nimekufahamu kabisa.

Hapo ndipo uone mshangao wangu ulivyokuwa ndani ya ufahamu wangu huo mdogo kuhusiana na ulichoandika.

Sasa nikurudie kwenye hoja hii:

1. Huko "uzima tele" wala sikuwahi kukusikia. Tafadhali niwekee link. Fahari ya macho au vipi?
2. Kukujibu kuhusu maoni yangu, waziwazi ni kama nilivyokujibu kwenye hoja zangu zile:

"Kuhisiana hakuna nafasi katika mapambano. Tena kusipewe nafasi."

Tuwahukumu watu kutokea kwenye hoja na matendo yao si hisia zetu kwani hayupo aliyekuwa supernatural.
 
Mwabukui aligombea ubunge akakosa...means naye ni mchumia tumbo tu kama wengine........... akipata madaraka huwezi jua atakuwaje......kama anagombana na akina Chadema wakati lengo lao ni moja, basi ujue ni takataka tu kama Slaa

Movement ya kina Mwabukusi Ina watu zaidi yake. Kulikoni makasiriko yote haya dhidi yake? Kugombana na Chadema ni kupi?

"Uko kama kakuchukulia tonge mdomoni ndugu?"

Pambana na hoja zake, si yeye kama binadamu. Huo ndiyo ulio ustaarabu.
 
Back
Top Bottom