Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo nchi yako maskini na viongozi wanajali wao tu wajipimie urefu wa kamba.......kule walikoendelea walimu ni highly paid profession.Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
😅😅😅 tena hayawahusu!KhaaTuache...tumeridhika na hali yetu.
Jamaa ni wajinga sana.Ni kweli kabsa walimu wengi huwa mbumbu sijui kwanini, utakuta anakimbizana ni kipindi huku mfukoni hakuna kitu.
wajinga hao,ndiyo wanakufundishia mwanao!Real?Jamaa ni wajinga sana.
Mimi mlinzi wa taasisi moja hivi ya serikali. Posho ya headmaster ambayo ni laki 2 Mimi napewa hiyo kama nauli.
Bado posho zingine , badala ya kudai haki zao wao wanajiona sehemu ya serikali
Ukijiuliza kwanini wapishi wengi ni maskini utapata common factor kuwa wote ni walishaji mmoja analisha akili mwingine mwili lakini hawana thamani kabisa.Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Umasikini upo kichwani mwako jiongezeni fursa kibao.Nunua ardhi panda miti ya mafuta mfano mlonge, muarobaini,nyongo,tengeneza sabuni na mafuta ya kujipaka uza kwa Jamii inayokuzunguka.Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Mna laana.Kataeni kusimamia chaguzi za kihuni ili muwapendelee CCM!pMtakalia kuuza visheti na kalimati Hadi mjute.😝😝😝😝Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Engineer s,lawyers,Kwani kada ipi ina matajiri tuu.? Wewe haupo sawa. Maybe unakaribia kwenda mbinguni!!
Upo sahihi, kwa mwalimu mwenye degree anaeanza ni 430,000. Sasa hiyo ukigawa kwa siku 30 exactly per day unaingiza 14,333/=Mimi sio mwalimu ila nadhani zifuatazo zinaweza kua ni sababu kwa kiasi kikubwa;-
- Mishahara midogo. Kada ya ualimu ni miongoni mwa kada zenye mshahara midogo ukilinganisha na kada nyingine. Nakumbuka mwalimu mwenye shahada gross salary yake ni 730,000 sasa hii ikikatwa inabaki almost 400,000k. Gharama za maisha yani nyumba, nauli, usafiri, ada za watoto, umeme, chakula, n.k inakua ni shida.
- Kukosekana kwa posho. Katika maofisi mengi kumekuwepo na posho mbali mbali na watumishi wengi wananufaika sana na hizi posho. Mojawapo kubwa kabisa ni posho ya kazi za ziada. Yani ukifanya kazi kuzidi masaa yanayokubaliwa kiutumishi unakua subject to compensation. Ila sasa huko kwa walimu hakuna posho ya over time, hakuna house allowance, hakuna transport allowance etc. Kukosekana kwa hizi posho kunafanya walimu waishi mshahara to mshahara. Na kwakua mshahara ni mdogo, wanajikuta katika ukata
- Kukosekana kwa safari. Kwenye maofisi mengi kuna vijisafari safari vya hapa na pale vya training, workshops, seminars, technical commitees na kadhalika. Safari katika kada ya ualimu ni chache sana na unakuta wanachaguana mkuu wa shule au makamu wake au academic officers. Ndani ya miaka mitatu possibility ya mwalimu kusafiri na kulipwa per diem ni ndogo sana na safari yenyewe utakuta ni ya muda mfupi haizidi wiki.
- Kukosekana mianya ya kupiga dili. Walimu wateja wao ni wanafunzi. Hakuna dili yoyote hapo. Kwanza elimu ya siku hizi ni bure. Hakuna motisha wala hakuna mzazi atakupa laki mbili kama zawadi kwa kumfundisha mwanae vizuri. Kuna watu huko bandarini wana mijengo Mbweni kwa hizi dili ndogo ndogo za hapa na pale.
- Kutochangamka. Walimu wengi hua hawako sharp kwenye harakati nyingine za kimaisha ukiachana na kazi. Wengi wanakua busy kukimbizana na wanafunzi unakuta mtu yuko job had saa kumi na moja jioni anawapa wanafunzi wachelewaji adhabu wakati huo hana hata genge la kuuza nyanya pale home au wanafunzi watano wa kupiga pindi after work.
Nimechokoza mada