cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Point ya 5 uko sahihi sana, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mimi sio mwalimu ila nadhani zifuatazo zinaweza kua ni sababu kwa kiasi kikubwa;-
- Mishahara midogo. Kada ya ualimu ni miongoni mwa kada zenye mshahara midogo ukilinganisha na kada nyingine. Nakumbuka mwalimu mwenye shahada gross salary yake ni 730,000 sasa hii ikikatwa inabaki almost 400,000k. Gharama za maisha yani nyumba, nauli, usafiri, ada za watoto, umeme, chakula, n.k inakua ni shida.
- Kukosekana kwa posho. Katika maofisi mengi kumekuwepo na posho mbali mbali na watumishi wengi wananufaika sana na hizi posho. Mojawapo kubwa kabisa ni posho ya kazi za ziada. Yani ukifanya kazi kuzidi masaa yanayokubaliwa kiutumishi unakua subject to compensation. Ila sasa huko kwa walimu hakuna posho ya over time, hakuna house allowance, hakuna transport allowance etc. Kukosekana kwa hizi posho kunafanya walimu waishi mshahara to mshahara. Na kwakua mshahara ni mdogo, wanajikuta katika ukata
- Kukosekana kwa safari. Kwenye maofisi mengi kuna vijisafari safari vya hapa na pale vya training, workshops, seminars, technical commitees na kadhalika. Safari katika kada ya ualimu ni chache sana na unakuta wanachaguana mkuu wa shule au makamu wake au academic officers. Ndani ya miaka mitatu possibility ya mwalimu kusafiri na kulipwa per diem ni ndogo sana na safari yenyewe utakuta ni ya muda mfupi haizidi wiki.
- Kukosekana mianya ya kupiga dili. Walimu wateja wao ni wanafunzi. Hakuna dili yoyote hapo. Kwanza elimu ya siku hizi ni bure. Hakuna motisha wala hakuna mzazi atakupa laki mbili kama zawadi kwa kumfundisha mwanae vizuri. Kuna watu huko bandarini wana mijengo Mbweni kwa hizi dili ndogo ndogo za hapa na pale.
- Kutochangamka. Walimu wengi hua hawako sharp kwenye harakati nyingine za kimaisha ukiachana na kazi. Wengi wanakua busy kukimbizana na wanafunzi unakuta mtu yuko job had saa kumi na moja jioni anawapa wanafunzi wachelewaji adhabu wakati huo hana hata genge la kuuza nyanya pale home au wanafunzi watano wa kupiga pindi after work.
Nimechokoza mada
Wanaboa mno.