Upo sahihi, kwa mwalimu mwenye degree anaeanza ni 430,000. Sasa hiyo ukigawa kwa siku 30 exactly per day unaingiza 14,333/=
Sasa hicho ni kipato cha mtu wa kawaida sana ambaye ukimuona mtaani utamdharau mfano mchoma mahindi au bodaboda.
Kinacholeta mwalimu afeli maisha na mchoma mahindi atoboe ni life expenses.
Hapa mwalimu atataka apange nyumba ya laki kwa mwezi, kiwi kila siku, msosi nyama kwa sana. N.k
Lakin huyu dereva boda atapanga chumba cha 30 elfu na maisha ya kawaida ndo maana ataweza kutoboa maisha na kuongeza kipato.
Ushaur kwako mwalimu, jiongeze kwa huo mshahar wako, ile jion pika uji tembeza au supu kwa maeneo ya mjini ila kwa vijijn unaweza ukalima mazao mbalimbl ya muda mfupi na kwa malengo ya muda mrefu nenda Iringa huko panda miti ,patachichi, chai n.k baada ya miaka kadhaa we ni don.!