Kwanini Walimu wengi ni maskini hapa Tanzania?

Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Tatizo nchi yako maskini na viongozi wanajali wao tu wajipimie urefu wa kamba.......kule walikoendelea walimu ni highly paid profession.
 
Ni kweli kabsa walimu wengi huwa mbumbu sijui kwanini, utakuta anakimbizana ni kipindi huku mfukoni hakuna kitu.
Jamaa ni wajinga sana.
Mimi mlinzi wa taasisi moja hivi ya serikali. Posho ya headmaster ambayo ni laki 2 Mimi napewa hiyo kama nauli.
Bado posho zingine , badala ya kudai haki zao wao wanajiona sehemu ya serikali
 
Aise, swala la maisha inatokana na uelewa mdogo wa mtu,walimu Wana mda mkubwa Sana wakufanya mambo Yao binafsi yaani biashara,mfano,wao hutoka shuleni saa 8 au saa 9 mchana,huu no mda mkubwa Sana Kwa mtu ambae Yuko sharp,sasa tatizo la walimu wengi ni wamejaa majungu,Fitina,wivu nk. Wanaoenda madaraka ambayo hayana posho, yaani ukiwa labda Mwalimu wa nidhamu unataka uabidiwe,unashinda mda mrefu kazini uendelee kulinda hako kanafasi ambako hakana hata posho yyte.
Pia,walimu wengi huwezi kuwakuta sehemu za starehe ambapo kuna "big boys".but waliochangamka Wana pesa nzuri mjini
 
Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Ukijiuliza kwanini wapishi wengi ni maskini utapata common factor kuwa wote ni walishaji mmoja analisha akili mwingine mwili lakini hawana thamani kabisa.
 
Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Umasikini upo kichwani mwako jiongezeni fursa kibao.Nunua ardhi panda miti ya mafuta mfano mlonge, muarobaini,nyongo,tengeneza sabuni na mafuta ya kujipaka uza kwa Jamii inayokuzunguka.
Pesa tele ukiwa na akili,mikopo tele,
 
Kati ya watu wanaongoza kugawa riziki ni walimu
 
Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Mna laana.Kataeni kusimamia chaguzi za kihuni ili muwapendelee CCM!pMtakalia kuuza visheti na kalimati Hadi mjute.😝😝😝😝
 
Unachukua Mkopo unajenga madarasa, unaanza Mdogo mdogo primary school wakilipa ada unajenga madarasa baada ya miaka 10 una bonge la shule. Mungu akupe nn
 
Ngazi gani msingi au secondary au veta
 
Upo sahihi, kwa mwalimu mwenye degree anaeanza ni 430,000. Sasa hiyo ukigawa kwa siku 30 exactly per day unaingiza 14,333/=
Sasa hicho ni kipato cha mtu wa kawaida sana ambaye ukimuona mtaani utamdharau mfano mchoma mahindi au bodaboda.
Kinacholeta mwalimu afeli maisha na mchoma mahindi atoboe ni life expenses.
Hapa mwalimu atataka apange nyumba ya laki kwa mwezi, kiwi kila siku, msosi nyama kwa sana. N.k
Lakin huyu dereva boda atapanga chumba cha 30 elfu na maisha ya kawaida ndo maana ataweza kutoboa maisha na kuongeza kipato.
Ushaur kwako mwalimu, jiongeze kwa huo mshahar wako, ile jion pika uji tembeza au supu kwa maeneo ya mjini ila kwa vijijn unaweza ukalima mazao mbalimbl ya muda mfupi na kwa malengo ya muda mrefu nenda Iringa huko panda miti ,parachichi, chai n.k baada ya miaka kadhaa we ni don.!
 
Wewe sio Mwalimu, mbona tunawaona wenyewe wana-enjoy tu. Wanajenga, wanaonesha watoto wao. Tafuta pesa acha kuwewesuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…