Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

Biology , English na Kiswahili ni masomo ya Lazima Tech. schools.
Hizi shule za technical zinaua talents za watoto maana pale utasoma ufundi kumbe huyo mtu angesoma shule za kawaida angekuwa mwanasheria mzuri au mchumi mzuri ungeandaliwa mfumo mzuri wa kuwapata wale watoto wenye talents za ufundi ndiyo wapelekwe huko siyo kulazimisha watoto kusoma ufundi
 
Apo sidhan kama itakuwa sawa, maana kuna watu primary wanakuwaga vipanga wa mahesebu wakifika secondary wanachemka vibaya sana, na ushahid wa washikaji zangu wengi tu

Hamna cha ushahidi hao hawajaandaliwa tu, wangekuwa vizuri kuna namna tu uzembe unafanyika unazima ndoto za wanafunzi wengi tz
 
Unaruhusiwa kumuamisha mwanao Mkuu..

Ila hakuna elimu bora duniani kama inayopatikana shule za ufundi.
 


Kwani hayo makundi ya chakula ni lazima aje afundishwe darasani?
 
Unaruhusiwa kumuamisha mwanao Mkuu..

Ila hakuna elimu bora duniani kama inayopatikana shule za ufundi.
Hizi shule kwasasa hazina kitu performance ya hizi shule ni mbovu alafu watoto wanaotoka huko kichwani ni weupe tofauti na miaka ya nyuma Ukisikia mtu katoka Moshi tech au Musoma tech unakuta kweli kichwani anakitu anakijua ata kujiajiri anaweza ila siku hizi ni Magofu ya majengo na mashine chakavu zilizopitwa na wakati
 
Lengo la mwanafunzi wa O'level kusoma masomo yote nikupata foundation knowledge ya somo husika ebu fikiria mtoto atakapoanza kidato cha kwanza asisome biolojia
Mimi ninazungumzia Physics na Chemistry wewe unaleta story za Biology. Kwani ni nani hajui kuwa Biology ni somo la lazima?...
 
Hayo masuala ya Sayansi (Fizikia na Kemia) si amesoma tayari huko shule ya msingi kuanzia darasa ka kwanza mpaka la saba, tena kwa lugha mama ya Kiswahili, na amekwisha elewa sasa aachana nayo akiingia kidato cha kwanza yasimpotezee muda wake.
 
Ndio hivyo mkuu, ikiwezekana hata wakianza darasa la 5 sio mbaya kwa maana akili zinakuwa zimekomaa kidogo...
Naunga mkono hoja PCB ianze darasa la tano hapo msingi mzuri utakuwa umejengwa.
 
Unaongea kama maCCM...

UNAJIANDIKIA TU.
 
Umefanana nao akili.
Huyo jamaa Kurutu wa Mungu ameropoka sana humu, na kuna kitu niliandika katika andiko langu kuu naona lilifutwa na hao jamaa zake ndio yeye akapata nguvu ya kuja na ile hoja yake ya somo la Biology.
 
Sasaivi wanafunzi wote wanaoanza wanafundishwa physics na chemistry ya form 1, hii inasaidia katika maisha.. Mfano topic kama za fire, combustion and mixer... Hii wanafunzi wote wanahitajika kufaham namna gani watakabiriana na majanga ya moto...sasa kama ikitokea mwanafunzi anaanzia kidato cha kwanza tayari yupo masomo ya biashara au arts unategemea hiyo topic ataipata wapi??
 
Fizikia kemia na bailojia ianzie LA saba ILI watakaofaulu wakaisome kidato cha 1 ngoja ndali mkaa arudi tuanze kazi ya kufumua mfumo mzima Wa helimu bure Bure
... lengo la mitihani ya F2 sio tu kuchuja wale wenye uwezo hafifu bali pia kuwawezesha wanafunzi kufanya maamuzi sahihi ya masomo gani ya kuendelea nayo kwani ndani ya miaka miwili waliyojifunza wanakuwa wameshaelewa hatma ya kusoma au kutosoma kitu fulani; ni kipindi muhimu cha kufanya maamuzi ya maisha yao ya baadaye. STD7 bado ni underage kufanya maamuzi ya aina hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…