Kwanini wanajeshi wanapenda sana kukopa vitu ovyo?

Hii imekuwa kero sana baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakikopa madukani na hawarudishi vitu na pengine hutumia ubabe wao kutokulipa hata unakuta ukimpeleka polisi ana achiwa tu maana hutumia kazi yao kujiona wakubwa kwa wenzao yaani wanapewa pesa kubwa kila mwezi lakini huishia kwenye pombe na kukopa hovyo sana wanajeshi badilikeni
Unafikiri wanayaona mambo kama unavoyaona!!?

Unafikiri mbuzi akimuona nyoka image anayopata ni sawa na ya kwako!?!?

Jaribu kufikiri!
 
Mkuu zinazokuja na mishahara ni za watu wa afya ila kwa majeshi wanapoozwa katikati..ulizia hapa jf utapewa jibu maana mtu kumuulizia nje ya hapa atakuona unamchora
Aisee sijui ni kwambie nini ila nina uhakika na ninachoongea. Nawazungumzia maafisa wa jwtz. Labda kama unaongelea wengine.
Posho zao..nyumba, maji nk zinakuja mwisho wa mwezi pamoja na mshahara.
 
Kuwa na adabu na wanajeshi wetu. We unazungumzia wa zamani. Wa kisasa wana elimu zao na wanalipwa vizuri.
**** Madaktari, wanasheria, Engineers, Land officers, Architects, nurses, Geologists, Walilmu n.k

Hawa wote wanalipa almost double salaries kwa majukumu yao ya Kitaalum then maslahi ya kijeshi
Mwache akariri huyo, Kila kada zina watu aina mbalimbali tu ambao uki generalize unatoa hitimisho hilo.

Watovu wa nidhamu wapo tu kila mahala jeshini kwa sasa mambo mengi yapo tofauti watu wameamka mno.
 
Hii imekuwa kero sana baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakikopa madukani na hawarudishi vitu na pengine hutumia ubabe wao kutokulipa hata unakuta ukimpeleka polisi ana achiwa tu maana hutumia kazi yao kujiona wakubwa kwa wenzao yaani wanapewa pesa kubwa kila mwezi lakini huishia kwenye pombe na kukopa hovyo sana wanajeshi badilikeni
Pole sana mkuu wamekuchukulia mke nini maana sio mapovu haya mkanye mkeo aache kuwashobokea watampiga mtungo
 
Mimi kuna mmoja namdai milioni 7, zilikuwa za kulipia mafundi site, nilisimamia nyumba yake na nimeshamkabidhi na amehamia tayari since 17 october mwaka jana.

Hilo deni la malipo ya mwisho lina mwaka sasa ni kupigwa kalenda tu, mbaya zaidi ni jirani yangu kabisa nyumba zinatazamana , nashindwa kumuwashia moto kutokana na huu ujirani.
Kuna project anataka kunipa, ndio imekuwa kisingizio kwamba tukianza project mpya ntakulipa kwanza deni lako ndio tuendelee.
Mi namuangalia tu...
 
Kuwa na adabu na wanajeshi wetu. We unazungumzia wa zamani. Wa kisasa wana elimu zao na wanalipwa vizuri.
**** Madaktari, wanasheria, Engineers, Land officers, Architects, nurses, Geologists, Walilmu n.k

Hawa wote wanalipa almost double salaries kwa majukumu yao ya Kitaalum then maslahi ya kijeshi
Ninaemdai mimi ni daktari sijui unaniambiaje sasa!!
 
Mimi kuna mmoja namdai milioni 7, zilikuwa za kulipia mafundi site, nilisimamia nyumba yake na nimeshamkabidhi na amehamia tayari since 17 october mwaka jana.

Hilo deni la malipo ya mwisho lina mwaka sasa ni kupigwa kalenda tu, mbaya zaidi ni jirani yangu kabisa nyumba zinatazamana , nashindwa kumuwashia moto kutokana na huu ujirani.
Kuna project anataka kunipa, ndio imekuwa kisingizio kwamba tukianza project mpya ntakulipa kwanza deni lako ndio tuendelee.
Mi namuangalia tu...
Mimi dukani kwangu wananifanyiaga ushenzi nawakopesha hawalipi yaani paka tunapelekana makazini kwao
 
Back
Top Bottom