Mwenye Uzi huu, nimesoma maelezo yako, nikagundua kirusi wa biashara yako, siyo wanajeshi, ila ni wewe mwenyewe.
Hivi kwanini duka lako wewe wateja wake wawe wengi ni wanajeshi; inamaana uko karibu nao, na biashara yako uliwalenga wao zaidi.
Ndiyo maana unawajua wateja wako kwa hiyo kazi yao, maana katika mazingira ya kawaida ni ngumu kujua kazi za wateja wako, labda kwenye miji midogo.
Mpaka kufikia kumkopesha mtu, inamaana unamjua na siyo kumjua tu kuwa huyu ni fulani, bali ni mteja wako.
Sasa una ulivyo kirusi, kwenye biashara yako, unajua jamii unayoishi nayo wakikopa hawarudishi, wewe una wakopesha, hata kama umesema ni wababe, Sidhani ukitaa kukopesha, wanaingia ndani na kujichukulia wenyewe.
Kama wanachukua bidhaa kwa nguvu, hata akili ya kuhamisha biashara eneo hilo imekushinda, ukaona ujisalimishe mtandaoni pole sana.
NIkujulishe tu, kila sehemu kuna wakopaji muhibu ni wewe kujiridhisha, kuhusu unae mkopesha, na huo mtaji wako.
Hata huku uswahilini tunakopa sana, ndiyo maana wakopeshaji wako wengi mpaka mtandaoni, simu ukipita kwa uzaji kwa sisi tunaishi Dar, wanakutanga mkopo hapo hakujui.
Hivyo jipange biashara siyo lelemama.