Kwanini wananchi Afrika siku hizi wanafurahia mapinduzi ya kijeshi?

Kwanini wananchi Afrika siku hizi wanafurahia mapinduzi ya kijeshi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kule Sudan, Burkina Faso, na kwingineko inaonekana wananchi wakifurahia mapinduzi haramu yanayofanywa na wanajeshi wanaoziondoa serikali za kidemokrasia badala ya kuchukia mapinduzi, hii ni tofauti sana na enzi za akina Nkrumah, Lumumba, na wengine wa aina Yao. Kumetokea nini?
 
Haki ni shida kupatikana... Hata ukienda Mahakamani ni shida kupata..
Hali hii inachochea watu wayatamani mapinduzi
 
Wajeda hawana hela.

Kule Guinea-Bissau sababu ni mihadarati. Ile nchi ni muhimu katika biashara ya mihadarati na uwepo wa Serikali inayotishia maslahi ya wauza madawa huwa inapinduliwa
 
Kwa maoni yangu ni kwamba wamechoshwa na uongo wa wanasiasa. Ahadi wanazotoa kabla ya kupewa madaraka hazitekelezwi badala yake wanafikiria tu kula kwa urefu wa kamba zao. Kibaya zaidi wengine huzidisha kula hadi kuvimbiwa wakati wananchi wakiganga njaa.
 
Leo asubuhi nilitumia usafiri wa umma kutoka gongo la Mboto kwenda kazini, eebhae!!! Wananchi wanapata tabu sio utani. Ukiona watawala wanapiga pesa badala ya kutatua kero za aina hii inachosha kidogo,
 
Baada ya mapinduzi kufanyika, je madhila ya wananchi yataisha? Au hali itakuwa vilevile? uncertainty principle.
 
Kule Sudan, Burkina Faso, na kwingineko inaonekana wananchi wakifurahia mapinduzi haramu yanayofanywa na wanajeshi wanaoziondoa serikali za kidemokrasia, hii ni tofauti sana na enzi za akina Nkrumah, Lumumba, na wengine wa aina Yao. Kumetokea nini?
Tawala za kiimla na kidiktetea zimerudi kwa kasi sawa.Wananchi hawana tena uwezo wa kutumia kura kuchagua viongozi wao.

Utakuta kiongozi mkuu wa nchi anateua tume ya uchaguzi yenye watu wake na anawapa maelekezo polisi wabane wapinzani.

Mwisho wa siku yeye anapata kura kwa asilimia 100 na anapata wabunge 100%.
 
Wajeda hawana hela.

Kule Guinea-Bissau sababu ni mihadarati. Ile nchi ni muhimu katika biashara ya mihadarati na uwepo wa Serikali inayotishia maslahi ya wauza madawa huwa inapinduliwa
Ingekuwa hivyo punda wasingelazimika kupañda ndege kwenda Brazil na India kupakia mzigo🏋️.
 
Tawala za kiimla na kidiktetea zimerudi kwa kasi sawa.Wananchi hawana tena uwezo wa kutumia kura kuchagua viongozi wao.

Utakuta kiongozi mkuu wa nchi anateua tume ya uchaguzi yenye watu wake na anawapa maelekezo polisi wabane wapinzani.

Mwisho wa siku yeye anapata kura kwa asilimia 100 na anapata wabunge 100%.
Yule wa Malawi mbona alishinda na Sasa nae anayafanya yaleyale aliyokuwa anayapinga akiwa nje?
 
Hili swala liko namna hii: Afrika tuna asili ya tawala za kitemi ambazo misingi yake mikuu ni utawala wa kibabe.

Sasa basi, mtu anapopewa mamlaka ya utawala anatawala kibabe kwa sababu lile jinamizi bado tunalo na linaishi miongoni mwetu,

Sasa nini kifanyike: tuendelee tu kufanya haya mapinduzi hadi pale hili jinamizi litakapoondoka kabisa, tusichoke kufanya mapinduzi kwa maana hatuna njia mbadala.

Hatuwezi kuwaondoa madarakani kupitia kisanduku cha kura kwa sababu ya mifumo haramu waliyojiwekea.

Long live military coups and no to African dictators,
 
Baada ya mapinduzi kufanyika, je madhila ya wananchi yataisha? Au hali itakuwa vilevile? uncertainty principle.
Bora hata hali ingekuwa inabaki vile vile, Bali hali huwa inakuwa mbaya zaidi.

Mfano Sudan Sasa hivi hali imekuwa mbaya zaidi hicho kipindindi cha Omar Al Bashir
 
Kule Sudan, Burkina Faso, na kwingineko inaonekana wananchi wakifurahia mapinduzi haramu yanayofanywa na wanajeshi wanaoziondoa serikali za kidemokrasia, hii ni tofauti sana na enzi za akina Nkrumah, Lumumba, na wengine wa aina Yao. Kumetokea nini?
Sudan walifurahia lakini sasa hivi wanakiona, hali imekuwa mbaya sana.
 
Unataka kujenga hoja gani hapO?
Afrika Kuna matatizo yanayotoka nje ya Africa, Tshishiked kule DRC sio kwamba nae anafanya vizuri kumzidi Kabila. Sio kweli kwamba Marais waliopinga uwepo wa corona kwenye mataifa Yao lazima wote wafe ghafla kama ilivyotokea kwa Tanzania na Burundi, hii so kweli, inawezekana Marais wote wanapokea amri, vitisho, na maelekezo kutoka nje ya Nchi zao.
 
Watu kufurahia mapinduzi chanzo chake hasa ni uvutaji wa bhange likaenda kuvuka mipaka likaleta madhila hayo!.
 
Afrika Kuna matatizo yanayotoka nje ya Africa, Tshishiked kule DRC sio kwamba nae anafanya vizuri kumzidi Kabila. Sio kweli kwamba Marais waliopinga uwepo wa corona kwenye mataifa Yao lazima wote wafe ghafla kama ilivyotokea kwa Tanzania na Burundi, hii so kweli, inawezekana Marais wote wanapokea amri, vitisho, na maelekezo kutoka nje ya Nchi zao.
Kwa hiyo unasema hakuna madekteta Africa ? KUWA ata Magu alikuwa anapokea maelekezo kutoka nje kukandamiza demokrasi?
 
Back
Top Bottom