Kwanini wanaoshuhudia miujiza kwa Mwamposa wengi ni waislam tena wanawake?

Kwanini wanaoshuhudia miujiza kwa Mwamposa wengi ni waislam tena wanawake?

Bwana Yesu asifiwe milele..hakika anazidi kuwafungua watu wake kutoka kwa minyororo ya shetani..

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787]
IMG_20210924_074847.jpg
 
Tabu ni pale unapinga wakati hujui kitu[emoji38][emoji38][emoji38] shuhudia hata kupitia tv tu ujionee mwenyewe na hata wangepangwa mbona watu kibao wanapona na wengine biashara zao zinafanikiwa nina ushahidi kabisa nilishuhudia watu
Bwana Choko na elimu yako unaamini yale yote unayoyaona ? Wenzako wote asilimia 90% wakupinge we ndio uko sahihi . Kuna msemo unasema "lisemwalo lipo kama halipo laja"

Statistics never lie ..
 
Nipo naangalia mahubiri kanisa la rise and shine naona wanawake wengi wa kiislam wengi ndio wanatoa ushuhuda wa kupitia magumu kwenye maisha

Kweli yesu ni jibu

USSR
"Kweli yesu ni jibu"


Nimekunukuu hapo Mungu ndio jibu mkuu sio nabii/mtume wake
 
tatizo gani mkuu??

maana Yesu alizurula kueneza injili,njiani akatenda miujiza.
hawa ndugu zetu kwa sasa wamekaa ktk mahekalu yao wanasubiri wagonjwa wawafate,na mahubiri ni kuhusu kufanikiwa kimaisha na mali.
Wakati umebadilika sana,watumishi wote wanapenda hela,isipokuwa misingi ya makamisa yao inawanyima uhuru kamili
Kwa hiyo waache waliowatafuta waumini kwa nguvu zao wale pesa
 
Kama una uelewa wa Marketing and Sales huwezi shtuka. Ushuhuda wa mkristo hauna mvuto si ajabu wakapangiwa siku nyingine ila sio siku yenye hadhara kubwa. Ushuhuda wa mwislamu ndio unauza mahubiri.
Hayajakukuta

Siku yakikukuta ndio utaamini kuwa wanaogopa au wana shida kweli
 
Acheni wafu wazike wafu wenzao,anaekwenda mwacheni aende na asiekwenda abaki aliko na Imani yake Wala hakuna haja ya kumsema anaekwenda kisa wewe huendi. Tujifunze kuheshimu Uhuru wa mtu jamani.
 
Bwana Choko na elimu yako unaamini yale yote unayoyaona ? Wenzako wote asilimia 90% wakupinge we ndio uko sahihi . Kuna msemo unasema "lisemwalo lipo kama halipo laja"

Statistics never lie ..
Mnaopinga nyote ni muslims but kwa mkristo anayejitambua hayupo kiivyo toka na mihemuko yako wewe
 
Hayajakukuta

Siku yakikukuta ndio utaamini kuwa wanaogopa au wana shida kweli
Sijakataa kuhusu huduma wanayoipata ila na huenda wanasaidika kwa uwezo wa Mungu. Mchungaji kusimamisha Muslim madhabau kwa ushuhuda inavutia zaidi hadhira kuliko akisimama Mkristo... Sijui tumeelewana!
 
Hiyo ni mipango tu ya kimjini mjini ili wateja wapatikane hapo hakuna muislam wala nini.
 
Hakuna hata mtoa ushuhuda ambaye keshapatikana kwa kudanganya kwa MWAMPOSA au KUHANI MUSSA, hawa watu tunaishi nao huku mitaani kwasababu haiwezekani mtu augue uchizi miaka 20 na anapoishi anapataja halafu watu wasifahamu...

Nafkiri la kujadiliwa ni NGUVU WANAZOTUMIA KUFANYA HII MIUJIZA ila ishu ya kupangwa mtu haina mashiko...
 
Mkuu ile inaitwa Stage Managed, yaani Kwenye Mikutano ya Jamaa wale wabao toa shuhuda ni watu kutoka sehemu nyingine kabisa.

Kama yuko Singida watakao toa ushuhuda lazima awachukue Mwanza, au Arusha au kwingine,
Kwahiyo na SURA nazo wanazibadilisha au? Maana TV yake iko STARTIMES na AZAM TV ina maana UKANDA wote wa Afrika Mashariki wanaangalia..
 
Back
Top Bottom