Kwanini wanaume huwa na michepuko?

Kwanini wanaume huwa na michepuko?

Dah! Hapa kuna bonge la maana, Asiekuelewa basi tena!

Kaongea kitu cha kizito na chenye ujumbe watu tunasahau ya kua hata kabla ya dini kujulikana wazee wetu ndo ilikua balaa wake mpka 10 anajimilikisha na ilikua sawa tu
 
ahahahahahaaa kama unaweza kuhudumia kwa kila siku na mara tatu za nguvu ila si ile ya kitoto mm nitavumilia ila kama n huo mgao wa umeme sahau kuchapuka n lazima mamamamamamamaamamamayeeeeee
 
men species... akili imevurugika sijui...hua siwaelewi...au upendo ndo umechakachuliwa... they never get enough..SITASHANGAA mume wangu akitoka nje japo ananipenda ,,tho it hurts...bt these species i dont understand them:confused2: uongo mwingiii... macho juu juu:blabla: ..... wachache sana wateule nawaita may be wapo.......any way... naacha tu ...hasa miafrika , mi tz...mi bongo...tumezidiii.. kucheat lol. sina maana huko wenzetu wanaume hawacheat, they do bt not to our level.. at least they are trying to be honest compared to us...:disapointed:

Ungehadisiwa ya babu wa babu yako na hali ya sasa ungeshukulu kabsaa
 
Uislam umeruhusu kuoa wake wengi kwa sharti.
1. Isizidi idadi ya wake wanne.
2.kufanya uadilifu baina yao.

"...BASI OENI MNAOWAPENDA KATIKA WANAWAKE (maadamu mtafanya uadilifu) WAWILI(2),AU WATATU(3),AU WANNE(4) TU.NA MKIOGOPA KUWA HAMUWEZI KUFANYA UADILIFU,BASI OENI MMOJA TU. ..." (4:3)

Faida za kuoa mke zaidi ya mmoja kwa upande wa mwanaume.

1.Inawezekana kabisa mkewe akawa hamtoshelezi haja yake ya kimaumbile,Hii husababishwa na uwezo mkubwa wa mume katika tendo la ndoa,na udhaifu wa mke.
Mume hataki kumuacha mke wake.
Sasa ataitosheleza wapi kiu yake?

Hapo ndipo Uislam ukamruhusu mume kuoa mke mwingine na yule wa mwanzo kubaki pale pale.

Lau kama Uislam usingemruhusu mtu huyu kuongeza mke mwingine ili kukidhi haja yake ni dhahiri kuwa mume angefanya moja kati ya mawili haya..

°Angemtaliki/angemuacha huyu aliyenaye, asiye kidhi haja yake na kuoa mwingine.
°Angekua na nymba ndogo (mwanamke wa pembeni/kimada) ili kukidhi haja yake.
NA HIKI NDICHO CHANZO CHA KUENEA KWA MAGONJWA YA ZINAA.

2.Kadhalika mwanamke anaweza kuwa tasa, hazai na mumewe anatamani kupata watoto,na ambalo hili la kupata watoto ni mojawapo ya malengo na madhumuni ya ndoa.na mumu anampenda mkewe kwa sababu moja au nyingine,na hataki kumuacha.

Sasa huyu mume afanyeje ili kuweza kupata watoto na kuendeleza kizazi cha binadamu?

Akazae nje ya ndoa?
Hapana! Hilo ni kosa,
Hapa ndio Uislam ukaziangalia haki za huyu mume kupata watoto,ukamruhusu kuoa mke mwingine,akajaribu bahati yake.
Huwenda mola wake akamruzuku watoto kwa mke huyu.

Haya ni baadhi ya maslahi ya mke zaidi ya mmoja kwa mwanaume.

FAIDA WANAZOPATA WANAWAKE KWENYE NDOA ZA MKE ZAIDI YA MMOJA.

1.Inawezekana mwanamke akapatwa na maradhi,akashindwa kabisa kuitekeleza haki ya unyumba kwa mumewe.
Maskini mke huyu mgonjwa, aende wapi,na hana uwezo wa kutekeleza haki ya ndoa?
na ilhali katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa ndio anahitaji zaidi huruma,mapenzi na liwazo la mumewe!

Mume amtaliki/amuache? La, hapana!
Sheria inambana mume kuwa katika mkataba wa ndoa alichukua ahadi ya kuishi naye kwenye shida na raha, uzima na ugonjwa.
basi amuuguze mkewe.na ili kukidhi haja yake ya kimaumbile, aoe mke mwingine.
Asichepuke.
Je,hapo mwanamke hajanufaika?

2.kadhalika kama binadamu wanavyotofautiana katika sura,tabia,akili nakadhalika.
Ni hivyo hivyo pia tunatofautiana katika uwezo/nguvu za kujamiiana.
Inawezekana kabisa uwezo wa mume ukawa ni mkubwa sana kuliko wa mkewe.uwezo wa mume ni kama tembo na uwezo wa mke ni kama kondoo.
Vipi,kondoo atahimili vishindo vya tembo?

Sasa ili mke huyu asiichukie ndoa yake,hatimaye kuikimbia,
Uislam ukamruhusu mume kuongeza mke mwingine.
Ili siku ya zamu ya mke mwingine,huyu asiyeweza kuhimili vishindo apate kupumzika.
Hebu tuwe wakweli,mwanamke huyu hajanufaika? Kanufaika?

Vile vile sheria hii ya mke zaidi ya mmoja ina maslahi makibwa kwa jamii.
Hakuna jamii isiyokuwa na wajane.ambao nao ni binadamu,wanahitaji kimaumbile nawao kujamiiana pia.
Vipi, wakazini? La,hapana,hilo ni kosa.

Pia kuna mayatima,ambao wanataka wapate uangalizi na malezi.

Hivyo basi, ni nani atawasitiri wajane waliofiwa na waume zao?
Nani atawaangalia na kuwalea hawa mayatima waliofiwa na baba zao?

Uislam ukampa RUHUSA mwanaume ambaye tayari ana mke,kuongeza mke mwingine.
Pengine atakaye muoa ni huyo mjane mwenye mayatima!

Je,mwanamke huyu hajasitirika?
Na wanawe hawajapata uangalizi na malezi?
Kwani huyu mume katika Uislam atakua na wajibu wa kumhudumia yeye na wanawe.

Hata waswahili wanasema,"ukipenda boga upende na ua lake"

Tuwe wakweli.
Je,hapa jamii imenufaika haikunufaika?

Pia ipo wazi,
Duniani idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume.na udadi ya wanyama jike ni kubwa kuliko wanyama dume(KAMA HUAMINI CHUNGUZA UTAGUNDUA).

Na kila binadamu ana haki ya kupenda/kupendwa katika jamii.
Anayo haja ya kimaumbile,ya kukidhi haja yake!

Je,wanaume wakioa mke mmoja tu, hawa wengine wakakidhi wapi haja zao?

Ndipo hapo wanapoanza kuvaa nusu uchi,ili waonekane.
Ndipo hapo wanapoanza kujiuza.
Ndipo hapo wanapogeuka michepuko( wezi wa waume za watu).
Ndipo magonjwa yanapoingia kwenye ndoa.
Ndipo mpango wa shetani wa kupunguza watu duniani kuelekea (new world order) unapoelekea kutimia.
UKIMWI TUSINGEUJUA!
 
Mbona nyie mnapokea hela toka kwa wanaume wengi..
 
Nimekuwa nikijiuliza kuhusiana na hii tabia ya wanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja hivi nini sababu? Au kwanini hamridhiki na mwanamke mmoja? Hili jambo limekithiri kwa sana.

Karibuni wakuu tujadiliane

Jina lako linareflect lililo moyoni
 
Kwa mume mtiifu kabisa na anayejali familia na kumpenda mkewe kwa mwaka inambidi achepuke mara nane tu. , ukiwa mvivu sana mara tano.
 
Nimekuwa nikijiuliza kuhusiana na hii tabia ya wanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja hivi nini sababu? Au kwanini hamridhiki na mwanamke mmoja? Hili jambo limekithiri kwa sana.

Karibuni wakuu tujadiliane

Mbona hata wanawake siku hizi nao wamo?hawariziki na mume mmoja?
 
Back
Top Bottom